TAHAJUDI (Meditation): Mbinu, faida, aina na mambo ya kuzingatia


Wacha wee...
Unaogopa nini?
 
Last edited by a moderator:



Mkuu Pasco mie ni mtu ninayependa kwenda beyond hata kusoma na kuchunguza mambo ambayo siyapractice. Inawezekana hujanielewa vizuri. Hayo unayoeleza wewe na Mtambuzi ni sahihi kwa mtazamo wa interests na imani zenu.

Concern yangu sio kama wewe uko sahihi au sio shahihi, bali ni kwamba meditation ni moja ya derivatives za practices, belief systems ambazo ni against christianity.

Ninachotaka kusema ni kuwa, kama mtu ni mkristo na anajua maana ya kuwa mkristo hatakiwa kupractice meditation kwa sababu ni kinyume na imani yake. Meditation ni ibada ya kuabudu vitu vingine na kuacha njia alizotoa Mungu wa kwenye Biblia za kufanya na kufanikisha mambo ya mwanadamu ya kila siku. Biblia imetuambia tujibidishe sana katika kutafuta maarifa, ndio maana katika kupekua kwangu nimeweza kujua meditation ni kitu gani, and simply ni paganism. Kwa namna hiyo naweza kutofautisha mabaya na mazuri, yapi ya kufuata na yapi sio.

Popote palipoandikwa kwenye Biblia neno meditation linamaanisha ""to think, conteplate, devise, ponder" sometimes to "sigh or murmur".

Wapi kwenye Biblia pameandikwa Yesu alimeditate kwa maana unayoielezea wewe?

Imani zote ambazo hazina coherence na ukristo ni paganism, kama vile waislamu wanavyoamini yeyote ambaye sio mwislamu ni kafiri.
 
Meditation (uliyoilezea wewe) ina mchanganyiko wa vitu ambavyo vingine vinaweza kukubalika kwa imani ya kikristo, mfano to calm yourself, think deeply, sit in a quite place to read a Bible or pray, kutenga muda kila siku kumeditate with the God our Father. Katika ukristo kwa kifupi meditation ni kutenga muda katika hali ya utulivu "quite time" kwa nia ya kucommunicate na Mungu kupitia maandiko, maombi au tafakari ya aina yoyote kuhusu Mungu au Neno lake. Hii ndio meditation inayoelezewa kwenye Biblia.

Lakini meditation unayoielezea Wewe na Mtambuzi inaembrace na kuborrow a lot from paganism, in that sense the whole thing ni paganism, kwa sababu Neno la Mungu halitaki mchanganyiko.

CC Pasco
 
Miaka 1980....

Ok nimempata mkuu, anasema about 1980 years ago. Kumbuka Ukristo hata kabla ya kuanza was foretell several thousands years ago. Yaani habari za ukristo ziliandikwa - soma agano la kale kabla ya ukristo wenyewe kuanza.
 
Pasco acha uongo ukristo haujaanza miaka ya 1980.
Mdukuzi, unapomuita mtu ni muongo, ni busara ukiuweka ukweli ili kuuonyesha uongo wangu.

Nijuavyo mimi ukikristu ulianza mara tuu baafa ya kufa kwa Masiya.

Yesu alizaliwa mwaka 1. Aliishi kwa miaka 33, alipokufa ndipo Ukristu ukaanza!.

Pasco
 
Angalia hapa unasema nini,

Na hapa jee, unasema nini kuhusu meditation!.
Meditation is simply concentration, mara use me ni paganism, mara useme Ukiisha ji confine ndani ya Bibilia pekee, then you think in a confinement!, humu pia ni ndani ya box tuu, unachofanya hapa ni unafurukuta tuu humo humo ndani ya box ulilomo baada ya kusikia sauti za nje ya box!.

If kwa kuwepo kwako ndani ya box, makes you happy!, then its fine be there na tulia there, a chana kabisa na sisi tulip née ya box, ila usiwatishe wenye kuhitaji ufahamu zaidi ya huo kiduchu ulionao ndani ya box ulimo!. You either come out tujadiliane objectively, or jinyamazie waache wenye kuhitaji kufanya meditation tufanye!.

Hii tabia ya "a barking dog" kila mara kubweka tuu, toka ndani ya box alimofungiwa, inakera!, kero yenyewe ni kelele tuu za kubweka usiku kucha huku anazunguka mumo humo!.

