little master
JF-Expert Member
- Jul 16, 2018
- 2,465
- 4,862
Kama unatumia Imani yako kulithibitisha hilo ni sawa naweza nisikukatalie kwasababu kila mtu ana namna anavyo amini. Ila kuniambia bahari ina utambuzi na ni kiumbe kwangu bado hujatoa hoja ya kutetea hilo na kulithibitisha.Bahari ni kiumbe hai
Aaaah sasa wewe mwenyewe umesemaInasapoti vipi vilivyo hai? Bahari yenyewe ni kiumbe hai mkuu...
Hili ni jambo la kiroho zaidi..
Nakumbuka siku ile nilipokuwa ndani ya maji nilisema maneno haya,
Ewe bahari najuwa ni kumbe cha MUNGU,,
Naomba nirudishe tena baharini....
Nikatoka zng kwenye maji nikajumuika na wenzangu kule kwenye beach part..
Mkuu haikupita week company yng inanitafuta nakwenda tena melini..
-bahari inaweza ikakutaka na
pia inaweza ikakukataa.
- bahari inaweza ikakulilia, ,bahari inakuita pia,
-bahari inasikia pia.
ukiwa deep sea utaelewa...
16 Na wewe uinue fimbo yako, uunyoshe mkono wako juu ya bahari, uigawanye; na wana wa Israeli waingie katikati ya bahari katika nchi kavu.”
Lakini pia tunaona Yona aliepewa agizo na Mungu alipolikata basi alikumbana na vingi21 Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na BWANA akaisukuma bahari kwa upepo mkali wa mashariki usiku kucha, akafanya bahari kuwa nchi kavu, na maji yakagawanyika.
22 Wana wa Israeli wakaingia katikati ya bahari katika nchi kavu; na maji yalikuwa ukuta kwao upande wa kulia na upande wa kusho
Mkuu bahari inaweza ikautulia ,bahari inaweza ikakasirika pia.Aaaah sasa wewe mwenyewe umesema
"Hili ni jambo la kiroho zaidi" ndiyo maana nimesema kwa Imani yako siwezi kusema ndiyo au hapana wewe ndiye unaeamini ila upande wangu bado hujalithibitisha.
Huwa napenda sana kuangalia videos mbalimbali za North Atlantic ocean hasa maeneo yenye north atlantic winter storm si kwamba mawimbi tu ni marefu, bali upepo mkali, mawimbi yanayokuja kutoka directions tofauti, low pressure storms vinaweza kuifanya meli ionekane kama inatupwa hewani nawakati huo meli kubwa ya mafuta au makontena na kuna nyimbo yao wanaita national anthem of the sea.
Kwa wewe mtu wa bahari unaamini ile ni hali ya jiografia ya bahari imebadilika au bahari imekasirika yenyewe?
Enhe; baada ya hapo, kwani si ulikijaribu? Hebu tupee mrejesho.Niliambiwa cha Arusha ni kikali nikawa ninabisha
Mkuu kuna kitu nimekusoma sasa wewe umebase kwenye experience ya bahari (maisha ya melini).Mkuu bahari inaweza ikautulia ,bahari inaweza ikakasirika pia.
Japokuwa upepo na mawimbi vinakwenda pamoja..
Ila vyote ni viumbe vya MUNGU..
Pia unapaswa uelewe kuwa hata hizo bahari tulizonazo duniani zote zina tabia na rangi ya maji tofauti na pia haziingiliani maji yake..
Maana yake ni viumbe tofauti..
Maana yake ni kwmba hizo bahari ni viumbe tofauti
Mimi ni asili ya moto na ninapenda maji sana. Hii imekaaje?Bahari inakuona, inakusikia na inaweza kufanya maamuzi ya ajabu juu yako mpaka watu wakashangaa 😳 unapoiangalia Bahari unaona ni maji tu ila bahari ina uhai, yaani Bahari inajua nini kinaendelea, nini cha kufanya, inajua kila kitu.
