kombomshana
Member
- Sep 2, 2013
- 88
- 14
Hivi karibuni niliamua kufanya biashara ya Pweza hivyo nikaona ni vyema nifanye utafiti wa kina kabla ya kuanza,hii ni biashara nzuri hapa Dar es salaam na mtaji wake sio mkubwa pia inatoa fursa kwa vijana wetu.
Kilichonishtua ni kuwa daktari mmoja alinieleza kuwa Pweza huongeza protein muhimu mwilini na hawana uhusiano na kuongeza Nguvu za kiume wala si kichocheo cha body metabolism.
Hapo nikapata shauku ni kwa nini wateja wa hii kitu hupata Nguvu za ziada za mambo ya kikubwa pindi tu walapo hao pweza au kunywa mchuzi wake?
Jibu lilinistua sana maana hata mie ni mpenzi wa hawa Pweza na hata supu yake. Kumbe wauzaji huwa wananunua dawa ya kuongeza nguvu za kiume Viagra aina ya Sildenafil na kuchemshia Pweza kabla ya kuwakaanga.
Nikafanya uchunguzi kwa vijana kama wanne wanaofanya wanaofanya hii biashara maaeneo ya Ferry na Kariakoo wakathibitisha kuchanganya na Viagra.
Sikuishia hapo nikaenda kwenye Pharmacy moja na kudadisi ambapo Mfamisia mmama mtu mzima alibainisha kuwa ni kweli ana wateja wengi sana wa Viagra hio ambayo ni mahususi kwa kuchanganya na Chakula au Kinywaji.
Aisee nimekoma kula Pweza wa magengeni na sikuwa na hamu ya hio biashara nono. Nawashauri wapenzi wa Sea Foods hasa Pweza wanunue moja kwa moja Sokoni Ferry na waandae nyumbani vinginevyo with time Nguvu za kiume zitaathirika kwa kutumia Viagra bila kujua.
Nafunguka funguka.
Hiyo ni kwa Dar es salaam ndio wana uhun huo....
Njoo jijin Tanga ujipatie supu ya pweza..... Kwan pweza wana kias kingi cha madin ya zinc amboyo huwanya vijana wengi kua marijal pind nguvu hizo zikiwa hafif.