Uko sahihi, mtu mwenye mawazo kama
Yako ni Yule Tu ameshakombolews kwenye dimbwi la mawazo ya kimaskini
Mtu maskini hudhani kwamba akiwa na hela shida zote zinatisha😂😂
Vitu vingi kama huna vinaweza kukuzuzua, halafu ukibipata na kubizoea, unaviona vya kawaida.
Kuna siku nilienda kumtembelea rafiki yangu mmoja hapo downtown Dar karibu na Clock Tower.
Sasa rafiki yangu alikuwa na dada yake, huyu dada akaona tangazo la gari moja la kifahari kwenye TV. Yule dada alivyoona lile tangazo, alibadilika sana, akasema kwamba yeye anatamani sana lile gari, ni kama akilipata maisha yake yatakuwa yamebadilika kabisa.
Mimi nilishangaa sana, kwa sababu lile gari tulikuwa nalo nyumbani, mimi nilikuwa nimelizoea, naliona la kawaida sana. Ila nikakumbuka siku za kwanzakwanza tulivypata lile gari na mimi nilikiwa nalishobokea fulani hivi, halafu nikaliona la kawaida tu.
Sasa kwenye mambo mengine hata ya pesa ni hivho hivyo tu. Of course pesa ina kazi nyingi muhimu sana na kusema sana kuwa pesa watu wanazishobokea sana kwa kuwa hawana tu it is kind of elitist, mtu ambaye hana ada, hana pesa ya chakula, hanankidi ya nyumba, hana pesa ya matibabu, kumuambia hivyo, kwamba oesa si muhimu sana, ni kukosa empathy na kukosa adabu.
Lakini kuna level fulani ya kuabudu pesa inakuja kuwa kama yule dada aliyekuwa anashobokea gari analoona akilipata litambadilisha maisha, wakati mimi ambaye kwetu hilo gari lipo kwa miaka kadhaa nikawa najiuliza, mbona mimi kwetu hili gafi lipo na nimelizoea mpaka nalipotezea, halijanibadilishia maisha hivyo?