Tahadhari na ushauri kwa system: Msimwonee haya mtu, akishindwa achaneni naye na akishinda atangazwe

Ili Tanzania iwe imara na hata CCM iwe imara kwa miaka mingi ijayo tunahitaji Tundu Antiphas Lissu awe rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania hata kwa miaka 5 tu!!

Kwa nini nasema hivi??!
Tanzania yetu ya leo imefika hatua ya kutoweza kupata mabadiliko ya kudumu chanya yatakayokaa na kustawi kwa muda mrefu kwa sababu tu tuna katiba mbovu kupindukia na mtu pekee wa kututoa kwenye huu mtego tena vizuri ni Tundu Antiphas Lissu tu.

Katiba tuliyonayo Tanzania inaweka madaraka makubwa sana kwa Rais, kiasi ambacho Rais anaweza ku control Bunge na Hata Mahakama. Kwa stahili hii tusahahu kabisa kuwa na maendeleo ya kudumu ya watu na vitu maana unaitaji Rais mwenye Hekima za Mfalme Suleiman ili uendelee kwenye mfumo huu.

Mchanganyiko wa mfumo wa CCM kutoweza kumcontrol Mwenyekiti wake hata akikosea, ukiongeza na Katiba mbovu tulionayo Tanzania inayoweka madaraka yote kwa Raisi kamwe haviwezi kuipa Tanzania maendeleo ya kweli na kila siku tutakuwa tunajiuliza tumekosea wapi!!

Kama ni kipindi muhimu cha system kuamua mustakabali sahihi wa maendeleo ya nchi yetu basi ni kwenye uchaguzi huu kwa sababu tunamuitaji sana Tundu Antiphas Lissu ili atuwekee Katiba Mpya ya Wananchi itakayopunguza, nguvu na madaraka ya Rais, itakayoweka Bunge huru na imara la kutunga sheria na kuisimamia serikali, itakayoweka Mahakama huru na imara itakayotafsiri sheria vizuri na kuwalinda kweli watanzania dhidi ya udhalimu wa aina yeyote ile.

Lissu pia ataweka Katiba Nzuri na imara itakayo vifanya vyombo vya dola kuwa huru na kufanya kazi zake kwa weredi na kuzingatia taaluma.

Huu ni wakati sahihi wa kumuweka Tundu Antiphas Lissu Ikulu.
 
Hii inaitwa devil's advice.

Yaani mshaona hampati kitu sasa mnawaandaa watanzania kisaikolojia kwa kuvuruga amani ya nchi yetu baada ya matokeo kutangazwa.

Mtashangaa this time hatutakubali kufuata matakwa yenu wajivuni wakubwa nyie
 
Hii inaitwa devil's advice.

Yaani mshaona hampati kitu sasa mnawaandaa watanzania kisaikolojia kwa kuvuruga amani ya nchi yetu baada ya matokeo kutangazwa.

Mtashangaa this time hatutakubali kufuata matakwa yenu wajivuni wakubwa nyie
System haitatuangusha itatenda haki. Akishindwa waachane naye. Akishinda atangazwe
 
Hii inaitwa devil's advice.

Yaani mshaona hampati kitu sasa mnawaandaa watanzania kisaikolojia kwa kuvuruga amani ya nchi yetu baada ya matokeo kutangazwa.

Mtashangaa this time hatutakubali kufuata matakwa yenu wajivuni wakubwa nyie
Mikwara mnaijua kweli ikija ktk utendaji mnakuwa kama mbwa koko mamamae ref: lisu kuendelea na kampeni,maana alivimba kutaka juendelea[emoji38][emoji38][emoji38] ila akaufyata.
 
Kwa maoni yako atashinda ila hatatangazwa sio??
Lisu wenu hawezi, hawezi. Baada ya uchaguzi mtaanza kuimba wimbo wa kuibiwa kura, na katiba mpya. Akili za kuku hizi, kweli Lisu, anafkiri ataweza. Hatashinda, na baada ya uchaguzi kesi zake zinamsubiri.
 
