Tafadhali usivae hii bangili kwa kufuata mkumbo

Tafadhali usivae hii bangili kwa kufuata mkumbo

Vipi kwa wale ambao wanaaa kama urembo.
Alafu hii kitu wanapenda sana kuvaa madereva na mafundi,ukute hii kitu inafaida zake ila wewe umeamua kuja kututisha tu mkuu.
Ungeweka faida zake na hasara zake
Nakujibu kama hivi dereva wa malori wengi wanavaa hii baada ya kupewa maelekezo hii ni kinga ya ajali mkuu hajavaa kama pambo bali ni kinga tosha namaanisha hio bangili imepewa maelekezo fulani, kwa mfano bangili hii ikibana basi tulia maana hua inaashiria hali mbaya
 
Muulize baba ako huenda mimba yako ilitungishwq baada ya kuhuzzulia unaouita ushirikina, na serikali imetambuq mchango na sasa waroto wetu wanafundishwa wasijekuwa kama wewe hili soma linaitwa historia na maadili anyway fata wazungu tusikuforce
Mwanadamu akifa amekufa tu, tofauti na hapo ni kujivisha ukichaa kichwani.
 
Hivi mizimu za mababu ipo kweli au ni hadithi tu.. na tunathibitisha vipi?
Ndo inayokulinda wewe apo, chakufny onana na wakubwa zako sema vjn wa sasa hamna muda wa kuongea na babu zenu mko busy kubet tu shauri yenu
 
Nakubalina na wewe kuwa vitu vya urembo kama BANGILI ,PETE ,HERENI,hata midoli vinyago,nguo za fasheni zenye nembo nembo,hata vyakula tunavyoalikwa kula au kununu bidhaa za vyakula na mboga mboga sokoni..au gengeni..hata bidhaa za viwandani kama vinywaji n.k

VITU VINGI VINAWEZA kutumika na ulimwengu wa giza kama alama za uaminifu ..za Maagano..AGANO.. ya kiroho...ikiwemo hata vipindi tunavyotazama kwenye Tv,mtandao,na kusikiliza na kuona au hata ndotoni..
ikiwemo ibada za matambiko na makafara ya mabibi na mababu zako katika madhabahu za miungu ya ukoo hata kabla ya wewe hukazaliwa.

Sio lazima uvae physically unaweza ukawa umevaa bangili au pete katika mikono yako ya kiroho au mikoba uko nayo ya maagano na madhabahu za giza ndani yako hata kama katika ulimwengu wa mwili physically hujavaa chichote.

unaweza kuingia kwenye maagano au kuongizwa na watu kupitia damu ya ukoo mababu,au kuingizwa katika maagano kwa kutegwa katika vitu vingi hata chakula tu ,au ndotoni au .kulogwa..kukanyaga unyayo..kwwnda kwa waganga wa kienyeji..kuzini,uasherati,kupitia maneno unayotamkiwa au kutamka

Usipende kula kula ovyo ,usipende kuvaa vaa ovyo alama mbalimbali kwenye mavazi iwe nguo,viatu,zina maana yake na ni maagano,isovae vae MAPETE,MABANGILI ,mikufu...n.k
usipende kuweka mapambo kama midoli,vinyago vina madhara yake midoli..hata mawigi na nywele bandia ikiwemo marasta..na hereni..

wengi weingia katika maagano na ulimwengu wa giza bila kujua

OMBEA sali juu ya kila kitu sali muda wote Mungu atuepushe na mabaya yote ..
 
Poor mind

Mwili hufa roho hubaki afu nahisi hata dini hujui vizuri wewe, unaenda kutafuta videmu tu huko kanisani
Hatupo kwenye utani mkuu, neno la mungu linajiweka wazi, wafu hawaoni wala kusikia ni kama mshumaa unapozimika, je, huendelea kutoa nuru, fundisho la kwamba mwili hufa na kuacha roho ni mafundisho ya shetani na unapaswa kuyaepuka.
 
