Interlacustrine R
JF-Expert Member
- Jan 22, 2022
- 8,365
- 16,444
Hata ardhi nayo ni kiumbe hai, kuna mahali iliamrishwa na Nabii kufunguka na kujifunga ikawaua watu, lilikuwa ni tamko la adhabu ambayo iliombewa kibali toka kwa Mungu baada ya watu kumdhihaki Nabii wa Mungu.Kwasababu swala la bahari kuwa na uhai halina uthibitisho isipukuwa ina support viumbe walio hai
Umesema bahari kuwa na uhai halina uthibitisho Lakini wakati huo huo umekubali bahari isiyokuwa na uhai ku support viumbe walio hai (umejichanganya)
Na kama bahari ni mfu inawezaje ku support viumbe hai???
Nilikaa miezi kama 9 bila kazi nikawa mnyonge sn,Uliongea vitu gani na bahari ilikufungukia? hebu jazia nyama tujifunze zaidi mkuu.
Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
Kwamba Bahari imechapwa bakora na ili kuishikisha adabu🙄🙄Mtawala Xerxes 1 wa Persia aliamua kuiadhibu Bahari baada ya kuona imeharibu daraja alilokuwa amelijenga, akawaita wanajeshi wake wakaanza kuichapa baada ya hapo akalijenga tena daraja na Bahari haikulibomoa tena. Hii inaonesha ni kwa namna gani Bahari ina uhai.
Hakika mkuu lakini bahari haizoeleki,,Wavuvi na mabaharia wana siri nyingi sanaa.
Maji ya bahari yana chumvi, kuoga maji ya chumvi automatically yanatoa nuski na mikosi...Sawa kwa muktadha huo ni jambo la ajabu sana, kimsingi kupitia bahari nimejifunza mengi sana japo si kwakufanya kazi melini, kuna muda nikiwa mwanza nilikuwa naona watu wanakuja kabisa na maji kutoka dar es salaam. Kwa malengo tofauti tofauti sana, swali ambalo sijawahi jibiwa kwanini maji ya ziwa yanaonekana ya kawaida sana mbele ya maji ya bahari?
Hapo kuna vitu 2 usije ukachanganya,, science na dini..Kama unatumia Imani yako kulithibitisha hilo ni sawa naweza nisikukatalie kwasababu kila mtu ana namna anavyo amini. Ila kuniambia bahari ina utambuzi na ni kiumbe kwangu bado hujatoa hoja ya kutetea hilo na kulithibitisha.
Aisee siyo mchezo baharini huwa navuta picha usiku sijui inakuwaje tu.Kabisa mkuu,,sisi tulitakiwa kutumia siku 35 toka Surabaya Indonesia hadi Daresalam,
Lakini ilitokea hitilafu njiani tukiwa ni siku kumi baada ya safari..
Ilitufanya tutumie miezi 2 njiani ,tena tuna cross deep sea..
chakula hatuna tunakula andazi 1 na maji,,baadhi ya mabaharia wakafyatuka akili tukiwa njiani..
MUNGU kweli kaumba bahari,inatisha sana mkuu kuna kipindi inalia kuna kipindi inakuhurumia na kutulia kabisa..
Lakini hapo kwa nyani hapana si sayansi vile vile japo sayansi inaongelea habari za big bang lakini haindoi dhana kwamba hata wanasayansi nguli swala la Mungu lilibaki kama swala binafsi. Mfano Isaac, Nikola, Pascal, na wengine wengi sana walisoma hadi theology.Hapo kuna vitu 2 usije ukachanganya,, science na dini..
Science haitambuwi kama bahari ni kiumbe.
Ila dini zote 2 Christian na Islam inatambuwa kwamba bahari ni kiumbe..upepo ni kiumbe.
Mfano science inasema binadamu tulikuwa nyani na hakuna MUNGU .
Au unaamini dini isemavyo kwmba binadamu tuliumbwa na MUNGU?.
Science inapinga kila kitu ktk dini kwahyo chaguo ni lako mkuu..
Ni hatari na nusu mkuuAisee siyo mchezo baharini huwa navuta picha usiku sijui inakuwaje tu.
Sayansi inasema binadamu ameumbwa au alikuwa nyani ?Lakini hapo kwa nyani hapana si sayansi vile vile japo sayansi inaongelea habari za big bang lakini haindoi dhana kwamba hata wanasayansi nguli swala la Mungu lilibaki kama swala binafsi. Mfano Isaac, Nikola, Pascal, na wengine wengi sana walisoma hadi theology.
Niliambiwa cha Arusha ni kikali nikawa ninabisha
Kwa mtazamo wa sayansi ya evolution, jibu sahihi si kwamba binadamu alitokana na nyani wa leo. Hilo ni kosa linalosemwa sana.Sayansi inasema binadamu ameumbwa au alikuwa nyani ?
nilidhani utatoa ishahidi wa kisayansi kumbe unanukuu vitabu vya stori za kusadikikaMkuu hivi ni uthibitisho gn unahitaji ili uamini kama bahari ni kiumbe cha MUNGU?
