Tahadhari ya utapeli mpya Dar kwa sasa

Tahadhari ya utapeli mpya Dar kwa sasa

Utapeli wa mabenki

Hapa ninachojiuliza ni kuwa .....Nina pesa nying kwenye account .....na hyo ni siri yangu...( kama kawaida wabongo kuficha siri kuhusu pesa zangu)
Je siku nikifariki ......benk inapeleka WAP ....fedha zanguuuu
Kama ulifungua account lazma utakuwa umeandika warithi wa fedha zako hivyo hao ndo wana haki ya kuzichukua fedha zako baada ya kuthibitisha kuwa umefariki
 
Mimi nina Duka la AGROVET.. nikiwa Dukani, alifika jamaa amevaa cap na barakoa akaulizia mbegu za alizeti. Baada ya kumjulisha bei aligoma kununua akidai kuwa bei aliyojulishwa ni ndogo.

Nilimshauri aende kwenye maduka mengine ajiridhishe bei, lakini alinijulisha kuwa atamsubiri aliyemuagiza maana yupo njiani kuelekea mjini. Mi niliendelea na mishe zangu kumbe jamaa alitoka nje akawa amekaa kwenye kiti kilichopo nje ya Duka.

Baada ya masaa kadhaa nilitoka nje ili nikapate chakula, nikamkuta jamaa amekaa nje.. alivyoniona akaniambia jamaa anakaribia kufika hivyo nimvumilie kidogo.

Nimerudi dukani kama dk 5 hivi nikashangaa jamaa ameingia dukani ameshika laptop mpya, akaniambia kuna jamaa anataka kumuuzia laptop anaomba aitest kwenye chaji.

Baada ya kuiweka kwenye chaji aliomba aende kutafuta flash ili aweke movie ajaribu kuitest laptop, aliondoka na baada ya dk kama 5 tena alirudi akiwa amepaniki kidogo akaiomba laptop akaitia kwenye begi akaondoka zake.

Baada ya dk 15 aliingia mshikaji mmoja akamuulizia , mi nikamjulisha kuwa yule ni mteja tu na ameondoka.. jamaa jasho likamtoka .. kumbe huyo mshikaji anauza laptop aliongea na huyo taperi akamdanganya kuwa anamiliki duka langu hivyo aletewe laptop hapo.

Baada ya kukagua laptop wakiwa nje ya duka alimwambia asubiri aiweke laptop ndani then waelekee benki akamchukulie pesa, walipofika kwa wakala wa benki jamaa akamwambia amsubiri dk 3 achukue simu amesahau dukani.. ndo hakurudi tena hadi leo.

Tuwe makini ndugu zangu.. bahati nzuri huyo jamaa alikamatwa..
 
Hata wew unaweza kuwa victim wa utapeli mda wowote. Usinambie we ni clever insuch eti huwezi kupigwa never! watu wanatumia akili mpya kilasiku omba hyo mbinu mpya wasianzie kuitumia kwako
Utapeli wowote huwa una kitu kimoja ambacho ni common: Tamaa ya kupata kitu kizuri kwa gharama ndogo. Ukiweza kudhibiti hili hata waje na mbinu gani hawakupati.
 
Yupo dada ana page insta anajiita Veethriftstore anauza vitu used. Jina lake halisi ni Victoria. Nilitaka kununua washing machine used mwezi wa 6 akadai hela kabla nikarusha, delivery akasema baada ya siku 2. Mpaka leo siku 2 hazijafika na kufatilia refund ofisini kwake nikakuta mtu mwingine naye anadai refund amekata mpaka RB.Mimi nikaambiwa mzigo wangu haujafika. Baada ya kufatilia sana kwa simu, maana ofisini hawafungui tena hata geti, nikajibiwa nisimtishe. Bado namwona yupo insta analiza watu kule...ila dawa yake inachemka
 
Huyu Dada page yake Ina vitu vizuri mno..yaani mno.. Binafsi kuna wakati nilitaka kununua kitu kwake.. nikaona mlolongo wa mambo sana.. alipost bidhaa nikamwambia naweza kuja kulipia na kuondoka nayo kabisa?Akaniambia nitume hela then bidhaa nitafata kesho yake.. nikaona kuna jambo si bure.. sikuhangaika..

Baada ya muda kupita nikaona baadhi ya page Instagram wanamlalamikia..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yupo dada ana page insta anajiita Veethriftstore anauza vitu used. Jina lake halisi ni Victoria. Nilitaka kununua washing machine used mwezi wa 6 akadai hela kabla nikarusha, delivery akasema baada ya siku 2. Mpaka leo siku 2 hazijafika na kufatilia refund ofisini kwake nikakuta mtu mwingine naye anadai refund amekata mpaka RB.Mimi nikaambiwa mzigo wangu haujafika. Baada ya kufatilia sana kwa simu, maana ofisini hawafungui tena hata geti, nikajibiwa nisimtishe. Bado namwona yupo insta analiza watu kule...ila dawa yake inachemka
Namfaham ofis zake c ziko msasani ... huyu dada yeye vitu vingi anavyopost ..huwa anatumiwa picha .mfano hata ww ukiwa na kitu chako unakiuza ukimfuata dm mkaelewana bei ,atakipost kwenye page yake then anaongeza commission yake ..then mteja akikipenda atatakiwa alipie kwanz then ndo akifuate ......huu utaratibu wake wa kulipia kwanza ndo unao mcost coz sometimes inatokea ..mmliki wa kitu ana gairi kukiuza kitu chake ..na hapo ndo matatizo yanapoanziaga
 
Ukimkamata mle "ndogo" kavukavu ngese sana huyo anadhani pesa zinapatikana kiurahisi.
 
Jamaa kajiingiza kwenye mercury huko, akikusimulia jinsi atakavyopata 500milioni unajiuliza hivi huyu anadhani pesa inakuja kirahisi hivi? Mwambie sasa unaenda kupigwa uone atavyokudharau..
Mpige mabanzi ya kumshtua
 
Ukitapeliwa tuma namba ya simu ya aliyekutapeli in kwenda 15040 BURE. Laini ya mtu huyo HUFUNGWA pia namba ya NIDA(iliyotumika kusajili laini ya utapeli) huwekwa BLACKLIST yaani inakuwa useless, mwenye hiyo NIDA hawezi kuitumia kokote kule hata kama ni benki
20210722_110443.jpg
 
Namfaham ofis zake c ziko msasani ... huyu dada yeye vitu vingi anavyopost ..huwa anatumiwa picha .mfano hata ww ukiwa na kitu chako unakiuza ukimfuata dm mkaelewana bei ,atakipost kwenye page yake then anaongeza commission yake ..then mteja akikipenda atatakiwa alipie kwanz then ndo akifuate ......huu utaratibu wake wa kulipia kwanza ndo unao mcost coz sometimes inatokea ..mmliki wa kitu ana gairi kukiuza kitu chake ..na hapo ndo matatizo yanapoanziaga
mbona mimi hakunambia hayo
Screenshot_20211211-101307_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom