Tafakuri ya FaizaFoxy 7: Shule za kusomea ujinga. Tanzania na propaganda za Udini Shuleni

Tafakuri ya FaizaFoxy 7: Shule za kusomea ujinga. Tanzania na propaganda za Udini Shuleni

๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„

Hizi Dini zinatesa watu kweli.

Sasa hao kwenye video si wanajadilli Kama humu JF tuu wanauwezo wa kutumia Reference wazitakazo kutetea hoja zao.

Lakini vipi vitabu vinavyoeleza kuhusu Waarabu na UTUMWA
Hata Wazungu wapo waliofanya UTUMWA.

Ila waarabu ndio walikuwa Kama madalali wa Biashara hiyo.
 
Wewe una uhakika gani kuwa huyo ni Mwarabu na huyo ni Mwafrika, ndiyo mliozowea kjazwa ujinga kila mnalooneshwa kwenye mtandao mnaamua kuwa ni la kweli Si kila unaloliona kwenye mtandao ni la kweli.

Teknolojia inavyotumika vibaya siku hizi kwa kujazana ujinga, hata wewe unaweza kuwekwa unakula mavi.

Kwani umesahau Lema aliwekwa kwenye mitandao anafanywa nini? Ilikuwa ukweli ule?

๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„
Hujui yanayotokea uarabuni Mkuu?
 
Mara nyingi sana hapa JF nimekuwa nikitumia usemi "Hizo shule mlienda kusomea ujinga/?". Hapa chini naweka mojawapo ya mfano hai wa kusomeshwa ujinga, ambao umefanyiwa tafiti na Profesa ukuyakinisha kauli yangu hiyo. Huu ni baadhi tu ya ujinga tunaosomeshwa.

Nayaleta haya kwa kuwa bila ya kuyaongea na kuyaweka wazi hayatakoma na wale tulioaminishwa ujinga huu tujionee jinsi tunavyosomeshwa ujinga.

Tafadhali jionee hii video kabla hujajibu kijinga...

Umetumwa kuleta ujinga na huyu Prof. Rudi kamuambie ya kuwa mada za kuleta udini kwa lengo la kuwagawa waTanzania, badala ya kuwaelekeza waja waamini kwa Mola wao, waache uzinzi, ufisadi, na zina kwa ujumla hazina nafasi hapa. Tuna mambo mengi ya kuijenga jamii yenye kicho kwa Muumba wao. Hayo ya udini baki nayo wewe mwenyewe.
 
Nnachoona ni kuwa wengi wanachangia huku wakiwa hawajaelewa profesa amezungumzia nini!

Nilivyomuelewa ni kwamba
Hakusema kama Waarabu hawakushiriki Katika biashara hiyo ila ushiriki wake sio kama unavyoonyeshwa katika historia ya sasa mashuleni, kwa asilimia kubwa anayehusishwa ni Mwarabu, huku mzungu mhusika mkuu akiwekwa pembeni.
Na bahati nzuri ushahidi upo wazi Kwa sasa, huko uzunguni ngozi nyeusi inaongoza kuliko nchi za kiarabu, lkn Kwann atajwe sana Mwarabu hii leo?

Kama mzungu alikuwa anazuia utumwa, na watumwa waliopo huko kama walipelekwa na Waarabu mbona hatuoni Waarabu huko wakiwa wamezaliana ila tunaona ngozi nyeusi tu na wazungu.

Kama hili nalo wewe unaechangia mada kwa jazba hukuliona, jua ya kuwa hutumii akili kufikiri.

Maelezo mazuri kwa wanaotumia akili!
 
Ninavyojua utumwa ulikuwepo kwenye jamii zote, haikuwa na dini wa kabila. Ila kuna walioufanya kwa "industrial level". Labda tujiulize, masoko ya watumwa yalikuwa wapi? Na hao watu walikuwa ni wa aina gani?
 
Nnachoona ni kuwa wengi wanachangia huku wakiwa hawajaelewa profesa amezungumzia nini!

