Tafadhali usile chakula kabla ya kumshukuru Mungu na kukiombea

Tafadhali usile chakula kabla ya kumshukuru Mungu na kukiombea

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Kama ulikuwa hujui, kila kipande cha chakula tunachoweka mdomoni ni zawadi kutoka kwa Mungu. Maandiko yanatufundisha kwamba kila kitu kizuri hutoka kwa Baba wa nuru (Yakobo 1:17).

Hizi hapa faida za kushukuru na kuombea chakula:
1. Ni njia ya kumheshimu Mungu Mtoaji – Unaposhukuru, unatambua kuwa si kwa nguvu zako bali kwa neema yake umeweza kupata chakula (Kum 8:10). Mungu anapendezwa sana na watu wanaoshukuru.

2. Unajiletea baraka na ulinzi – chakula kinapoombewa, kinatakaswa na hivyo unapokea ulinzi wa Mungu dhidi ya madhara ya siri kama sumu au wadudu wabaya (1 Timotheo 4:4-5).

3. Kushukuru kabla ya kula kunakufanya uwe na moyo wa furaha na kuridhika na kile Mungu alichokupa, kiwe kidogo au kingi (Wafilipi 4:11-12).

4. Ni ushuhuda wa imani – Wengine wanapokuona unaomba kabla ya kula, unawafundisha kimyakimya kuhusu kumtegemea Mungu.

Kula bila kumshukuru Mungu ni kama kupokea zawadi bila kumshukuru aliyeitoa. Ni kujikosesha ulinzi wa kimwili na kiroho. Usipoombea chakula unaacha mlango wazi wa kupata madhara ya kimwili au ya rohoni yanayoweza kuondolewa kwa sala.

Mtu asiyeshukuru huanza kuamini kuwa kila anachopata kimetokana na juhudi zake mwenyewe, na moyo wake huingiwa na kiburi na kuelekea mbali na Mungu (Warumi 1:21).

Mifano ya walioshukuru na kuombea chakula:
Yesu Kristo
– Kabla ya kugawa mikate na samaki, alishukuru na kuombea chakula (Mathayo 14:19).

Paulo Mtume – Hata alipokuwa katika hatari ya meli kuzama, aliombea chakula mbele ya wote kabla ya kula (Matendo 27:35).

Waisraeli – Mungu aliwapa maagizo ya kumshukuru walipoingia nchi yenye mazao mengi (Kumbukumbu la Torati 8:10).

Huu hapa mfano wa Sala fupi ya kushukuru na kuombea chakula:

"Baba Mungu wa mbinguni, nakushukuru kwa kutupatia chakula hiki. Naomba ukibariki na kukitakasa, kilete baraka na afya njema katika miili yetu. Kwa Jina la Yesu, amina."
 
Mkifundishwa kidogo tusomo tu dogo dogo mnaona tayari mnaweza kuwa waalimu kwa wengine....nakuambia kuomba ni wakati wote...omba hata kama si wakati wa kula...Kila upatapo nafasi omba..maana shetani anawinda watu wakati wote si wakati wa kula tu...hata wakati wa kukiandaa chakula tu kabla ya kula...usinyamaze omba, hujawahi ona watu barabarani wanatembea wanatupa mikono njiani?? Kuna maneno wanatamka Kila wanapovusha hatua moja...yafanye ndio maisha Yako ya wakati wote🫣
 
Asante Mwalimu IQup kwa kufafanua. Somo la maombi ni pana sana. Mimi nimetaja kipengele kimojawapo tu cha maombi. Ila hao wanaoomba barabarani huku wakitupa mikono waambie wajihadhari wasiingie kwenye kundi la wanafiki. Waambie wasome:
Mathayo 6:5-6
“Nanyi mnaposali, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wao wamekwisha kupokea thawabu yao. Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye sirini atakupa thawabu yako."
 
Nimekwambia kama ni la siri, litaje tu bila kulifafanua. Kwa mfano sema: "Iombee familia yangu....Iombee kazi yangu....Au ninahitaji fulani la kibiashara...."
Mimi nitaomba na kumwambia Mungu ajuaye details zote za hitaji lako, atakupa.
Ila bado hujajibu swali langu: "Umeokoka?" Nina sababu muhimu ya kukuuliza swali hilo.
 
Wewe niombee. Mungu anayajua ya sirini. Mwambie anifanyie yote ninayoyataka
 
nahitaji me uniombee madame Setfree nikisha okoka tuwe wachumba
 
Wewe niombee. Mungu anayajua ya sirini. Mwambie anifanyie yote ninayoyataka
Nimekuuliza: umeokoka? Umekataa kunijibu. Kama umeokoka, unaweza kuomba mwenyewe jambo lolote utapewa.
Hii hapa ni ahadi ya Yesu mwenyewe:
Yohana 16:24
"Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu."
 
Back
Top Bottom