Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Ili Tanzania iwe imara na hata CCM iwe imara kwa miaka mingi ijayo tunahitaji Tundu Antiphas Lissu awe rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania hata kwa miaka 5 tu!!
Kwa nini nasema hivi??!
Tanzania yetu ya leo imefika hatua ya kutoweza kupata mabadiliko ya kudumu chanya yatakayokaa na kustawi kwa muda mrefu kwa sababu tu tuna katiba mbovu kupindukia na mtu pekee wa kututoa kwenye huu mtego tena vizuri ni Tundu Antiphas Lissu tu.
Katiba tuliyonayo Tanzania inaweka madaraka makubwa sana kwa Rais, kiasi ambacho Rais anaweza ku control Bunge na Hata Mahakama. Kwa stahili hii tusahahu kabisa kuwa na maendeleo ya kudumu ya watu na vitu maana unaitaji Rais mwenye Hekima za Mfalme Suleiman ili uendelee kwenye mfumo huu.
Mchanganyiko wa mfumo wa CCM kutoweza kumcontrol Mwenyekiti wake hata akikosea, ukiongeza na Katiba mbovu tulionayo Tanzania inayoweka madaraka yote kwa Raisi kamwe haviwezi kuipa Tanzania maendeleo ya kweli na kila siku tutakuwa tunajiuliza tumekosea wapi!!
Kama ni kipindi muhimu cha system kuamua mustakabali sahihi wa maendeleo ya nchi yetu basi ni kwenye uchaguzi huu kwa sababu tunamuitaji sana Tundu Antiphas Lissu ili atuwekee Katiba Mpya ya Wananchi itakayopunguza, nguvu na madaraka ya Rais, itakayoweka Bunge huru na imara la kutunga sheria na kuisimamia serikali, itakayoweka Mahakama huru na imara itakayotafsiri sheria vizuri na kuwalinda kweli watanzania dhidi ya udhalimu wa aina yeyote ile.
Lissu pia ataweka Katiba Nzuri na imara itakayo vifanya vyombo vya dola kuwa huru na kufanya kazi zake kwa weredi na kuzingatia taaluma.
Huu ni wakati sahihi wa kumuweka Tundu Antiphas Lissu Ikulu.