Mtawala Xerxes 1 wa Persia aliamua kuiadhibu Bahari baada ya kuona imeharibu daraja alilokuwa amelijenga, akawaita wanajeshi wake wakaanza kuichapa baada ya hapo akalijenga tena daraja na Bahari haikulibomoa tena. Hii inaonesha ni kwa namna gani Bahari ina uhai.
Niliona hata kwenye video moja kuna mwanamke alikuwa akiingia kwenye Bahari anapigwa na mawimbi, ni kama Bahari inachafuka. Ilitaka kumuua ila cha ajabu watu walipokuwa wakimchukua na kumpeleka nje, Bahari inatulia, hakuna mawimbi. Akienda kuingia tu, mawimbi yanaanza kupiga tena, ni kwamba Bahari ilikuwa inamkataa. Watu wenye asili ya moto ndiyo wengi wanaoongoza kufa baharini, kama asili yako ni moto usipende sana kuogelea baharini utakufa.
Mimi ni asili ya moto na ninapenda maji sana. Hii imekaaje?
Ushahidi wa kibaiologia sina mkuu,Mkuu kuna kitu nimekusoma sasa wewe umebase kwenye experience ya bahari (maisha ya melini).
Tunaposema bahari imekasirika, hiyo ni lugha ya kawaida ya binadamu kuelezea hali ya bahari kama tunavyosema mlima umeficha uso wake bila kumaanisha mlima una uso.
Kuhusu bahari kutokuwa na rangi sawa hilo pia si ushahidi kwamba ni viumbe tofauti. Rangi ya maji inaweza kubadilika kutokana na kina, mwanga, chumvi, joto na vitu vingine vilivyomo majini.
Na kuhusu bahari kuwa na tabia tofauti hilo ni sawa kuna maeneo ambayo mipaka ya maji yenye tofauti ya joto la maji, chumvi ya maji au density (uzito wa maji)inaweza kupelekea kuwa na utofauti.
Kwa hiyo kama unatumia neno “kiumbe cha Mungu” kwa maana ya uumbaji wa Mungu, hapo tunaweza kukubaliana kwamba bahari ni sehemu ya uumbaji. Lakini kama unamaanisha kiumbe hai kwa maana ya biology, basi tunahitaji ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba bahari yenyewe ina sifa za kiumbe hai.
Sawa kwa muktadha huo ni jambo la ajabu sana, kimsingi kupitia bahari nimejifunza mengi sana japo si kwakufanya kazi melini, kuna muda nikiwa mwanza nilikuwa naona watu wanakuja kabisa na maji kutoka dar es salaam. Kwa malengo tofauti tofauti sana, swali ambalo sijawahi jibiwa kwanini maji ya ziwa yanaonekana ya kawaida sana mbele ya maji ya bahari?Ushahidi wa kibaiologia sina mkuu,
Ila ni ushahidi wa kufikirisha na kiroho.
Mfano umesema bahari hubadilika rangi ya maji sababu ya kina cha maji ni Kwl, ila kuna utofauti wa rangi ya kina cha maji na rangi ya bahari yenyewe.
Kuna bahari zina rangi blue,zipo rangi kama maji ya mto,kuna rangi nyeusi nk..
Zote hizi huwa zimeweka mipaka baina yao na haziingiliani huoni kama ni jambo la ajabu?
Hili sina experience nalo mkuu,,ila hili la bahari nimejifunza mengi sn especially niliposafiri na meli mbovu toka Surabaya Indonesia to Daresalam.Sawa kwa muktadha huo ni jambo la ajabu sana, kimsingi kupitia bahari nimejifunza mengi sana japo si kwakufanya kazi melini, kuna muda nikiwa mwanza nilikuwa naona watu wanakuja kabisa na maji kutoka dar es salaam. Kwa malengo tofauti tofauti sana, swali ambalo sijawahi jibiwa kwanini maji ya ziwa yanaonekana ya kawaida sana mbele ya maji ya bahari?
