Yamebakia kama masaa 24 kabla ya mtanange muhimu kwa Yanga na Al Hilal hapo kesho.
Niwatahadharishe kitu kuwa, kesho inaweza ikatokea bahati mbaya Yanga wakafungwa goli la mapema sana. Sasa niwaambie ndugu zangu hawa kuwa, hawatakiwi kukata tamaa mpira ni dakika 90.
Goli la mapema linaweza likawaumiza vibaya na kuwavuruga na wakatoka kabisa kwenye mchezo kwa kuwa tayari Al Hilal wana utangulizi wa goli la ugenini.
Niwakumbushe fainali moja ya mataifa Kombe la Dunia nahisi ilikuwa kama siyo robo fainali basi ni nusu fainali.
Ilikuwa ni kati ya Italia na Ujerumani na Italy. Italy walikuwa nyuma kwa magoli 2 tena walikuwa wanacheza pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kutolewa kwa kadi nyekundu enzi hizo za akina viungo hatari wenye mapafu ya kutisha kina Gatuso, Materazi, Maserano kama sikosei.
Lakini waliweza kurudi kwa kishindo na kupindua meza kwa ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya miamba Ujerumani tena magoli mengine yalifungwa kipindi cha dakika 30 za nyongeza kwani hadi mwisho wa mchezo goli zilikuwa 2-2. Kwa wenye kumbukumbu nzuri juu ya mechi hii mtasaidia.
Sasa ndugu zangu wa Yanga mpira ni dakika 90. Msivuruge mechi kwa kukataa tamaa mapema kwa goli la mapema. Pambaneni hadi mwisho kieleweke kama ni kufa basi iwe kufa kiume.
Kila heri.