Tafuteni njia bora, Vicoba ni upotevu wa pesa!

Tafuteni njia bora, Vicoba ni upotevu wa pesa!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Kwa sisi wataalamu wa Fedha huwezi kuita uwekezaji kama hakuna vitu viwili Risk & Return. Sijui kwa kiswahili nisema vipi. Vicoba ni wizi tu maana pesa haiendi kwenye uzalishaji wowote lakini kibaya ukitoa pesa kuna faini. Hivyo Fedha mnaweka bank ambako kuna fees bila riba, hakuna faida yoyote wala riba yoyote pesa inapata.

Wafaidika wakuu ni waanzilishi matapeli ambao wanapeta pesa mwanzoni mfano watu ishirini wenyewe wanapata pesa leo ya watu wote ishirini halafu wale wa mwisho wanapoteza pesa. Jiulize Pesa ya leo hii thamani yake haiwezi kuwa sawa na pesa hiyo ukipata mwaka kesho.

Mimi ushauri wangu ni kuweka pesa yako UTT na mashirika ya hivi badala ya Vicoba ambavyo ni utapeli na wizi mkubwa

 
Ni ukweli mtupu, unawapa watu wakae na hela yako mwisho wa siku shukran yao ni kukukata fees yaan gharama ya wao kukutunzia wakati huo huo bado wanaitumia hela yako kuzalisha zaidi, kuweka hela bank ni ujinga mmoja mkubwa sana.
 
Wengi hawaelewi vzr hii kitu na ilitokea wapi na hasa inawahusu watu gani na hapa ndio tatizo linapoanzia. Kwa ufupi ilianzia Niger kwa wakinamama waliokuwa wanateseka na familia wakati waume zao wakilewa na kutelekeza familia ndipo wakaungana na wakaamua kutengeneza kikundi kitakachowasaidia kukusanya mtaji na kisha kutumia mtaji walionao kuanzisha vibiashara vidovidogo. kwetu hapa kiuhalisia vinatakiwa kuwa vijijini na kwa mafunzo maalum kwa zaidi ya wiki nane.

Shida mjini mmevamia kiuhalisia hivi sio size yenu kabisa na vitaendelea kuwatesa tu. Wako watu vijijini maisha yao yamebadilika sana yuko dada mmoja miaka 15 iliyopita alikuwa na maisha magumu lakini ninapokueleza kwa sasa ameweza kusomesha mtoto mpaka chuo kikuu amejenga nyumba na anamaisha mazuri kwa sasa.

Yuko mwingine alikopa kutoka kwenye mfumo huo akachonga mzinga mmoja wa nyuki lakini mpaka mwaka juzi alikuwa na zaidi ya mizinga 100
 
Hao wakina mama wa huko Niger vimewasaidia??
wengi hawaelewi vzr hii kitu na ilitokea wapi
na hasa inawahusu watu gani
na hapa ndio tatizo linapoanzia...
 
Kwa sisi wataalamu wa Fedha huwezi kuita uwekezaji kama hakuna vitu viwili Risk & Return. sijui kwa kiswahili nisema vipi. Viroba ni wizi tu maana pesa haiendi kwenye uzalishaji wowote lakini kibaya ukitoa pesa kuna faini...
Lema hajaeleweka na watu wengi, ila yuko sahihi
 
Hao wakina mama wa huko Niger vimewasaidia??
Vimewasidia sana kiasi kwamba hao wazungu tunaowaamini walicopy kwao wakafanya marekebisho kidogo na wanatumia kuwafundishia kaya masikini huko Asia na kwingineko hata hapa Afrika
 
Safi sana mkuu, na huo ndo uwekezaji na sio kuwapa watu wasio na shukran wakae na jasho lako
Ukiweka kwenye account inayokupa interest, siyo mbaya. Mbaya ni kuweka kwenye account ambayo badala ya kuzalisha, yenyewe inakucharge. Ukishindwa kuweka kwenye fixed account, basi wekeza kwenye assets/estates.
 
Back
Top Bottom