Sawa kabisa ni kama wiki 3 zimepita niliona kuna captain alikuwa anahojiwa UTV ni mstaafu kwa sasa aliongea mambo mengi sana moja wapo ni kwamba aliwahi kushuhudia meli ina capsize mbele yao hali ilikuwa mbaya sana, huwa natazama pia hata vipindi vyao muda hali ya hewa ikibadilika wale jamaa wana heshima yao aisee ni kazi ya kiume mno.Hili sina experience nali mkuu,,ila hili la bahari nimejifunza mengi sn especially niliposafiri na meli mbovu toka Surabaya Indonesia to Daresalam.
Ilikuwa safari mbaya ktk maisha yng zaidi ya sinbad baharia..
Ukitaka kuijuwa bahari vzri basi ukutane nayo deep sea na sio Coast Coast.
Kwaiyo hapa mkuu unamaanisha kitulizo cha moto ni maji. Sasa iweje tena bahari iwe hatari kwa moto. Shusha madini.Moto na upepo kinawaka vibaya, na maji utatulia vzr sana
Kabisa mkuu,,sisi tulitakiwa kutumia siku 35 toka Surabaya Indonesia hadi Daresalam,Sawa kabisa ni kama wiki 3 zimepita niliona kuna captain alikuwa anahojiwa UTV ni mstaafu kwa sasa aliongea mambo mengi sana moja wapo ni kwamba aliwahi kushuhudia meli ina capsize mbele yao hali ilikuwa mbaya sana, huwa natazama pia hata vipindi vyao muda hali ya hewa ikibadilika wale jamaa wana heshima yao aisee ni kazi ya kiume mno.
Udongo hufaKama unatumia Imani yako kulithibitisha hilo ni sawa naweza nisikukatalie kwasababu kila mtu ana namna anavyo amini. Ila kuniambia bahari ina utambuzi na ni kiumbe kwangu bado hujatoa hoja ya kutetea hilo na kulithibitisha.
Wavuvi na mabaharia wana siri nyingi sanaa.Kabisa mkuu,,sisi tulitakiwa kutumia siku 35 toka Surabaya Indonesia hadi Daresalam,
Lakini ilitokea hitilafu njiani tukiwa ni siku kumi baada ya safari..
Ilitufanya tutumie miezi 2 njiani ,tena tuna cross deep sea..
chakula hatuna tunakula andazi 1 na maji,,baadhi ya mabaharia wakafyatuka akili tukiwa njiani..
MUNGU kweli kaumba bahari,inatisha sana mkuu kuna kipindi inalia kuna kipindi inakuhurumia na kutulia kabisa..
Uliongea vitu gani na bahari ilikufungukia? hebu jazia nyama tujifunze zaidi mkuu.Mkuu hivi ni uthibitisho gn unahitaji ili uamini kama bahari ni kiumbe cha MUNGU?
Nabii Musa alipokimbizwa na Pharao na jeshi lake alipokuta bahari akaichapa fimbo na bahari ikatii kwa kukatika katikati wakapita salama.
-Siku moja Yesu yupo kwenye mtumbwi na wanafunzi wake wanasafiri akapitiwa na usingizi,,alipoamka alikuta bahari inadhoruba kali sana ,,akaikemea na bahari ikatiii..
Narudi kwko mkuu,,hivi kitu ambacho unakikemea na kukutii sio kiumbe hai?
-Jaribu siku moja ongea mambo ya hovyo baharini kama utatoka salama..
-Kuna siku moja niliwahi kwenda baharini,,nilikuwa nimekwenda ktk beach part fulani hivi,,wakati wenzangu wapo busy na music mimi nilikwenda baharini maji ya magoti,,,nikaongea na bahari na haikupita siku 7 mambo yng yote yalifunguka .
Bahari ni kiumbe cha Mungu mkuu...