Tahadhari kwa wapenzi wa supu ya pweza

Tahadhari kwa wapenzi wa supu ya pweza

Hivi karibuni niliamua kufanya biashara ya Pweza hivyo nikaona ni vyema nifanye utafiti wa kina kabla ya kuanza,hii ni biashara nzuri hapa Dar es salaam na mtaji wake sio mkubwa pia inatoa fursa kwa vijana wetu.

Kilichonishtua ni kuwa daktari mmoja alinieleza kuwa Pweza huongeza protein muhimu mwilini na hawana uhusiano na kuongeza Nguvu za kiume wala si kichocheo cha body metabolism.

Hapo nikapata shauku ni kwa nini wateja wa hii kitu hupata Nguvu za ziada za mambo ya kikubwa pindi tu walapo hao pweza au kunywa mchuzi wake?

Jibu lilinistua sana maana hata mie ni mpenzi wa hawa Pweza na hata supu yake. Kumbe wauzaji huwa wananunua dawa ya kuongeza nguvu za kiume Viagra aina ya Sildenafil na kuchemshia Pweza kabla ya kuwakaanga.

Nikafanya uchunguzi kwa vijana kama wanne wanaofanya wanaofanya hii biashara maaeneo ya Ferry na Kariakoo wakathibitisha kuchanganya na Viagra.

Sikuishia hapo nikaenda kwenye Pharmacy moja na kudadisi ambapo Mfamisia mmama mtu mzima alibainisha kuwa ni kweli ana wateja wengi sana wa Viagra hio ambayo ni mahususi kwa kuchanganya na Chakula au Kinywaji.

Aisee nimekoma kula Pweza wa magengeni na sikuwa na hamu ya hio biashara nono. Nawashauri wapenzi wa Sea Foods hasa Pweza wanunue moja kwa moja Sokoni Ferry na waandae nyumbani vinginevyo with time Nguvu za kiume zitaathirika kwa kutumia Viagra bila kujua.

Nafunguka funguka.

Hiyo ni kwa Dar es salaam ndio wana uhun huo....
Njoo jijin Tanga ujipatie supu ya pweza..... Kwan pweza wana kias kingi cha madin ya zinc amboyo huwanya vijana wengi kua marijal pind nguvu hizo zikiwa hafif.
 
Hii imewagusa wengi na wengi walikuwa hawajui.

Nafunguka fung'uu.

Umehadithiwa nawe umekuja kutuhadithia..haimaanishi kuwa upo sahihi..maana ushaanza kujiona mkombozi wakati unaweza kuwa sababu ya kuziba rizki za watu kwa kusambaza maneno ya kuambiwa..
 
WALA PWEZA SIKIENI HII Hivi karibuni niliamua kufanya biashara ya Pweza hivyo nikaona ni vyema nifanye utafiti wa kina kabla ya kuanza. Hii ni biashara nzuri Hapa Dar na mtaji wake sio mkubwa pia inatoa fursa kwa vijana wetu.

Kilichonishtua ni kuwa daktari mmoja alinieleza kuwa Pweza huongeza protein muhimu mwilini na hawana uhusiano na kuongeza Nguvu za kiume wala si kichocheo cha body metabolism.

Hapo nikapata shauku ni kwa nini wateja wa hii kitu hupata Nguvu za ziada za mambo ya kikubwa pindi tu walapo hao pweza au kunywa mchuzi wake? Jibu lilinishtua sana maana hata mie ni mpenzi wa hawa Pweza na hata supu yake.

Kumbe wauzaji huwa wananunua dawa ya kuongeza nguvu za kiume Viagra aina ya Sildenafil na kuchemshia Pweza kabla ya kuwakaanga. Nikafanya uchunguzi kwa vijana kama wanne wanaofanya hii biashara maaeneo ya Ferry na Kariakoo wakathibitisha kuchanganya na Viagra.

Sikuishia hapo nikaenda kwenye Pharmacy moja na kudadisi ambapo Mfamisia mmama mtu mzima alibainisha kuwa ni kweli ana wateja wengi sana wa Viagra hio ambayo ni mahususi kwa kuchanganya na Chakula auKinywaji. Aisee niliacha kula Pweza wa magengeni na sikuwa na hamu ya hio biashara nono.

Nawashauri wapenzi wa Sea Foods hasa Pweza wanunue moja kwa moja Sokoni Ferry na waandae nyumbani vinginevyo with time Nguvu za kiume zitaathirika kwa kutumia Viagra bila kujua.
 
Imekula kwako

Hahahaha jamaa kanitisha kweli,nilikuwa mpenzi kweli wa hiyo kitu japo haikuwa kwa lengo la kujiongezea chochote ilikuwa kama bite tu but hamu yote imenitoka...nasubiri aniambie kuhusu ngisi,nao nawapenda ila nahisi nao wanakuwa wanafanyiwa mchezo huo.
 
