Humu kuna watu watu wanajifanya wateja lakini ni matapeli walikubuhu.
Niliweka tangazo langu la kuuza maziwa hapa, akaja kaka mmoja mtu mzima kwa makadirio anaumri wa 36-40 anakaa kimara, akanipm namba kuwa anahitaji, nikampelekea kama mara atatu akanilipa cash.
Baada ya hapo, kuna siku akaagiza tena maziwa lakini kabla ya hapo alidai alikuwa anaumwa, sikutaka kupeleka maziwa kwakua ratiba ilinibana akanibembeleza sana, ilikuwa jumapili nikampelekea maziwa hadi ninapomkuta hakuwepo, nikampigia akasema bado anaumwa hvo nimpelekee nyumbani kwake akanielekeza, nikampelekea kufika pale nikampa nikawa nasubur hela akatoka akasema hapa sina hela twende kwenye ATM nikakutolee, tukatoka hadi suka kufika akaingia kwenye ATM akatoka anajisemesha, "kadi sijui imefanyaje,imeisha muda wake inabidi kesho nikaishughulikie" mim nikaona ananichekewesha nikamwambia utanitumia hyo kwenye sim, akasema sawa, Mim nikaondoka.
Haukupita muda mrefu akanitext kuwa anaazima 120000 kwa kua ile siku asingeweza kufanya miamala ila kesho yake ambayo ni jumatatu atanirudishia pamoja na ile nyingine, nikamwambia sawa, nikamtumia.
Nikakaa wiki 1,2,3 nikamtext vipi, akasema ooh!! Nipo Arusha nimesafiri, nikamwambia poa, nikaaa wk 3 tena mbele, akanitext "Ooh nimepata dharula naenda morogoro naomba nipe 200000 " nikawaza huyu mtu hela ya kwanza hajanipa alafu anataka tena hela, nikamwambia sina, etii ooh!! Nipe hata uliyonayo nikamwambia nina hela ya kula tu, eti nipe hyo hyo, nikamwambia sina, akasema naomba niazimie, kwa kua alinichosha akili nikamwambia mim pesa ipo mikonon mwa watu labda usubir warudishe alafu nikaachana nae, akanisumbua siku 3 anataka hela, nikaachana nae,
Mwez wa 11nikamtext nahtaj hela yangu, akawa anajibu kama atatuma, alafu anakaa kimya, nikatumia mbinu zote kumdai lakini wapi, mwisho akawa hapokei sim anadanganya hayupo kasafiri, baadae akaniblock whatsapp, na call nikawa nikipiga naambiwa sim bze 24hrs,
Nikimuangalia kwenye sim yangu nyingine namuona online na nikipiga inaita, nikamtafutia target nikiwa na rafiki zangu nikampata hewan nikatolea uvivu na nikamwambia nitakutangaza watu wote watajua tabia yako ya utapeli, baada ya kuona hvo wiki iliyopita akaanda polisi eti nimemtukana, nikapigiwa sim na polisi nikamwambia usijali sipo nikirudi tu nakuja, Nikawapigia wanasheria 4 tofauti mmoja ni member humu nikawaeleza nin nifanye na wawili kwakua wapo Dar wakaniambia wataisimamia nikawa sina shaka.
juzi akapiga yeye tapel kwa namba ya halotel eti anajifanya polis, nikamtuliza bila woga na nikamwambia nipe maelekezo nimuone nani, akajikanyaga na sauti yake ya kishamba nikakata sim yangu, naona anatafuta mtaji hato pata na deni langu atalipa.
ANGALIZO:
Huyo kaka namuonaga sana hapa kuuliza bei vitu, hana kazi inayoeleweka anajifanya fundi, mtalizwa.