Tafakari Ya Mateso ya Lisu Kwa Siku Hii Ya Ijumaa Kuu.

Mungu haangaiki na wajinga au wasioshika Sheria zake maana asema ......Mtu achungue mdomo wake ajiweka mbali na mitego itayoharibu maisha yake.

Lisu yeye anaponzwa na kinywa chake mwenyewe.
Kinywa kipi,kufanya uasi kwenye mifumo kandamizi ya uchaguzi ni sahihi kabisa,Badilisheni hizo sheria basi kama mnaamini katika haki.
 
suala la kuwasingizia watu kwa mashitaka ya uongo linaguswa sana katika Biblia, na Mungu amelifanya wazi kuwa ni dhambi. Maandiko haya yanaeleza hayo kwa uwazi, vifungu hivi hapa chini:
  1. Kutoka 20:16 – ‘Usimshuhudie jirani yako uongo.’ (Akiwa ni moja ya Amri Kumi)
  2. Mithali 19:5 – ‘Shahidi wa uongo hataachia kuadhibiwa, wala asemae uongo hatapona.’
  3. Mithali 6:16-19 – ‘Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana, naam, saba ni chukizo kwake: macho ya kiburi, ulimi wa uongo, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, moyo uwazao mawazo maovu, miguu ifanyayo haraka kwenda maovuni, shahidi wa uongo asemaye uongo, na apandaye fitina kati ya ndugu.’
  4. Isaya 5:20 – ‘Ole wao wasemao ya uovu kuwa mema, na ya mema kuwa maovu…’
  5. Zaburi 101:7 – ‘Afanyaye hila hatakaa ndani ya nyumba yangu; asemaye uongo hatathibitika mbele ya macho yangu.’
  6. Ufunuo 21:8 – ‘…na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti; hii ndiyo mauti ya pili.’
Maandiko haya yanaonyesha kwamba uongo ni chukizo kwa Mungu, hasa pale unapomdhuru mtu asiye na hatia. Hivyo, kwa wanaotunga mashtaka ya uongo, wanajiwekea laana na hukumu mbele za Mungu, si tu kwa sasa bali hata kwa maisha yajayo.”
 
Asante kwa nukuu njema.

Tena andiko lingine linanena juu ya umuhimu wa kuwa wakweli:

Waefeso 6:14
Jifungeni umweli kama mkanda kiunoni na haki kama kinga ya kifuani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…