TAHADHARI: Mboga za majani wanazokula wakazi wa Dar ni sumu tupu

Niliamua kulima mbele ya nyumba kuna sehemu ndogo iko wazi huu mwaka wa 5 sinunui mboga asilani. Naweka kila kinachoweza kuota kidogo kidogo. Mwaka jana nilipanda biringanya miche kama 8 nilikuwa navuna ndoo inajaa. Hapo hapo niliweka miche 4 ya papai kufanya utafiti nayo. Nafanya zaidi nikitoka kazini na weekends. Wadada hawapendi hizo kazi but kumwagilia wanasaidia ila akimwagilia jioni asubuhi nawahi kuamka namwagilia maana wanalipua pia kama huingii sana. Ninasupply pia kidogo kazini kwangu kwa sababu zinakuwa nyingi familia yangu haiwezi kumudu kutumia zote. Majirani zangu wanatumia pia kila wanapohitaji. Inawezekana, kama huna eneo panda kwenye makopo na ndoo. Nina mpili pili 1 tu lakini umezaa sana sana nimegawa sana pilipili mafungu kwa mafungu na bado uko fiti.
 
Unaweza kuniunganisha kwenye hiyo supply chain yako?
 
Unaweza kuniunganisha kwenye hiyo supply chain yako?

Sitaweza, Mboga sio nyingi sana, bustani ni ndogo tu ya kutumia mimi mwenyewe ila mboga zinakuwa nyingi hatuwezi kumaliza ndio maana nawauzia pia ofisini nilipo ambapo pia hazitoshelezi mahitaji yao, nawaletea mara 1 kwa wiki kila mmoja mafungu anayohitaji halafu naacha ichipuke tena, lakini wangependa kupata karibu kila siku jambo ambalo kwa sasa haliwezekani.
 
Ongeza uzalishaji, huo ni ujasiriamali mzuri utakutoa biashara ipo
 
Mbezi beach sehemu gani?
 
word
na zingine zinashinda zinakojolewa na wapita njia, Mungu atusaidie
 

tunapanda majani/ukoka na kuweka parking, kazi kweli kweli
 
Ongeza uzalishaji, huo ni ujasiriamali mzuri utakutoa biashara ipo

Tatizo wasaidizi wa www.com ni shida. Mfano; Ili niupate mchicha inabidi kuusimamia kufukuzia ndege wasiule unapoanza kuota. Ukiondoka dada anashinda kwenye TV anaangalia movie ukija weekend kucheck unakuta kipara umeliwa wote. Niliweka hadi kijana ashughulike tu na hiyo bustani maana inanilipa na ingemlipa pia, hakuweza hata kuinulia tu biringanya zilizokuwa kubwa zinakaa chini kwa miti achilia mbali kuweka mbolea. Najitahidi asilimia kubwa nafanya mwenyewe na muda ni mchache, eneo ni dogo, labda nikistaafu nitahamia shamba kabisa.
 
Mboga za majani nazo nadhani kila mtu ajifunze kutengeneza bustani yake mwenyewe hata simple tu kama hii....
 

Attachments

  • 9604_1173130409366122_2132786412911108260_n.jpg
    13.4 KB · Views: 99
Mboga za majani nazo nadhani kila mtu ajifunze kutengeneza bustani yake mwenyewe hata simple tu kama hii....
Nimeshafanya hivyo before nitakueleza wapi kwenye maongezi yetu. Mwenye nyumba wangu aliniiga sasa watoto na wajukuu wake huko ughaibuni wanatumia mapipa yangu.
 
Nimeshafanya hivyo before nitakueleza wapi kwenye maongezi yetu. Mwenye nyumba wangu aliniiga sasa watoto na wajukuu wake huko ughaibuni wanatumia mapipa yangu.
Hii ni nzuri hata kama huna ardhi ya kutosha unaifanya tu
 
Kwani during week days hauishi hapo? Kwanini ustuke weekend kuwa spinach imeliwa na ndege
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…