Tafakuri kuhusu matokeo ya kidato cha 4 mwaka huu

Kwa Sisi maveteran A ilikuwa inaanzia 81 sasa Kwa Gz inaanzia 75 unategemea nini
 
Ila kiuhalisia...kunapaswa uchunguzi ufanyie...this is not really...no matter what...
 
Hawana maana wale,walishajikatia tamaa,
Nimekaa mahali moja hivi kama wiki (chumbageni) saa tatu ndo wanatoka kufungua maduka sasa hapo ni maali pa kuishi watu kweli, niliswaki saa nne hiyo siku sitosahau
Ahahahha wee bana weee kuna watu wakikusikia hapa jua huu ugomvi utaubeba peke yako mkuu
 
Watu wanapambana.... Tembelea hizo shule ukajionee.
Elimu ni uwekezaji.. Hakuna Cha Bure.

LIKUD
😂😂
 
Goli limetanuliwa ili mwenye uwezo wa kawaida, (ambao wengi ni shule "zetu") wa kupiga shuti afunge, sasa wale wenye uwezo mkubwa wa kupiga mashuti wanafunga wote
 
Nashukuru Mungu Binti yangu kapiga three masomo yote kapata c kasoro math na physics kachana mkeka nimechukia lkn hamna namna
 
Tutazunguka koooote mara materials za kusomea zinapatikana, mara madogo wanasoma sana nk, ila uhalisia elimu sasa imechakachuliwa sana hasa kwakuwa nchi hii hata masuala nyeti ccm wamechagua kuyaendesha kisiasa.

Hao watoto wanafaulu sana ila vyuoni uwezo wao ni mdogo ajabu kiasi mtu unashangaa ukisikia wengi wao wana div 1!

Bahati mbaya vyuoni nako tangu mwaka juzi AI imeingia, yaani ndio imekuja kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza. Ikitolewa assignment wachache sana wataumiza vichwa vyao, zaidi ya 90% wata copy swali kama lilivyo na kulitupia kwenye ChatGPT ambayo itatiririka majibu yote na reference za kubuni, wao ni ku copy na ku paste kisha mbio steshenari. Usipotafutwa mwarobaini wa kuidhibiti basi kuna hatari ya watu kuingia vyuoni na kutoka kama walivyoingia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…