System ni nini?
Je ni kikundi cha siri chenye agenda ya kutawala kupitia chama wanachokitaka wao?
Nani anawateua au kuwaajiri?Au wanaajiriwa kutoka uvccm?

Asee kama nchi inatawaliwa na kikundi cha siri,wanatuamulia tutawaliwe na nani,ni masikitiko sana na maumivu yasiyo na matumaini ya kupona. Kwani,ni kama tunategemea huruma ya kikundi hicho.

Sasa itakuwaje wasipotuonea huruma?
Itakuwaje wakipewa hisa kwenye makampuni ya kuuza milipuko kama mabomu?Nani anawadhibiti hawa wanaitwa system?Itakuwaje siku hiki kikundi kikiwa cha ukabila ama udini?
 

Kwa maneno marahisi system ni watu wambea wanaopeleka Majungu kwa watawala, na kuhakikisha mtawala anatawala kwa jinsi atakavyo. Na ukienda kinyume na mtawala, wambea hao wana jukumu la kukuchomea kwake.
 
Nani anaijua system ya Ghadafi ilivyokuwa? Ya bashir, ya sadam, ya Mugabe acheni kupiga porojo hapa, dunia ikikuchoka hasa USA hata ulindwe na malaika, ikulu utaiachia tu utakeusitake.

Namshangaa huyu wa burigi anasesema amewaweza mabeberu, yamkini hawajui mabeberu anawadanganya tu wana ccm waliovimbiwa.

Narudia tena dunia ikimchoka magu hata begi la nguo zake atasahau kubeba
 
Waambie hawa wajinga wa Lumumba
 
Watu huongelea sana system lakini ukweli kama ipo itakuwa ni wale walioshika mpini hasa kwenye nchi zetu zenya uchamadola. Kumbuka Kenya walivyomliza Raila mchana kweupe na mtu akaapishwa ndani ya saa moja baada ya kutangazwa halafu mwenyekiti wa tume Kivutha mchana kweupe akasema hajui nani kashinda.
Rudi kwa Mzee Mkapa anaposema walichukua dola 100M (EPA)-na hakuna wa kuwapeleka popote hiyo ndio system kama unaiamini. Chaguzi za Zanzibar ndio kabisa kaingia Jecha halafu tukaambiwa na kuimbiwa kwamba CUF walivuruga uchaguzi hiyo ndio system. Lakini mwisho wa yote ni umma kuamua.
 

Kwahiyo unasema iwapo huu ukondoo a.k.a amani ukiendelea, hilo genge linalojiita system litaendelea kumuweka wamtakaye, lakini kiboko ya hilo genge ni nguvu ya umma?
 
Kwahiyo unasema iwapo huu ukondoo a.k.a amani ukiendelea, hilo genge linalojiita system litaendelea kumuweka wamtakaye, lakini kiboko ya hilo genge ni nguvu ya umma?
Tatizo letu kubwa ni ukondoo ambao wengi tunao ndio maana Chamadola husisitiza utumiaji wa nguvu kuleta amani amani na haki huipotezea. Tutakapo amka ndio mambo yatabadilika. Lakini uvumilivu una mwisho. Watu kama Lissu wanaweza wakawa catalyst nzuri ya kuua au kupunguza ukondoo.
 
Mashoga mnambwembwe!
 
Hao ni ma desk officer tu,kule vyumbani kuna wenyewe....Si uliona Dodoma Makonda alivyopigwa pini asipande jukwaa la wakubwa!
Makonda alipokuwa RC aliwajambisha sana hao system, wakawa wanamlinda hadi Lemutuz a.k.a Le kibamias.

Leo hii DC kama Jerry Muro au Sabaya anaweza kuwayumbisha system kwa jinsi anavyotaka. Yaani ni ujinga ujinga tu. Dawa ni Katiba mpyaaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…