Uchaguzi 2020 Tahadhari kuhusu Uwepo wa Vituo Feki/ Bubu/ Hewa vya Kupigia Kura

mama D
Em njoo huku na zile takwimu zako.. Kama Ni za kweli kwa nini ccm wanahangaika kutengeneza vituo feki/bubu/hewa?!
CCM wameshashinda kinachofanyika sasa ni kumalizia zile kura million 7 Tanzania iwe ya kijani. Upo???
POVU ruksa😂😂😂😂
 
Yaani haya mambo ya wizi yanaratibiwa na serikali kweli?
Naona kama muujiza kabisa.
Labda we mgeni. Bila wizi ccm wangesahaulika kitambo. Ila mwaka huu kazi wanayo. Orodha ya wahusika wote inaandaliwa kwa ajili ya hatua kali
 
Ccm itaongoza kwa miaka miamoja ijayo Tanzania

Tanzania haiwezi kuongozwa na mtu aliyetengenezwa na Mabeberu, ondoa kwenye fikra zako

Pia Tanzania hatutaki ushoga,
Jiandae kuwa mpinzani kwa heri au kwa Shari,angalia usije ukapoteana humu baada ya 28th
 
Chadema wote wanajua kabla ya uchaguzi walisha shindwa kwasasa wanaokoteza sababu na baada ya uchaguzi hawatakosa sababu.
 

Yes, unasema kweli kabisa..

Ni kweli liko lundo la kura feki na zimeshapigwa tayari zikiwa na tiki (√) kwa mgombea Urais wa CCM - Jiwe..

Huu ndiyo mtindo wa wizi wa CCM katika kila uchaguzi...

Uwepo wa vituo hivi feki (hewa) lengo lake ni kupitishia hizi kura feki..

Zingine zitapitia kwenye vituo hivyo hivyo halali iwapo kituo hakitakuwa na wakala aggressive..

Tukumbuke wasimamizi wa vituo vya kupigia kura ambao wengi ni watumishi wa umma (walimu, manesi, maafisa kilimo na mifugo, madaktari, watendaji vijiji na mitaa nk nk )wana maelekezo maalumu ya namna ya kufanikisha zoezi hilo la wizi wa kura ili kumshindisha Magufuli.

Hawa watumishi wametishiwa kufukuzwa kazi iwapo kituo anachosimamia mtumishi yeyote wa umma itaonesha Tundu Lissu (CHADEMA) amemzidi Magufuli (CCM) kwa idadi kura zilizopigwa kituoni hapo..!

Solution ya hili ni kuwadhibiti tu. Yaani iwe toe to toe, face to face ktk kila stage na wakionekana wachezee kichapo cha haja bila kuwaonea haya..
 
Mnatapatapa tu, kipigo kiko palepale! Kura zote kwa ccm
 
Mkuu, ni wapi huko?
Kumbe ndo maana maccm yanasema lzm yashinde, Ni kwa sabb yanajua yameandaa mikakati ya wizi hatari.

Kama ccm wanapendwa Kama wanavosema, si waache wananchi wachague?!
Ilikuwa Mbeya mkuu.
 
Chadema wote wanajua kabla ya uchaguzi walisha shindwa kwasasa wanaokoteza sababu na baada ya uchaguzi hawatakosa sababu.
Umeona hiyo video clip? Na wewe umeona hayo Magunia ya Mahindi kama Wenzio?
 
Vyama vya Upinzani waunganishe nguvu kuijulisha dunia udhalimu huu mana kumbe tupo chini ya Utawala wa Kikoloni mana inaonekana hatuna tena namna ya kisheria/rasmi ya kuwatoa madarakani wakoloni hawa weusi.
Mkuu, upo sahihi.. lkn usidhani kuwa vyama vyote vya upinzani, ni vya kweli. Vingi ni vya ccm. Kuna vilivyoanzishwa na ccm, na vipo vilivyonunuliwa na ccm
 
Muda watakaokuwa wanayapeleka dipo wananchi wawe makini.
Sio Lazma wayabebe. Wanapeleka namba Tu Tume wanatangaza. Hivyo wananchi wakisubiria kuona malori itakuwa ngumu.
 
Jiwe ametufikisha hapa anaogopa uchaguzi wa haki kuliko hata kumuogopa Mungu.
Ila maajabu yanaenda kutokea safari hii, Mungu hawezi kuwaacha hawa mawakala wa shetani waendelee kututesa,ndio mana wananchi wana ujasiri sana kuliko kipindi chochote
 
Tulimuomba Mungu akaiondoa Korona ili watanzania wasiangamie .
Sasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ni wakati wa Kumwomba Mungu ili Wasimamizi wa Uchaguzi wanaotaka kuvuruga nchi na kuwaumiza wananchi wao ndio waangamie kama Korona ilivyoangamia na kutoweka.
Mungu anaweza na Mungu sio Mwanachama wa CCM wala Chadema wala ACT wala chama chochote bali ni Mungu wa wote na ni Mungu mwenye kuhukumu kwa haki ili wanaotenda Uovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…