Hata Ngisi wanachemshiwa Viagra pia

Nashkuru mkuu kwa taarifa,sitakaa niwaguse tena,biashara za kibongo ni za kizushi zushii hadi kwenye afya za watu...me nikiwala kama kiburudisho tu kumbe wanatuekea viagra..what for!!!sijui kama nilishawahi kukutana nayo ila naamini wote wamoja bora niende feri nichukue wakaandaliwe home mtaani tena mimi hawanpati.
 
Anayetaka dawa ya hospital inayosaidia nguvu za kiume ani pm atafanikiwa.
 
Dawa ya nguvu za kiume watu wanazo na haina haja ya mapweza na hayo maviajira tatizo ni elimu tu, anayetaka kuwa rijali ani pm tusaidiane na tatizo kwishinei.
 
Simulizi za pweza kuongeza nguvu za kiume halijaanza Dar bali visiwani...
 
Uchunguzi wa ziada ni kuwa kiwango cha Viagra ni cha juu Sana kinachochanganywa na athari zake ni mbaya
Hapa sikubaliani na wewe kaka. Uchakachuaji wa dawa tunaita "Adulteration", na hufanywa kwa kutumia bidhaa ya bei nafuu ili kuzidisha faida. kidonge kimoja cha viagra huuzwa kwa sh 2000 hadi 3000/=, na supu ya pweza bakuli moja sh 200/=!
Utawekaje dozi kubwa zaidi (zaidi ya kidonge kimoja kwa kila bakuli) halafu uuze kwa 200/= bakuli moja na kupata faida?
Hapa umetia chumvi na kuharibu ladha ya story na research.
 
Hii ni maneno mbofu mbofu ngoja yeye akaulise mama Yeyoo
 
Ndugu wapendwa mi nimpenzi was pweza!!na supuyake naomba niongeeukweli tujiridhishe tusiaribu biashara za watu!!!binafsi nilionja sehemu nikaamua kuanza kununua jmomsi feri!!tunachemsha wenyewe akuna kinachpwekwa ukwelisiku nikinywa hii supu simimi mtaani nachemsha nyingi na Jirani zangu mwenye chakusukumia nasupu analeta!!nawaambia sikunikionja huwa namrarua madidy vilivyo kuna kipindi niliiogopa kabisa inawezanivunjia unyumbawangu wakatimwingine ajashusha hata pochi natakakuonja jikoni!!!

Ushauri nendanunua ombamaelekezzo jinsi ya kupika!!pikamwenyewe usiweke anything ujehumu kutijuza
 
Kama huna magonjwa yanayochangia upungufu wa nguvu za kiume k.v kisukari,figo, presha magonjwa ya mfumo wa chakula k.v vidonda vya tumbo n.k. Usihangaike na dawa za kuongeza nguvu za kiume unajiumiza bure.unachotakiwa ni kuwa na mtindo bora wa ulaji kila kitu kitakuwa sawa.booster ya nini kwa umri wa miaka kati ya 15-49 ? Utachosha hiyo penis mapema acha kabisa!
 
Watu mnapenda ngono sana, nikuulize, mnajifunzia wapi haya makitu??
Kuongezea chukua alluha kunywa na maziwa. Ikiisha jazia namajiyauvuguvugu njoo humu kama hujaniita prof pdidy
 
Huu utafiti ni kweli na kwa upande wa pili ni wa uzushi na hauna mantiki kwa sababu uko.general

nijuavyo mimi.SEA FOOD... Kwa.kawaida ni source kubwa ya zinc... Sasa nani asyejua kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya zinc na viungo vya sex??? na kufanya uume uweze kuerect kwa mda mrefu!!!!

Kwa dsm kusikia wafanyabiashara wanaweka viagra ktk vyakula ni jambo lisiloshangaza coz wafanyabiashara wengi wa dsm hawajali utu au madhara ya kiafya.. Hujali pesa tu.......


Si tu ktk pweza lakin pia ht juice za matunda huku mitaani yanatengenezwa kwa matubda hata yaliyooza

ukienda katika mapishi ya mama ntilie hadi nyanya zilizooza zinatumika
 
Kwanini ubusti mzigo na viagra?

Aisee mkuu umeuliza swali nililotaka kuuliza,sijui hawa jamaa ni wanaenda kunywa hiyo supu ya pweza kwakuwa wana matatizo kwny mitarimbo yao au laa

Btw sijawahi kuinywa hata siku moja kwsbb sioni sababu na niko vizuri sanaaaa kama farasi!!!

Ashe Engai.
 
Back
Top Bottom