Tafakuri kuhusu matokeo ya kidato cha 4 mwaka huu

Mabadiliko ya mfumo wa maswali
Zamani ilikuwa maswali mengi afu complicated saivi
section A maswali10
section B maswali5
section C maswali5
section D essay 2 au 3
maswali ni ya story mpaka raha yani unapewa kastory linafuata swali unatamani waweke na muendelezo
 
Au wote turudi tukarudie mitihani tusafishe vyeti?
 
Naungana hoja na wewe! Ila tofauti na enzi zetu, mazingira ya kusoma na vitendea kazi hayakuwa rafiki kabisa! Sasa hivi vitabu ni vingi hata kama huna uwezo wa kuvinunua lakini ukiingia kwenye mtandao na bundle lako la jero, buku unajipatia kitabu bure kabisa! Pastpapers tena nyingine zimesolviwa zipo zoote! Pili, mwamko wa wazazi kuwasimamia watoto na kuibuka kwa shule binafsi kufundisha kibiashara, tuition muda wote, nk, nk, vimewezesha watoto wetu kumudu div 1.7! Tatizo liko kwenye ubunifu wa kudhihirisha kilichokwenye makaratasi ndo kilichokichwani na mikononi?
 
Youtube na google zimerahisisha sana elimu.

Kila kitu kipo mtandaoni
 
Yale maswali ya,Nchi inayolima chai kwa wingi Duniani,au waziri wa ulinzi wa Zanzibar au Congo ilipata uhuru mwaka gani hayapo tena...
 
SIKU HIZI 1.7 WALA SIYO TAMU KAMA ZAMANI
 
Mkuu ujue wanakaza sana wale watoto
ni kweli mkuu hata dogo langu kapass kwa ufaulu mzuri japo hajanifikia ila kiukweli dogo alikua anasoma balaa yani mpaka inafika stage unamkataza dogo nenda kale utapata vidonda vya tumbo ye ni kupiga msuli tu, mpaka alinunua kitabu cha MBINU ZA KUFAULU MITIHANI dogo yani kajitahidi uwezo wake sikutarajia angeua hivi nilijua atapata wastani tu ila kapiga haswa
 
Mkuuu bora wewe..
Mi kuna dogo huyo an... Mkuuu shule za kata madg wapmbn jmn sijui shida nn
 
Kizazi hiki kinapiga sana shule, naishi karibu na shule ya kata, muda wao wa kurudi nyumbani ni saa 11 jioni na ukipita nyakati za usiku utawakuta wanajisomea pale shuleni.

Matokeo yao ya mwaka huu si haba wamejitahidi, maana hakuna aliyepata zero.
 
Kizazi hiki kinapiga sana shule, naishi karibu na shule ya kata, muda wao wa kurudi nyumbani ni saa 11 jioni na ukipita nyakati za usiku utawakuta wanajisomea pale shuleni.

Matokeo yao ya mwaka huu si haba wamejitahidi, maana hakuna aliyepata zero.
tatizo waliaminisha madogo elimu ni ufunguo wa maisha(meaning maisha yamefungwa)
Ila saivi madogo wamejua elimu ni kusoma upate maarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…