Nilivyomuelewa ni kwamba
Hakusema kama Waarabu hawakushiriki Katika biashara hiyo ila ushiriki wake sio kama unavyoonyeshwa katika historia ya sasa mashuleni, kwa asilimia kubwa anayehusishwa ni Mwarabu, huku mzungu mhusika mkuu akiwekwa pembeni.
Na bahati nzuri ushahidi upo wazi Kwa sasa, huko uzunguni ngozi nyeusi inaongoza kuliko nchi za kiarabu, lkn Kwann atajwe sana Mwarabu hii leo?

Kama mzungu alikuwa anazuia utumwa, na watumwa waliopo huko kama walipelekwa na Waarabu mbona hatuoni Waarabu huko wakiwa wamezaliana ila tunaona ngozi nyeusi tu na wazungu.

Kama hili nalo wewe unaechangia mada kwa jazba hukuliona, jua ya kuwa hutumii akili kufikiri.

Maelezo mazuri kwa wanaotumia akili!
Huo ndio uongo tunao upinga. Sijui mlisoma historia gani lakini niliyosoma mimi ilizungumzia sana uhusika wa wazungu katika biashara ya watumwa iliyovuka bahari ya Atlantic. Kwa wao ilikuwa rahisi zaidi kwenda Ghana mpaka Angola kuchukua watumwa kuwapeleka kwenye himaya zao Amerika ya Kusini, Amerika ya Kati, ya Kaskazini na Carribean. Wazungu wenyewe wanakiri hili na wanakubali kuwa babu zao walifanya ukatili mkubwa sana.

Waarabu, kwa sababu ya ukaribu wao na Afrika Mashariki walihusika sana katika biashara ya utumwa ya pande hizi. Ushiriki wao ulianza hata kabla ya Seyyid Said kuhamia Zanzibar. Wahindi walihusika kwa kuwakopesha fedha za kununulia vitu ambavyo wangenunulia watumwa. Baadhi ya makabila yetu yalihusika na walikuwa washiriki wa waarabu katika hiyo biashara dhalimu. Wazungu walianza kuja kufuata watumwa maeneo yetu biashara hii ilipopigwa marufuku na waingereza na hivyo kuwazuia kuchukua watumwa kutoka maeneo yaliokuwa sehemu ya himaya ya Uingereza. Hao watumwa anaosema walipelekwa Brazil wengi walichukuliwa kutoka Angola ambalo lilikuwa koloni la Ureno.

Waarabu kutokana na ukaribu wao, ndio walikuwa vinara wa biashara ya utumwa Afrika Magharibi iliyowapeleka watumwa Afrika Kaskazini. Dhana ya kuwa watu weusi ni watu wa kutumikishwa inaendelea bado Mauritania, Libya na Sudan.

Huyu profesa anashupalia vikatuni wakati kuna picha nyingi tu zikionyesha watumwa wakiwa katika majahazi ya waarabu. Simulizi la kilio cha watumwa Bagamoyo sio za kutungwa. Kuna ushahidi wa maeneo walikokuwa wakihifadhiwa. Kushamiri kwa tamaduni za kiarabu katika njia kuu ya utumwa ni ushahidi mwingine. Tamaduni hizi zilipelekwa na waarabu ambao anasema kwa zaidi ya miaka 1000 hawakudiriki kuingia ndani ya Afrika.

Kutuambia kuwa watu weusi walifanywa watumwa uarabuni ili kuwapikia chai waarabu ni matusi ya nguoni.

Hiyo hoja ya kusema kuwa kwa sababu kuna watu weusi wengi Marekani kuliko uarabuni haina mashiko. Watu weusi wapo uarabuni. Tofauti na Marekani ni kuwa waarabu waliwatambua watu weusi wenye damu ya kiarabu kuwa ni waarabu. Seyyid Said alizaa na waethiopia na watoto wake walitambuliwa kama waarabu. Huko Sudan, Janjaweed wengi ni weusi tii lakini kwa sababu wana damu ya waarabu wanajihesabu kuwa waarabu. Iraq weusi wapo. Kuwait wapo. Tofauti ni kuwa hawaitwi weusi bali waarabu.

Wazungu walikuwa tofauti. Wao mtu yeyote mwenye damu nyeusi alikuwa mweusi ( one drop rule) . Kwa sababu hiyo hawakuona taabu kuwafanya watumwa watoto waliozaa na watumwa wao. Mmoja wa waasisi wa taifa la Marekani, Thomas Jefferson alikuwa na familia kubwa tu ya watoto weusi aliozaa na mtumwa wake. Watoto pamoja na mama yao walibaki watumwa wake mpaka alipokufa.

Sababu nyingine ya kutokuwa na watu wanaohesabiwa weusi wengi uarabuni ilikuwa ni kuwa wengi hawakufika uarabuni na walifia njiani kutokana na mazingira ya kikatili waliyokuwa wakisafirishiwa.

Nyingine ni kuwa wale watumwa wa kiume waliokuwa wanafanya kazi za kuhudumia wanawake wa kiarabu walihasiwa.

Nyingine ni kuwa wengi waliingia kwenye Uislamu na hivyo kufunguliwa njia ya kutoka utumwani kwa sababu Uislamu unakemea kumfanya Muislamu mtumwa. Mara nyingi hili lilipuuzwa kwa watumwa weusi lakini Seyyid Said aliitumia kukataza kuwafanya wasomali watumwa. Wazungu wao hawakujali kama wewe mkristu au la. Kwa wao rangi ya ngozi yako ndio iliyowapa haki ya kukufanya mtumwa.

Ni uongo kusema kuwa historia inasema kuwa waarabu ndio waliopeleka watumwa Marekani na Carribean. Wazungu wanakiri kuwa ni mataifa ya Ulaya ndio waliopeleka watumwa maeneo hayo. Kuchukua kipicha kilichotumiwa na mtu asiyejua historia kama ushahidi kuwa wazungu walisema kuwa waarabu walipeleka watumwa Carribean ni kutaka kutuchezea akili. Hao waliochora hizo picha ni watu wasiojua historia. Wakosolewe kwa kutokujua kwao.

Waarabu na washiriki wao wanafanya juhudi kubwa sana kutaka kutuaminisha kuwa wao hawakuhusika katika biashara hii haramu bali ni sisi watu weusi tulijipeleka utumwani baada ya kuvutiwa na ukarimu wao! Watu kama huyu profesa wanajaribu kupunguza scale ya udhalimu huo kwa sababu wanajua ushahidibupo wa ushiriki wao kwa hiyo hawawezi kuukana jumla.

Tofauti na anavyosema huyu profesa, chuki katika jamii yetu inapandikizwa na watu kama yeye ambao wanataka tuangalie kila kitu kwa misingi ya dini. Na wanaweza kufanikiwa kwa sababu sasa hivi mtu unaweza kuishi maisha yako yote bila kushirikiana na mtu wa dini nyingine. Unaweza kusoma kuanzia chekechea hadi chuo kikuu katika shule zinazomilikiwa na watu wa dini yako. Unaweza kufanya kazi katika makampuni yanayomilikiwa na watu wa dini yako. Watu kama hawa inakuwa rahisi sana kuwachukia watu wa dini nyingine. Tunaona humu jinsi watu wanavyotupiana matusi ya nguoni linapotokea suala linalohusu dini zao.

Ndio maana najiuliza kama hawa watu kweli hawana marafiki na ndugu wasio wa dini yao? Watu kama huyu profesa wanatupeleka kubaya.

Amandla...

JokaKuu Nguruvi3
 
Nnachoona ni kuwa wengi wanachangia huku wakiwa hawajaelewa profesa amezungumzia nini!

Nilivyomuelewa ni kwamba
Hakusema kama Waarabu hawakushiriki Katika biashara hiyo ila ushiriki wake sio kama unavyoonyeshwa katika historia ya sasa mashuleni, kwa asilimia kubwa anayehusishwa ni Mwarabu, huku mzungu mhusika mkuu akiwekwa pembeni.
Na bahati nzuri ushahidi upo wazi Kwa sasa, huko uzunguni ngozi nyeusi inaongoza kuliko nchi za kiarabu, lkn Kwann atajwe sana Mwarabu hii leo?

Kama mzungu alikuwa anazuia utumwa, na watumwa waliopo huko kama walipelekwa na Waarabu mbona hatuoni Waarabu huko wakiwa wamezaliana ila tunaona ngozi nyeusi tu na wazungu.

Kama hili nalo wewe unaechangia mada kwa jazba hukuliona, jua ya kuwa hutumii akili kufikiri.

Maelezo mazuri kwa wanaotumia akili!
Sitaki kutia langu, mradi wewe umeliona hilo na wengine nao wataliona kivyao. Mimi nani ninyanyue mdomo wangu mbele ya Profes Abdul Noor? Ambae kaweka kila kitu kwa ushahidi na hakuna aliyetokea kumpinga mpaka leo.
 
Huo ndio uongo tunao upinga. Sijui mlisoma historia gani lakini niliyosoma mimi ilizungumzia sana uhusika wa wazungu katika biashara ya watumwa iliyovuka bahari ya Atlantic. Kwa wao ilikuwa rahisi zaidi kwenda Ghana mpaka Angola kuchukua watumwa kuwapeleka kwenye himaya zao Amerika ya Kusini, Amerika ya Kati, ya Kaskazini na Carribean. Wazungu wenyewe wanakiri hili na wanakubali kuwa babu zao walifanya ukatili mkubwa sana.

Waarabu, kwa sababu ya ukaribu wao na Afrika Mashariki walihusika sana katika biashara ya utumwa ya pande hizi. Ushiriki wao ulianza hata kabla ya Seyyid Said kuhamia Zanzibar. Wahindi walihusika kwa kuwakopesha fedha za kununulia vitu ambavyo wangenunulia watumwa. Baadhi ya makabila yetu yalihusika na walikuwa washiriki wa waarabu katika hiyo biashara dhalimu. Wazungu walianza kuja kufuata watumwa maeneo yetu biashara hii ilipopigwa marufuku na waingereza. Hao watumwa waliopelekwa Brazil wengi walichukuliwa kutoka Angola ambalo lilikuwa koloni la Ureno.

Waarabu kutokana na ukaribu wao, ndio walikuwa vinara wa biashara ya utumwa Afrika Magharibi. Dhana ya kuwa watu weusi ni watu wa kutumikishwa inaendelea bado Mauritania, Libya na Sudan.

Huyu profesa anashupalia vikatuni wakati kuna picha nyingi tu zikionyesha watumwa wakiwa katika majahazi ya waarabu. Simulizi la kilio cha watumwa Bagamoyo sio za kutungwa. Kuna ushahidi wa maeneo walikokuwa wakihifadhiwa. Kushamiri kwa tamaduni za kiarabu katika njia kuu ya utumwa ni ushahidi mwingine. Tamaduni hizi zilipelekwa na waarabu ambao anasema kwa zaidi ya miaka 1000 hawakudiriki kuingia ndani ya Afrika.

Kutuambia kuwa watu weusi walifanywa watumwa uarabuni ili kuwapikia chai waarabu ni matusi ya nguoni.

Hiyo hoja ya kusema kuwa kwa sababu kuna watu weusi wengi Marekani kuliko uarabuni haina mashiko. Watu weusi wapo uarabuni. Tofauti na Marekani ni kuwa waarabu waliwakubali watu weusi wenye damu ya kiarabu kuwa waarabu. Seyyid Said alizaa na waethiopia na watoto wake walitambuliwa kama waarabu. Huko Sudan, Janjaweed wengi ni weusi tai lakini kwa sababu wana damu ya waarabu wanajihesabu kuwa waarabu. Iraq weusi wapo. Kuwait wapo. Tofauti ni kuwa hawaitwi weusi bali waarabu. Wazungu walikuwa tofauti. Wao mtu yeyote mwenye damu nyeusi alikuwa mweusi. Hawakuona taabu kuwafanya watumwa watoto waliozaa na watumwa wao. Mmoja wa waasisi wa taifa la Marekani, Thomas Jefferson alikuwa na familia kubwa tu ya watoto weusi aliozaa na mtumwa wake. Watoto pamoja na mama yao walibaki watumwa wake mpaka alipokufa.