Nabii Musa alipokimbizwa na Pharao na jeshi lake alipokuta bahari akaichapa fimbo na bahari ikatii kwa kukatika katikati wakapita salama.
-Siku moja Yesu yupo kwenye mtumbwi na wanafunzi wake wanasafiri akapitiwa na usingizi,,alipoamka alikuta bahari inadhoruba kali sana ,,akaikemea na bahari ikatiii..
Narudi kwko mkuu,,hivi kitu ambacho unakikemea na kukutii sio kiumbe hai?
-Jaribu siku moja ongea mambo ya hovyo baharini kama utatoka salama..
-Kuna siku moja niliwahi kwenda baharini,,nilikuwa nimekwenda ktk beach part fulani hivi,,wakati wenzangu wapo busy na music mimi nilikwenda baharini maji ya magoti,,,nikaongea na bahari na haikupita siku 7 mambo yng yote yalifunguka .
Bahari ni kiumbe cha Mungu mkuu...
vyote vinaelezeka kisayansi gakuna uajabu wowoteUshahidi wa kibaiologia sina mkuu,
Ila ni ushahidi wa kufikirisha na kiroho.
Mfano umesema bahari hubadilika rangi ya maji sababu ya kina cha maji ni Kwl, ila kuna utofauti wa rangi ya kina cha maji na rangi ya bahari yenyewe.
Kuna bahari zina rangi blue,zipo rangi kama maji ya mto,kuna rangi nyeusi nk..
Zote hizi huwa zimeweka mipaka baina yao na haziingiliani huoni kama ni jambo la ajabu?
hiyo ni kawaida tu haithibitishi lolote kuna walipata hapo na hata hawajui bahari iko wapimwaka 1989 nilikwenda dubai kutafuta kazi mimi niliishia darasa la 7, nilihangaika kila siku naamka asubuhi napita kampuni zote ninazoziona mtaani nauliza kazi ikifika saa kumi jioni naenda baharini napumzika bahari ipo mjini nchi imezungukwa na bahari na nyumbani karibu na bahari nikawa na kawaida yangu jioni nikichoka kutafuta kazi naenda bahari nakaa halafu naenda nyumbani, siku moja nipo baharini naangalia bahari nimekata tamaa na kupata kazi nikiwa baharini nikakumbuka kila kitu kimeumbwa na mungu hata bahari inamuabudu mungu, nikasimama nikasongea karibu na maji ya bahari nikasema hivi; wewe bahari mimi na wewe wote tumeumbwa na mungu na wote tunamuomba mungu sasa nakuomba niombee kwa mungu wako na ndie mungu wangu nipate kazi nimechoka kutafuta, baadae nikaondoka kurudi nyumbani asubuhi kama kawaida saa mbili napita mtaa moja naona bus dogo linateremsha wafanyakazi na mabegi nikamuona mfanyakazi mmoja nikamuuliza hii ni kampuni ya nini akaniambia hii kampuni ya kuchimba mafuta baharini akaniambia kama unataka kazi kajaribu ingia ndani muone boss nikaingia nikamuona boss nikaomba kazi nikapata baada ya siku mbili nikapelekwa baharini kufanya kazi nimefanya kazi mpaka mwaka 2017 kumbuka kazi nimeipata baharini na niliomba bahari iniombee na nikapata hukohuko baharini sio nchi kavu
Shule zimefunga week hii ee??Bahari inakuona, inakusikia na inaweza kufanya maamuzi ya ajabu juu yako mpaka watu wakashangaa 😳 unapoiangalia Bahari unaona ni maji tu ila bahari ina uhai, yaani Bahari inajua nini kinaendelea, nini cha kufanya, inajua kila kitu.
Mtawala Xerxes 1 wa Persia aliamua kuiadhibu Bahari baada ya kuona imeharibu daraja alilokuwa amelijenga, akawaita wanajeshi wake wakaanza kuichapa baada ya hapo akalijenga tena daraja na Bahari haikulibomoa tena. Hii inaonesha ni kwa namna gani Bahari ina uhai.
Niliona hata kwenye video moja kuna mwanamke alikuwa akiingia kwenye Bahari anapigwa na mawimbi, ni kama Bahari inachafuka. Ilitaka kumuua ila cha ajabu watu walipokuwa wakimchukua na kumpeleka nje, Bahari inatulia, hakuna mawimbi. Akienda kuingia tu, mawimbi yanaanza kupiga tena, ni kwamba Bahari ilikuwa inamkataa. Watu wenye asili ya moto ndiyo wengi wanaoongoza kufa baharini, kama asili yako ni moto usipende sana kuogelea baharini utakufa.
Ushahidi kwamba bahari ni kiumbe cha MUNGU,,angalia movements za maji kupwa maji kujaa,, nani anafanya yote hayo?nilidhani utatoa ishahidi wa kisayansi kumbe unanukuu vitabu vya stori za kusadikika
Huna unalojuwa mkuu,,jifunze kuheshimu taaluma za watu..Shule zimefunga week hii ee??