macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Ndiyo maana Dar huwezi kusikia mtu kafa njaa japo ina wakazi wengi mno na hawalimi. Hili ni suala la kuku tu. Njia za kuingiza fedha kiharamu ni nyingi, na vyakula haramu ni vingi. Ukiamua kufuatilia kila aina ya chakula basi unaweza kuhama jiji.Unakuta mama mtaani anauza supu ya kuku bei poa unashangaa nyama kubwa inauzwa mia mbili, kumbe ni kibudu
Sikupingi,, nakumbuka kuna kijana alifumwa anaokota kuku maeneo ya darajani pale karibu na kituo cha jangwani cha mwendo kasi njia ya kuelekea posta kutokea magomeni mataa... Alikuwa anaokota kuku waliokufa na walikuwa wengi sana... SAsa sijui waliletwa na maji ya mtoni au walitupwa tu.... Na alivyo onwa aliacha ndoo alikimbia huyo..... Watu walijiuliza sana...... Ila wanadamu Wana roho mbaya sana.... Wanaangalia faida kubwa sio usalama wa mwengineNgoja niwasanue wananchi wenzangu
Siku hizi wilaya Bagamoyo (Mapinga, Kerege, Kiaraka), ambapo wengi wetu wafugaji wa kuku ndiyo tunafanyia ufugaji mkubwa)
Nimekuwa naona makundi ya wakina mama na vijana wamebeba ndoo alfajiri wakitokea mashambani kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi au jioni kuanzia saa 12 hadi 2 usiku.
Mwanzo nilifikiri Wanaenda kununua maziwa katika nashamba ya watu kisha wanayaleta mjini kwa ajili ya biashara
HAPANA! zile ndoo zina kuku waliokufa mabandani sasa wanaletwa mjini kwa ajili ya biashara
Ni hivi.., ukiwa mfugaji wa kuku wa nyama wengi (1000, 5000 hadi 10,000) ni kawaida sana kuingia bandani na kukuta kuku 5, 10 , 20, 30 hadi 50 wamekufa asubuhi au Jioni
Sasa utaratibu ni kwamba vijana wa kazi hawaruhusiwi kuwatupa mpaka mimi mwenye banda au meneja aje awashuhudie, awahesabu na kisha asimamie zoezi la kuwafukia kuku waliokufa
Sasa kumbe pale tunapofukia kuku waliokufa na ukiondoka tu, nyuma yake ndiyo wanaingia wale wamama wenye ndoo, wanauziwa wale kuku waliokufa Tsh 1,000 kwa kila kuku mmoja
Wanawafukua kisha wanahesabiana na kuwanunua, wale wamama wenye ndoo wanawaleta mjini kwa matumizi ya kitoweo
Wenyewe wanasema ukishaweka Kitunguu swaumu na tangawizi kujua kuku huyo alikuwa kibudu ni mpaka muuzaji akutonye la sivyo huwezi kujua
Lakini pia bei yake lazima ushtuke, kuku nusu anauzwa Tsh 3,000, kuku rangi yake nyeusi akisha kaangwa, kuku kapakwa rangi za njano au nyekundu kupoteza ishara za kuonekana ni kibudu.
Mimi au wewe huenda tumeshakula Vibudu tukifikiri ni Kuku,Tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku.
Pale Pugu mnadani kuna ng'ombe huja, wengine hufa kwa uchovu wa safari. Kuna watu hupewa kazi ya kwenda kufukia mizoga hiyo kwenye ule msitu kuelekea Kisarawe. Hawa jamaa hawatimizi jukumu lao la kufukia mizoga inakuwa ni fursa kwao kuchuna na kukatakata nyama na kuingia nazo mitaani kutafuta masoko. Watu wanakula mizoga kama hawana akili nzuri. Hii tabia ya kula mizoga nimeiona sehemu nyingi, hata sehemu za wafugaji mifugo ikifa na kutelekezwa na wafugaji waswahili huchangamkia nyama zake bila kujali huo mfugo umekufa kwa ugonjwa gani. Kuna mwingine mpika supu ya mbuzi anazuga kuweka kichwa na miguu ya mbuzi kumbe sufuriani kachemsha nyama ya mbwa, ukila unajisikia kiu balaa kumbe umekula mbwa.Ndiyo maana Dar huwezi kusikia mtu kafa njaa japo ina wakazi wengi mno na hawalimi. Hili ni suala la kuku tu. Njia za kuingiza fedha kiharamu ni nyingi, na vyakula haramu ni vingi. Ukiamua kufuatilia kila aina ya chakula basi unaweza kuhama jiji.