Sababu nyingine ya kutokuwa na watu wanaohesabiwa weusi wengi uarabuni ilikuwa ni kuwa wengi hawakufika uarabuni na walifia njiani.

Nyingine ni kuwa wale watumwa wa kiume waliokuwa wanafanyakazi za kuhudumia wanawake wa kiarabu walihasiwa.

Nyingine ni kuwa wengi waliingia kwenye Uislamu na hivyo kufunguliwa njia ya kutoka utumwani kwa sababu Uislamu unakemea kumfanya Muislamu mtumwa. Mara nyingi hili lilipuuzwa kwa watumwa weusi lakini Seyyid Said alilitumia kukataza kuwafanya wasomali watumwa. Wazungu wao hawakujali kama wewe mkristu au la. Kwa wao rangi ya ngozi yako ndio iliyowapa haki ya kukufanya mtumwa.
Ni uongo kusema kuwa historia inasema kuwa waarabu ndio waliopeleka watumwa Marekani na Carribean. Wazungu wanakiri kuwa ni mataifa ya Ulaya ndio waliopeleka watumwa maeneo hayo. Kuchukua kipicha kilichotumiwa na mtu asiyejua historia kama ushahidi kuwa wazungu walisema kuwa waarabu walipeleka watumwa Carribean ni kutaka kutuchezea akili. Hao waliochora hizo picha ni watu wasiojua historia. Wakosolewe kwa kutokujua kwao.

Waarabu na washiriki wao wanafanya juhudi kubwa sana kutaka kutuaminisha kuwa wao hawakuhusika katika biashara hii haramu bali ni sisi watu weusi tulijipeleka utumwani baada ya kuvutiwa na ukarimu wao! Watu kama huyu profesa wanajaribu kupunguza scale ya udhalimu huo kwa sababu wanajua ushahidibupo wa ushiriki wao kwa hiyo hawawezi kuukana jumla.

Tofauti na anavyosema huyu profesa, chuki katika jamii yetu inapandikizwa na watu kama yeye ambao wanataka tuangalie kila kitu kwa misingi ya dini. Na wanaweza kufanikiwa kwa sababu sasa hivi mtu unaweza kuishi maisha yako yote bila kushirikiana na mtu wa dini nyingine. Unaweza kusoma kuanzia chekechea hadi chuo kikuu katika shule zinazomilikiwa na watu wa dini yako. Unaweza kufanya kazi katika makampuni yanayomilikiwa na watu wa dini yako. Watu kama hawa inakuwa rahisi sana kuwachukia watu wa dini nyingine. Tunaona humu jinsi watu wanavyotupiana matusi ya nguoni linapotokea suala linalohusu dini zao.

Ndio maana najiuliza kama hawa watu kweli hawana marafiki na ndugu wasio wa dini yao? Watu kama huyu profesa wanatupeleka kubaya.

Amandla...
Umeitazama video? SAu unapayuka tu? Tuelezee japo kiduchu maudhui ya kwenye hiyo video. Maana wewe unaongea kitu ambacho hakipo kabisa kwenye maudhui.
 
Umetumwa kuleta ujinga na huyu Prof. Rudi kamuambie ya kuwa mada za kuleta udini kwa lengo la kuwagawa waTanzania, badala ya kuwaelekeza waja waamini kwa Mola wao, waache uzinzi, ufisadi, na zina kwa ujumla hazina nafasi hapa. Tuna mambo mengi ya kuijenga jamii yenye kicho kwa Muumba wao. Hayo ya udini baki nayo wewe mwenyewe.
Umeiona video na umeilewa maudhui yake au umeamua kubwekea hewa tu?
 
๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„

Hizi Dini zinatesa watu kweli.

Sasa hao kwenye video si wanajadilli Kama humu JF tuu wanauwezo wa kutumia Reference wazitakazo kutetea hoja zao.

Lakini vipi vitabu vinavyoeleza kuhusu Waarabu na UTUMWA
Hata Wazungu wapo waliofanya UTUMWA.

Ila waarabu ndio walikuwa Kama madalali wa Biashara hiyo.
Unaonesha hujaitazama video wala hujaielewa maudhui iliyopo. Usiwe mvivu wa kuhipatia elimu, ukishaipata halafu amua uichukuwe au ukatae, sio kabla.
 
Umeitazama video? SAu unapayuka tu? Tuelezee japo kiduchu maudhui ya kwenye hiyo video. Maana wewe unaongea kitu ambacho hakipo kabisa kwenye maudhui.
Ufafanuzi wote huo hajatazama tu video,wewe bibi unaumwa ugonjwa wa akili huku unatembea unadhani uislamu ndio kila kitu na huku ni ushenzi tu kama ushenzi mwingine.
Shwaini usiye na mafuta.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Umeitazama video? SAu unapayuka tu? Tuelezee japo kiduchu maudhui ya kwenye hiyo video. Maana wewe unaongea kitu ambacho hakipo kabisa kwenye maudhui.
Sasa si ingekuwa vyema kama ungesema ni kipi nilichosema hakipo kwenye hiyo video? Tofauti na wewe, sijawahi kukataa kusahihishwa.

Amandla...
 
Inawezekana kuwa kwel ama si kweli.

Na kama mwarabu ndie kafanya unyama na utumwa sana kwa mtu mweusi je hayo masalia ya watu weusi ama black Americans huko USA na magharibi ni nani alikuwa mteja na mnunuzi?

Kama mwarabu alkuwa akiwauza hawa watu huoni hata ktk nchi zake kungebaki masalia ya watu weusi haijarishi kuna visingizio vya kuhasiwa na kuuwawa kwa watumwa lkn ukwel hauondoi kuwa Mzungu ndie mshenzi ikiwezekana zaid ya mwarabu.

Maana mzungu alitumia utumwa kujinufaisha ktk nchi zake na pia anatumia media kupotosha ushenzi wake kwa kujisafisha na mabaya yake kumpelekea mtu wa Asia.

Kuna misemo watu wa magharibi husema ni wati weupe wana bahat kuwa mtu mweusi alichagua USAWA na kusahau kulipiza kisasi, maana dunia isingekalika tena, kwakua unyama aliofanyiwa mtu mweusi haujawai fanywa kwa jamii yeyote ile dunian tangu hii dunia iumbwe tafuta history yoyote hutoona mateso waliyopata wanadamu kama waliyopitia na wanayopitia watu weusi, hivyo basi ni bora mtu mweusi kachagua Usawa na haki ya kutobaguliwa na jamii yeyote hapa dunian kwakuwa hakuna ambaye angepona kama tukiamua kulipiza kisasi.

Itoshe kusema kuwa ni aibu na Laana kwa mtu mweusi kumtetea mwarabu ama mzungu kwa ushenz waliofanya, mamilion ya waafrika waliuliwa na kuchukuliwa utumwan na hayo majitu mnayoyaita ndugu zenu na waliowapa dini, ni vile tu tunasoma vitabu na elimu ambayo iko edited kwa mikono yao kitu kinachopelekea mengi kufichwa waliyoyafanya.

20220417_091030.jpg
 
Waarabu walikuwa wafanyabiashara wakubwa wa biashara ya utumwa na ujangili wa wanyamapori.
Hiyo historia itabaki hivyo, penda usipende.
Mpaka sasa usiwaone na milori na mibasi wanatakatisha, wengi ni majangili na madaktari wa Meno ya ndovu!
 
Ufafanuzi wote huo hajatazama tu video,wewe bibi unaumwa ugonjwa wa akili huku unatembea unadhani uislamu ndio kila kitu na huku ni ushenzi tu kama ushenzi mwingine.
Shwaini usiye na mafuta.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Ukiona mtu anakuja na matusi ujuwe umemshinda hoja. Sikushangai.

Wewe umeiona video?

Hizo porojo alizopiga ndizo zimenifanya niseme kuwa hajaitazama video. Wewe punguani wahed, wewe ndio wakili wake wa kumsemea huyo poyoyo mwenzako?? Au ni mkewe?

Sasa jibu wewe umeitazama video kwenye post namba 1 au unabwekea hewa tu?
 
Back
Top Bottom