Kwanini usivae bila maelekezo ni kwamba hizi bangili hutegemeana na aina ya mizimu ya ukoo wenu kila ukoo au kabila linanizimu yake na hio mizimu inautaratibu wake sasa ikitokea wewe umenunua bangili ya gold wakati mizimu yenu inapenda shaba hapo ndo chanzo cha matatizo kwako wewe uchumi wako utaanza kudolola, matatizo kibao ,mikosi na mabalaa maana sasa unaingia vitani na wazee wako wa zamani kwamba unapingana na energy yao.
Mizimu ingekuwa inafanya kazi, Tanzania ingekuwa mbele kimaendeleo kuliko Japan
 
Mnaamini vitu ambavyo havipo na havina nguvu yoyote kwenye maisha ya binadamu
Muulize kwanza bibi yako huenda anayo hii , anyway fanya utafiti kisha njoo na hoja za kupingana na mimi sio comment kama hii
 
Katika uchawi na mapokeo ya kipagani, bangili za shaba hutumiwa kama zana zenye nguvu za kutengeneza nishati, kukuza nia, na kutoa ulinzi. Zikihusishwa na sayari ya Zuhura, huvaliwa kwa kawaida ili kuvutia upendo, urembo, na ustawi, na pia kwa kuweka msingi, uponyaji, na kuimarisha mawasiliano ya kiroho.
 
nakubali mabangili haya ya shaba na fedha ,hata mapete ,na vingine vingi vinaweza kutumika kama alama ya uamnifu ya maagano.

nakumbuka kabla nikiwa kwenye kilinge cha mganga wa kienyeji nilipombiwa nina mizimu 6 hivyo nikanunue bangili la shaba lenye mikunjo kuno na fedha kwa ajili ya mzimu anaitwa MIDIMI au mdimu

nikapewa na ushanga fulani wa kuvaa begani kama rubega ndani ya mwili ,na kaniki na vitu vingine ..(kukatisha stori)

bangili niliambiwa ndio ulinzi wangu.
nisiivue..ni ya mizimu.

nilipokuja kuokoka nilivitupa vyote ,na nikajua maana ya mizimu ni mapelo ya ukoo au majini ya ukoo yanayokuja kwa sura za marehemu waliokufa katika ukoo yanavaa uhusika wa marehemu na wajihi wake kama sauti ,tembea yake tabia zake kila kitu.Yanapenda kujitambilisha kama wazee au babu yako au bibi yako..au shangazi au mjomba n.k

ila kiuhalisia ni pepo siyo roho ya yule marehemu babu yako ila ni pepo
na yanakupa MASHARTI yakitaka uya ABUDU uyatokee sadaka matambiko na mashartii..unaakuwa mtumwa kwayo

siku ukifa yanakuja kuwatokea watito wako au wajukuu kwa sura yako..mzunguko unaendelea katika ukoo.

Shetani mizimu,majini..hana urafiki wa kweli na mwanadamu mwisho wake ni kukupeleka kuzimu..na hata hapa ukiwa hai duniani bi kukufanya mtumwa wa dhambi .
 
Nimeziona zinatrend huko Twitter..
Screenshot_20260213_214532_X.png


Naona na wewe umeyabeba na kuyaleta huku JF.
 
Katika uchawi, bangili ya fedha hutumika kama hirizi yenye nguvu, inayoweza kuvaliwa kwa ajili ya ulinzi, uangavu, na uchawi wa mwezi. Ikihusishwa na nishati ya uke ya Mwezi, ya kupokea, fedha inaaminika kuwa huzuia roho mbaya, kunyonya nishati hatari na kuboresha ufahamu wa kiroho. Inatumika mara kwa mara kwa ajili ya kuimarisha, kuweka msingi, na kuunganisha na Mungu.
 
Back
Top Bottom