Tahadhari kubwa : Madini sio rasilimali ya kudumu, tukiendelea hivi mpaka 2050 yataisha

Tahadhari kubwa : Madini sio rasilimali ya kudumu, tukiendelea hivi mpaka 2050 yataisha

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Wasalam ndugu zangu.....

Kibaya zaidi Kampuni ya kigeni ikimaliza kuchimba inafunga na kuondoka, Itatuachia mashimo + kemikali + ajira zilizopotea.

Kiuchumi tunaita Resource Curse laana ya Rasilimali. Una mali lakini unabaki maskini zaidi.

TUTAPOTEZA VIZAZI 2
Kizazi cha leo kinapata ajira za vibarua.
Kizazi cha 2050 kinapata nini?
Hakuna madini, hakuna kiwanda, hakuna ujuzi. Tunabaki na uchumi wa kutoa huduma tu.

KUONDOA RUZUKU KWA WACHIMBAJI

1. Inaua wachimbaji Wadogo na wakati-90%
Mchimbaji wa jembe na kichungi hawezi kushindana na kampuni yenye mashine ya Dola Milioni 20.
Matokeo:

Watu milioni 2+ wanaojishughulisha na uchimbaji mdogo watakosa ajira, na hawa Kwa asilimia kubwa ndio mgongo wa sekta ya madini. Ukiwaondolea ruzuku ya mafuta, mashine, na leseni rahisi umewamaliza.
Matokeo Ajira zinapotea, vijana wanarudi mtaani.

2. Tunazalisha Uchumi wa Kampuni
Asilimia 100%, sekta inabaki na makampuni makubwa ya kigeni 5 tu.
Yale makubwa yanakuwa makubwa zaidi lakini Wadogo wanakufa.
Hii inaitwa kiuchumi Monopoly na monopoly ni hatari kwa nchi.

3. Tunapoteza Nafasi ya Value Addition,
Tatizo kampuni za kigeni hazipendi kujenga viwanda, Zinapenda kuchimba na kukimbia.
Mchimbaji mdogo akisaidiwa kidogo anaweza kujifunza kuchuja, kukata na kupamba mawe hapa hapa.
Lakini kampuni kubwa inachimba ghafi inaenda kusindika Dubai. Tunaipoteza ajira ya viwandani + mapato ya ushuru wa viwanda.

4. Nchi zote zilizofanikiwa na madini zilianza na kuwalea wachimbaji wao.
Afrika Kusini serikali iliwawezesha wadogo kwanza ndipo wakawa na kampuni kubwa.

Tukisema jisimamie mwenyewe tangu mwanzo ni kama kumtupa mtoto mchanga ajilee.

SULUHISHO LA KIUCHUMI

Badala ya kumpa mchimbaji milioni mpe hivi..
1. Kituo cha Pamoja cha Kuchuja Madini- Serikali ijenge kila mkoa, Mchimbaji alipe ada ndogo.
2. Benki ya Madini - Mikopo ya bei ndogo ya kununua compressor na pampu.
3. Soko la Uhakika - Serikali inunue madini kutoka kwa wadogo kwa bei ya soko.
4. Mafunzo + Leseni ya Bei Ndogo, Mwezeshe kuwa mtaalamu si ombaomba.

SULUHISHO LA HARAKA

Kiuchumi hakuna ndiyo au hapana kamili Kuna namna gani.

1. Tofautisha Wachimbaji
Mchimbaji mkubwa wa kampuni asipewe ruzuku kwasababu ana uwezo.
Mchimbaji mdogo na wa kati apewe msaada wa mwanzo kama vile mkulima.
Mfano: mashine za kukodisha, mafunzo, na leseni ya bei ndogo.

2. Badilisha neno Ruzuku kua Mazingira Wezeshi.
Badala ya kumpa mchimbaji pesa taslimu, mpe barabara ya kwenda mgodini, umeme wa bei ndogo, kituo cha kuchuja madini cha serikali, na soko la uhakika. Hii haipotezi pesa bali inajenga miundombinu.

3. Mkataba Mpya Kodi dhidi ya Huduma,
Serikali inachukua kodi nyingi kwenye madini, Basi na irudishe kwa huduma. Kila shilingi 100 ya kodi ya madini shilingi 20 irudi kwenye eneo la mgodi kwa hospitali, shule na
Hii sio ruzuku hii ni uwekezaji, Serikali inatoa leo, kesho inarudi kwa njia ya kodi.
 
Back
Top Bottom