Mshana Jr,
Asante Mshana kwa elimu ya rohoni ambayo umekuwa ikiitoa kila mara ila kuongeza fikra za mwanadamu na kumpa nafasi ya kuushiriki uumbaji wa MUNGU.
Tunajua kwa msingi wa uumbaji vitu vyote vimeumbwa na MUNGU, na elimu yote imeachiliwa na MUNGU, lakini pia ameachilia picha na taswira ya vitu mbalimbali ambavyo binadamu kwa kutumia nguvu ya fikra anaweza kuvileta kwenye uhalisia na uwepo kwenye ulimwengu wa mwili. mf uwepo wa ndege, nuklia,elements, magari nk ni nguvu ya fikra za watu.
Lakini pia tunajua kuwa sio vitu vyote vinakuja na nguvu za MUNGU kwani shetani naye ananguvu za kuleta vitu vyake ilikuimarisha utajiri wake na fahari yake, wote wawili wakitumia nguvu ya fikra ya mwanadamu. Nakama ulivyogusia kwenye nguvu ya kumeditati ambayo ndiyo chakula kikuu cha fikra, napenda kimsingi kabisa unisaidie je hiyo meditation uliyoitaja inahusianaje na ile ya MUNGU kwenye agano la kale wakati Mungu ana mwambia Joshua kitabu hiki cha torati kisitoke kinywani mwako, utafakari maneno yake usiku na mchana?
Je, unahisi kila unacho mediated kwa njia zilizotajwa hapo juu na wachangiaji kinakuongoza kumfunua MUNGU?, na kuna njia ambayo mcha Mungu anaweza kuitumia ili kurahisisha meditation yake kwenye maneno ya MUNGU na asije akawa anatoa sadaka kwa adui?
Nakushukuru tena kwa mchango mkubwa wa kuweka elimu hizi wazi, nawasihi watu wasiogope, uwe wa dini yoyote ile, pata maarifa changanya na za kwako, weka kwenye vipimo vya upande wa kule unakoamini na vipimo vinakubaliana songa mbele. Kumbuka awazavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa: hivyo tafuta sana maarifa ili ufanikiwe, kwa maana watu walioupande wa shetani wa maarifa sanaa, lakini watu wanao mtafuta MUNGU wavivu sana kutafuta maarifa kwa dhana ya uoga tuu na kudanganywaa.