Uchaguzi 2020 Tafakuri: Je, ni kwanini CCM inatumia nguvu kubwa kumnadi Dkt. Magufuli?

Maana yake bila vyombo vya dola CCM hawana ujanja
Huwa sipendagi kujadili mada na wewe kwasababu nakufahamu kuwa huwezi kujibu hoja badala yake huwa una viroja vingi sana.

Kama bila dola ccm haina ujanja sasa maana ya chama kushika dola ni ipi?
Mana tupo kwenye uchaguzi mkuu vyama vyote vinagombea kushinda uchaguzi vishike dola ina maana ikitokea CUF wakashinda na wenyewe watakuwa Chama dola?
 

Haa haa, ni andiko zuri sana....

Kwa hiyo jamaa Jiwe (Mfalme Sauli) wa maelfu ameghadhabika kwa Daudi (Manusura wa Risasi) Tundu Lissu kwa kuimbiwa na kupewa sifa ya kuua makumi elfu?

Ana wasiwasi huyu. Sasa anachokiona mbele yake ni jamaa kupewa ama kuchukua ufalme tu, ndicho kilichobaki.....

Vita imeanza. Vita inapiganwa. Bahati mbaya kwa mfalme Sauli (Magufuli) ni hii;

Imeshaandikwa na kutamkwa na "Mzee wa siku" kuwa, Ufalme umeondoka mikononi mwake.....

Kwa hiyo atapigana kwa kutumia mbinu zote na kwa kutumia kila aina ya silaha za kibinadamu alizonazo; Bunduki (risasi), NEC, maafisa waasi baadhi wa Polisi, maafisa waasi baadhi wa TISS, viongozi fake wa "dini" nk nk LAKINI HATASHINDA..!!

Tatizo ni moja. Binadamu ni wagumu sana kuuelewa utendaji kazi wa Mungu Yehova na kumpa heshima na utukufu wake...!!
 
Kwa sababu hana mvuto kwa kauli zake na amefanya maisha ya watu kuwa magumu kwa kisingizio cha miundombinu na midege.
Over
 
Ukiona hvyo jua Kuna tatizo linafichwa .. viongozi wa dini wanashiriki dhambi na wasanii wanashiriki ushirikjna wa ccm live
 
Mkuu acha ujinga, ujinga wenu,incompetency yenu,makaburi na ulafi wa madaraka uliopitiliza ndo unawafanya mtumie police,TISS,msajiri,tume na hata jwtz,Trump anauchaguzi tarehe 3 November,Je anatumia vyombo vya dola kukambiliana na Democrat? APM pale Malawi alitumia vyombo vya dola kukabiliana na MCP?
 
Furaha ya ccm ni kuona mkulima akizidi kufilisika na maskini wakiwapeleka watoto wao kwa shule za Kata wapumbae zaidi. Nonsense.
 
Kwa sababu, hali ngumu inawafokea wananchi halafu inapiga kelele mno. Kwa hiyo inabidi watumie nguvu kubwa ili kuzidi nguvu ya hali ngumu.
 
Unaona unavyo puyanga ovyo sasa? Hapo umejibu swali lipi nililouliza?
 
Kwani washaanza kumnadi mkuu? Acheni kupepesuka, hapo wanaelezea machache tu kutoka mengi aliyoyafanya! Subiri tume ipige kipyenga tuanze kampeni ya kitanda kwa kitanda, kama mtaambuli hata kura laki sita! Mwaka huu hadi Hashim Rungwe atawapiga bao. Viva Magu vivaaa, magufuli tano tena!
 
walio sema kuwa upinzani umekufa sijui sahizi wana hali gani..[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Kwa sababu hakubaliki Kwa wengi japo anasema amefanya mengi lakini hawezi na hatawezw kumshinda lissu kihalali ndio maana kila mda wanamfanyia figisu.
 
Hivi ukiwauliza wananchii haya maswali machache watamjibu nini!?

kati ya ndege na ajira watachagua nini!?

Kati ya SGR na nyenzo za kilimo na masoko watachagua nini!?

Kati ya Umeme wa Stigler gorge na maji Safi unafikiri wananchi watachagua nini!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…