Tafadhali usivae hii bangili kwa kufuata mkumbo

Mizimu huwa inakuja kwa sura za marehemu?
 
Wewe mbona story yako haieleweki mkuu?
 
Kuvaa tu haina shida, shida inaanza unapoanza kuamini mizimu na imani za kishirikina.
Kuna vitu vyengine ukivaa vina athari zake iwe chanya au hasi hata kama umevaa bila imani yeyote na hujui lolote.
 
Mkuu madini yana maana nyingi na mwili wako
mimi huwa navaa bangili tatu za shaba safi
zinanisadia sana kiafya!
Ni kweli kabisa bangili hutumika pia kama tiba na kinga kwa masuala ya kiafya, kama matatizo ya mifupa.
 
Imani itabaki kuwa mazingaombwe tuu
Katika saikolojia, imani si wazo tu tupu linalokaa kichwani. Ni nguvu inayotenda kazi inayochagua tunachokiona, inayoelekeza vitendo vyetu, inayoathiri afya yetu ya mwili, na hatimaye, inayounda maisha yetu. Kubadilisha imani zetu hasi na kukuza imani zenye afya na uhalisia ni lengo kuu la tiba nyingi za kisaikolojia.
 
Wapo wenye kuamini kuwa mizimu ni zile nafsi za mababu zetu waliyokufa huko zamani ila wapo wenye kuamini mizimu ni majini tu ambao mababu zetu waliunga ushirika nao au kuingia nao makubaliano kwa baadhi ya mambo.
Sawa mkuu... nimekuelewa vyema..
 
Sehemu kubwa ya wanaukoo ni wapumbavu! Bora ukae kivyako vyako! Chunga sana usije ukavishwa madude
 
Si Kweli
 
Wewe mbona story yako haieleweki mkuu?
hizo bangili ni kweli zinavaliwa kulingana na mizimu yako ya ukoo wako uliyonayo...hiyo mizimu ndiyo itaamua uvae bangili la aina gani kati ya shaba au fedha ,au mchanganyiko wa shaba na fedha..

na moja ya kazi za hayo mabangaili ni ulinzi kwa huyo anayovaa...hii kwa mujibu qa uzoefu wangu kipindi nafanya ushirikina na kwenda kwa waganga wa kienyeji na kutambika mizimu kabla sijaokoka.

nikilinganisha kipindi natumikishwa na mizimu na ushirikina na waganga wa kienyeji..na kipindi baada ya kuokoa na kuachana na ushirikina.
nahitimisha ni hasara kumtumikia mizimu na kumtegemea mwanadamu au viumbe chochote na vitu kama waganga wa kienyeji,mizimu ,majini na hirizi kama mabangili na mapete au chale...na hazitakusaidia zaidi ya chochote zaidi ya mateso ya kimwili na roho.

ILA KUMTEGEMEA MUNGU KATIKA KILA KITU KUNA FAIDA KULIKO KUTEGEMEA VITU (mabangili,pete,hirizi,chale n.k)AU VIUMBE WENGINE(majini,waganga wa kienyeji,mizimu n.k)
 
Yer 17:5 SUV
BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.
 
Walawi 19:28
“ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimi BWANA.
 
Ni kweli kabisa bangili hutumika pia kama tiba na kinga kwa masuala ya kiafya, kama matatizo ya mifupa.
Wafia dini wao wanaamini eti ni ushirikina
madini ya shaba safi ni tiba ya mifupa na uvimbe wa mwili
Ndio maana musa alichonga nyoka wa shaba ukimuangalia tu au ukimgusa unapona!
 
Story yako haieleweki mara ulikuwa unangaika kwa waganga mara ulikuwa unatumikia mizimu mara mizimu ilitaka uwe mganga, mkuu usihubiri habari za Mungu kwa kuingizia story za kutunga kama unafanya hivyo achana na hiyo tabia sio nzuri.
 
Wafia dini wao wanaamini eti ni ushirikina
madini ya shaba safi ni tiba ya mifupa na uvimbe wa mwili
Ndio maana musa alichonga nyoka wa shaba ukimuangalia tu au ukimgusa unapona!
Unajua ndio maana wanazitukanisha dini zionekane hazina maana, ila ni ujinga wa watu wenyewe tu hawataki kujielimisha kwanza jambo akalielewa yeye kakariri tu neno shirki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…