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji1544][emoji1550][emoji23]Humu wengi mtasema silibluku wa kisasa ila nafsi zenu zinawasuta[emoji23][emoji23] mimi nisichokula mjini ji miguu utumbo maini firigisi kutokana na dawa wanazokuziwa ila nyama hata ianze kuoza nakula. vitu vimekarangizwa vinaladha niviache haiwezekani. Alishakufa nguruwe wangu bandani doctor kuja ananiambia ni mambo ya sumu kuvu kwenye pumba mimi sikuuliza mara mbili nikapita na mapaja mbavu na mgongo nilizika vitu baadhi ila aliliwa kama kawaida. Mjini ukichagua sana unakutana na za uso
Huyu ni kuku au MpiraBaadhi ya wafugaji kuku wanawawapa vidonge vya ARVView attachment 2738137
Kuna ngombe wangu alikuwa anaumwa kaugua kama muda 2a mwezi hivi, sindano za haja. Zile dawa anazochomwa zina maelekezo.kama kula nyama iliwe baada ya siku kadhaa.Naonaga hata ng'ombe akifa anapakizwa kwenye guta wanamfunika sijui wanapeleka kuzika wapi[emoji1]
NI ngumu sana mganga kuacha uganga,kwani kipato chake huja mwake mwake!Kwa statement hii, hujaacha uganga kakangu. [emoji33][emoji33]
Huyo aliyeumwa kwa muda mrefu kidogo Afadhali kuliko yule anayejidondokea tu, ANTRAX! inaua fasta fasta, unavimba kichwa baada ya siku 2 niagie!Kuna ngombe wangu alikuwa anaumwa kaugua kama muda 2a mwezi hivi, sindano za haja. Zile dawa anazochomwa zina maelekezo.kama kula nyama iliwe baada ya siku kadhaa.
Sasa kimbunga siku amekufa, nikatafuta vijana wachimbe shimo wazike.
Aisee vijana walisema unazikaje Mboga, nikasema mimi siwezi kula ila nachoomba tulinde afya ya jamii. Wakasemq tuachie sisi hili swala. Walimchukua wakaenda kugawana huko
Ngoja niwasanue wananchi wenzangu
Siku hizi wilaya Bagamoyo (Mapinga, Kerege, Kiaraka), ambapo wengi wetu wafugaji wa kuku ndiyo tunafanyia ufugaji mkubwa)
Nimekuwa naona makundi ya wakina mama na vijana wamebeba ndoo alfajiri wakitokea mashambani kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi au jioni kuanzia saa 12 hadi 2 usiku.
Mwanzo nilifikiri Wanaenda kununua maziwa katika nashamba ya watu kisha wanayaleta mjini kwa ajili ya biashara
HAPANA! zile ndoo zina kuku waliokufa mabandani sasa wanaletwa mjini kwa ajili ya biashara
Ni hivi, ukiwa mfugaji wa kuku wa nyama wengi (1000, 5000 hadi 10,000) ni kawaida sana kuingia bandani na kukuta kuku 5, 10 , 20, 30 hadi 50 wamekufa asubuhi au Jioni.
Sasa utaratibu ni kwamba vijana wa kazi hawaruhusiwi kuwatupa mpaka mimi mwenye banda au meneja aje awashuhudie, awahesabu na kisha asimamie zoezi la kuwafukia kuku waliokufa.
Sasa kumbe pale tunapofukia kuku waliokufa na ukiondoka tu, nyuma yake ndiyo wanaingia wale wamama wenye ndoo, wanauziwa wale kuku waliokufa Tsh 1,000 kwa kila kuku mmoja.
Wanawafukua kisha wanahesabiana na kuwanunua, wale wamama wenye ndoo wanawaleta mjini kwa matumizi ya kitoweo.
Wenyewe wanasema ukishaweka Kitunguu swaumu na tangawizi kujua kuku huyo alikuwa kibudu ni mpaka muuzaji akutonye la sivyo huwezi kujua.
Lakini pia bei yake lazima ushtuke, kuku nusu anauzwa Tsh 3,000, kuku rangi yake nyeusi akisha kaangwa, kuku kapakwa rangi za njano au nyekundu kupoteza ishara za kuonekana ni kibudu.
Mimi au wewe huenda tumeshakula Vibudu tukifikiri ni Kuku, tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku.