The Mafia
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 257
- 545
Habari,
Kuna Wizi Mpya Upo Stendi Za Daladala, hasa asubuhi muda ambao usafiri unasumbua, anatokea jamaa karibu yako nae anajifanya kulalamikia ugumu wa usafiri, na wewe unachukulia ni abiria mwenzio mnaweza kuzoeana kwa muda mkiongelea adha za usafiri, baada ya muda linatokea gari private unakuta wanatangaza kuwa wanafika eneo ambalo nawe ndio unaelekea kwa gharama ndogo kabisa ya sh 1000 (Kumbuka katika story ulishamwambia uyu jamaa wa standi unapoelekea)..
Limemtokea Mtu wangu wa karibu kabisa leo asubuhi, gongo la mboto, alikuwa anaelekea mwenge akaambiwa ad mwenge ni sh 1000, tena anashawishiwa na uyo jamaa ambae walizoeana kwa muda mfupi apo stendi, kwamba kwa sababu ya ugumu wa usafiri na wamekuwa pamoja muda wote uo hivyo anashauri wapande gari hilo, wawahi makazini , tena uyo jamaa ni mzee mtu mzima kabisa ad mvi kichwani kiaina.
Wakawa jumla watu wanne kwenye gari, yaani dereva , Yule jamaa wa stendi , na mtu mwingine ambaye alikuwepo na dereva kabla yan walikuja pamoja na dereva kama na yeye ni abiria, pamoja na uyu Mama (jumla wanne).
Wameendelea na safari ad kufika maeneo ya banana, akashangaa gari linachepukia njia fulani kulia, akuuliza kitu alidhania labda ni shortcut, mda mchache anashangaa watu wale wawili pale nyuma pamoja na Yule mzee wa stendi wamembadilikia wote wamemshikia visu, wanamtaka simu zake zote na namba za siri za mitandao hiyo, mpesa alikuwa na 500,000 airtel money 200,000 (Pesa za michango ya harusi ya binti yake}, aisee wamemchukua pesa zote, begi lake la nguo, pochi, simu, wakamuacha pori uko na nguo alizovaa tu, hivyo akatembea kutoka uko pori ad banana, kuomba nauli kwa wasamalia aweze kurudi gomz alipotokea.
Jamani tuweni makini na hizo private hali ni mbaya sana.