Tahadhari: Makundi ya Bongo flavour yanaweza kusambaratika

Tahadhari: Makundi ya Bongo flavour yanaweza kusambaratika

ntemintale

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2016
Posts
952
Reaction score
1,874
Wasanii wengi wa Bongo Flavour wameamua kujiunga na kufanya music pamoja kama makundi. Ni jambo jema na zuri kabisa. Tunapata music mzuri wenye radha nzuri tofauti kutoka kwao. Wanasaidiana na kuinuana kimziki katika level za juu. Lakini hebu tujikumbushe makundi ya music yaliyokuwa bora na baadae kutawanyika au kupoteza mwelekeo kimuziki au pengine kufunikana na kusuasua.

1. Boys 2 men
2. Back street Boys
3. West life
4. P square
5. Destiny Child
6. Black eye pies
Je, nini kiliyasibu makundi haya, yakadorora kimziki au pengine kila mmoja kushika njia yake?

Basi makundi ya mziki ya Bongo flavour yachukue tahadhari kabla hayajafikwa na dhahama kama hii.

Hebu chukua kundi moja la mziki wa bongo flavour hapa Bongo then lipe miaka 10 mbele. Je litakuwaje?

Tafakari na chukua hatua.

USHAURI: Ni vizuri wanamuziki wetu wakasaidiana katika mawazo na collaboration/Featuring/Duet zaidi kuliko kufanya kazi kama makundi. Makundi hayana mwisho mzuri.
 
HEBU ANGALIA TMK ZOTE MBILI TENA ANGALIA TIPTOP CONNECTION FULL KUPOTEANA MKUU POINT YAKO IKO SAWA COZ MPAKA SASA HAKUNA KUNDI KUBWA LILOSIMAMA VZR ZAID YA WABONGO KUJIUNDIA VILABEL UCHWARA.
 
Kuna hii kitu tunajichanganya:
Mkijoin forces mtafanikiwa iwapo you are after the same goal through the same path.
If not that, then you cant hold that longer.
Sasa pale mkiwa mmezidiana kwenye progress, tatizo linaanza.
Remember, Life is business. I will stay if i get what i expect.

This is why groups ambazo hazina mipaka ndo zinadumu.
 
PSquare watoe hapo, bado bank account yao ina alert
 
HEBU ANGALIA TMK ZOTE MBILI TENA ANGALIA TIPTOP CONNECTION FULL KUPOTEANA MKUU POINT YAKO IKO SAWA COZ MPAKA SASA HAKUNA KUNDI KUBWA LILOSIMAMA VZR ZAID YA WABONGO KUJIUNDIA VILABEL UCHWARA.
Angalia mwandiko wako mkuu
 
Back
Top Bottom