Tafakuri kuhusu matokeo ya kidato cha 4 mwaka huu

Tafakuri kuhusu matokeo ya kidato cha 4 mwaka huu

Tunamshukuru raisi mama Samia suluhu Hasan kwa matokeo mazuri ya necta ya shule ya st Francis, na ya nchi kiujumla
 
Kulikoni siku hizi kwenye elimu ya nchi hii.?
Ni kwamba sisi zamani tulikuwa na uwezo mdogo wa kiakili ama la?
Au zamani elimu ilikuwa ngumu?
Au watoto wa siku hizi wana akili na uwezo mkubwa kuliko sie?
Au elimu na ufundishaji umekuwa bora sana kiasi kwamba Div. 1.7 zinaweza kutolewa na darasa zima...? Mpaka siku hizi shule za kata ambazo zinakuwaga na ufaulu wa kawaida nao wanatoa 1.7 hata mbili...? Au mitihani ni rahisi zaidi kipindi hiki?

Hii inamaanisha nini..? Sio husda...ila ina inafikirisha mno Div. 1.7 siku hizi zimekuwa kama njugu...VIPI ELIMU NA UPIMAJI ULIKUWA UPI...WA KIPINDI KILE DIV. 1.7 INAWEZEKANA KUWA MOJA TU TANZANIA NZIMA...AU HIVI SASA..?

Wasikutishe. Huku kitaa baada ya kumaliza shule maisha yanaenda kinyume nyume. ni wachache sana kati ya hao vipanga ambao hizo division 1 zitawakomboa. Wakifika chuo Kikuu mambo yanakuwa tofauti sana huwezi ona tofauti ya aliyekuja na div 1 na mwenye div 2 au 3. Kuna tofauti ya kukariri vitu na uwezo wa kuelewa mambo.Tena wengine hadi wanadisco
 
Back
Top Bottom