Tafakari: Uvamizi wa shamba la Kenyatta na shambulio la Lissu

Sheria zingine za nchi bhana daaah! robo 3 ya nchi inamilikiwa na Raia mmoja tu na nchi yenyewe ina kilometers chache sana za miraba ya ardhi.

Africa, Africa, Africa.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Wanahamasisha wananchi maskini maandamano wakati wamejimilikisha ardhi yote yenye rutuba.

Tolu, Odii na freedom yawapate Ili wananchi wapate Ukombozi wa Kweli.
 
~ Kenyatta mwenyewe alimuondolea ulinzi DP Ruto akiwa madarakani.

~Walinzi wa wastaafu huwa hawapelekwi kwenye mashamba bali makazi yao tu.

~Maandamano ya wafuasi wa RAO nayo yanaambatana na uporaji.

~ Hata kiwanda cha RAO ni vile kina electric fence tu ila Alhamis ijayo kitatiwa kiberiti.
 

Ujasiri wa kuona mwanasiasa kudanganya wananchi mnaupata wapi?

Kwani waandamanaji ni watoto wadogo au ni punguani?

Kwani waandamanaji hawajui hatari inayowakabili huko kwenye maandamano?

Kwanini kuwadhania msiowafahamu kuwa wanaweza kuwa wajinga na werevu ni ninyi?
 
Sasa,ni nini hukufanya uingie kwenye mijadala(jieleweshe maana ya mijadala)wakati huwa unakuwa na majibu yako?Ungeenda hata kwa katibu wako wa chama chako mjadili kuuza kadi.
 
Mkuu we nae ni bure una hoja lakini hujaileta vyema.
Hoja imeeleweka wazi kwa wenye uelewa mzuri.

Shambulio la Lisu, kwanza kilichofanyika ni kuondolewa ulinzi kwenye eneo alilokuwa akiishi kabla ya uhalifu. Dola iliondoa ulinzi.

Uhuru Kenyata kama Rais mstaafu, yeye mwenyewe, makazi na mali yake vinastahili kulindwa. Mali zake zimeharibiwa. Wahalifu wameachwa wafanye uhalifu wao bila ya kubugdhiwa na dola, sawa kama walivyoachwa washambuliaji wa Lisu, ambao hata baada ya shambulio, waliwekewa njia ya kupita bila bugdha, kwa askari kuyazuia magari na bodaboda.

Mlingano wa matukio - katika mazingira yote mawili, dola inanyoshewa kuwa nyuma ya uhalifu.
 
Yajayo yanafurahisha, wanaojitokeza kwenye maandamano niwengi kuliko waliomchagua Raisi na makamu wake fake....kwa hili lakuchoma moto mali za familia za Raisi mstaafu wametia moto kwa petroli.... wataikimbia ikulu wenyewe majambazi hawa... system ilimsaidia sn huyu Ruto kuingia madarakani, ndomana wale wa-Venezuela waliokamatwa na vifaa vya kupigia kura KINOTI aliwaachia kinyemela, hata kujiuzulu kwa KINOTI ni danganya toto wote wamehusika kumpora RAILA ushindi wake, jopo la majai na jaji mkuu wote ni VIBARAKA wa Ruto, sasa watajua maharage ni Mboga, wizi kwenye mradi wa Arror na kimwarer dam, wamemalizana kimya kimya na Wataliano juzi, kashfa ya wizi kwenye county wa makamu wa raisi kesi imefutwa, Aisha Jumwa anayekabiliwa na kesi ya mauaji bila aibu kahongwa uwaziri sasa unamshitakije? , Kenya KWISHA .
 
Duh

Tundu Lisu alikuwa na Cheo gani?
Alishambuliwa katika eneo linalolindwa na polisi 24/7 ndiyo ilikuwa point ya mleta mada.
Inawezekana vipi eneo linalolindwa 24/7 wakati wa mashambulizi polisi wote wa zamu wanakosekana katika eneo lao la ulinzi? Polisi wa zamu, wapangaji wa ratiba za ulinzi, mkuu wa jeshi la polisi, shirika la ujasusi(mashushushu) na wizara husika lazima kunakuwa na walakini.
-Only big brains can understand this.
 
Kufanana kwa scenarios hizi mbili ni pale polisi wa zamu wanapokosekana eneo lao la kazi ambalo wapaswa kuwepo 24/7, kwanini polisi wakosekane muda wa shambulio?
 
Aende mahakamani.
Nenda mahakamani
....haya wewe ndie unaejifanya umeelewa, umeelewa nini? manake sijaona umebandika lelote lenye kuonyesha huo uwerevu unaojipachika....Nieleweshe

Huwa ninakuambia una uwezo mdogo wa uelewa na kiuandishi, nadhani sasa umejionea kwa mdau mwingine.
 
Muwe mnasoma kwanza. Mzee amefanya comparison analysis ya matukio mawili wewe un jump kisa ametajwa lisu?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜Œ
Yaani nimecheka. Ati Nisome kwanza, kwamba sikusoma ila nimeona ametajwa lisu ni ka un jump. Ahhhh
Sasa ndugu yangu, unataka kusema nimeonaje katajwa lissu? Haya basi. Nitasoma tena.
 
Ukufuatilia jinsi wanavyojibishana utaona wao ndio walitaka kusema Hayati na Ruto wanafanana kiajenda. Kuwa wao ndio wanaonekana yaani Ruto na Hayati Magufuli(kulingana na udadavuzi wa mleta mada) ndio wanatumia ati ni viongozi wanaowachukia mabepari na ni watumiaji wa Dola....kuwa wao ndio walitoa maagizo kuwa hayo matukio yatendeke. Shaabash na wanajua fika hata mahakamani hawawezi kupruv hayo....kazi yao ni ya kumezesha midubwasha yao. na Kubadilisha uhalisia....wana spin taarifa.... na wapo kazini.
 
Mkuu nyomi hizi ni kubwa mno kujaribu kuuhalalisha kirahisi rahisi mgogoro kihivyo.

View attachment 2568407

Zingatia polisi walihusika Jana kupiga waandishi na kushadadia shamba la uhuru kuhujumiwa:
Ngoja tuone kama wataweza kuvumilia mali na vitega uchumi vyao kuharibiwa huwez kufanya fujo Kwa Raisi aliyechaguliwa kapeleka Kesi mahakamani huko amechemka na asipokuwa makin Mzee odinga akina Rutto watamuondoa kabisa dunian ki namna wanavyojua wao
 
Wee jamaa umeona na ndiyo mwelekeo anayofanya Rutto kuonesha wapi ilipo chakula kuwa ardhi yenu ni hii hapa waende wakachukue Sasa kitimutimu chake sio Cha nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…