Christians fundamentalists are as dangerous as Muslim fundamentalist, mkifanya Tahajudi inaweza kuwasaidia to see beyond.
Nakutakia J2 Njema!.
Pasco
 
Kwa kweli mimi binafsi hizi habari uwa zinanichanganya sana.
 
Hebu ndugu Pasco nisaidie,ninapotaka kufanya meditation yangu nikimshilikisha Mungu muumba ni jinsi gani napaswa kufanya,Je naingia katika maombi mahala palipo na utulivu?au nafanya nini kuweza kufanya jambo kubwa katika maisha yangu nikilejea katika somo lako la nguvu za kutenda miujiza,kimsingi nataka kufanya lolote kwa kumshilikisha Mungu tu na si kwa uwezo wangu,nijenge hapo tafadhari ndugu PASCO
 
Mkuu G'taxi, hakuna lisilowezekana, ndio maana kuna mafundisho mengi na ya aina tofauti tofauti!.
Kama unataka kutumia somo langu, then fuata yangu, katika somo langu nimesema tangu mwanzo kuwa
Mungu alitupatia zile nguvu za Uuungu siku ile alipotuumba, hivyo huyu Mungu yupo ndani yetu na hizo hizo nguvu zimo ndani yetu, ni suala la kuzifungua tuu hapo zilipo na kuzitumia!.

Unapotaka kutenda lolote kwa kwa kumshirikisha Mungu tuu na sio huo uwezo wako Mungu aliokupatia, unahatari na kutumiwa na mungu, ukadhani ni Mungu!. Kwa vile dini ziko nyingi, nguvu ziko nyingi na imani ziko nyingi, wewe just do what "you" think is right, na not necessarily unachoambia is right!.

Unaweza kusikiliza yote ila shika lako!.

Pasco.
 

Wewe kwa nini hutaki kuelewa ninachosema. Nimekueleza the etymological meaning ya meditation kwa mjibu wa Biblia. Halafu mie sijasema meditation haipo or whatever, wewe kama unajua kuhusu meditation leo, mie naijua kitambo. Na nimesema kuwa kwa mkristo akiiga au kuifuata meditation mnayoipreach wewe na mtambuzi atakuwa amepotea kwa sababu ina mchanganyiko ambao haukubaliki kwa imani ya kikristo!

Tofautisha kuwa ndani ya box na kujua kitu lakini huna nia ya kukipractice au hukipendi au hukitaki kwa sababu zozote zile. Wewe akili yako inakutuma kwamba mtu anayekataa au kupinga jambo fualani ni kwamba halielewi, uko chaka.

Hebu kuwa specific na unachotaka kusema, maelezo yangu yako sahihi. Na nasema tena mtu yeyote ambaye ni mkristo kweli na anajua maana ya ukristo hatakiwi (sio kwamba namkataza kwa nguvu, bali namaanisha inapingana na anachoamini) kupractice hii ----.ing meditation mnayoihubiri isipokuwa tu ile meditation kwa mjibu wa maelezo ya Biblia.
 
Pasco unapoongelea jambo lazima uwe na uwezo wa kupembua kwa kuzama zaidi! Mfano unaweza kuja hapa ukasema sex inaruhusiwa kwa wanandoa kwa mjibu wa Biblia, lakini haitoshi kusema hivyo tu, inabidi useme sex kati ya jinsia ya kike na kiume waliooana na sex hiyo isiwe ya kugeuzana (isiwe sodoma) na hairuhusiwi kati ya watu wa jinsia moja, etc.,

Ndio maana nimesema sio the whole krap about meditation inakubalika katika imani ya kikristo. Wewe kupreach au kunadi meditation au kuipractice hakuna mtu anayekukataza. Usibishe kwamba meditation haiembarce wicca, magic, witchcraft, spell, etc., halafu ni very wide na practiced in many ways na makundi mbalimbali, ni cult. Kama nilivyosema iwapo unaamini maandiko ya watu wengine ambako kimsingi maelezo yako yanatokana na research zao. Tafuta vitabu vingi soma, usilete habari za kijujuu tu au kupinga bila kujua hivi vitu vinahusianaje.
 
Mkuu is it special kwa wanawake tu !! naona wote kwenye picha ni ke ?
 
Pasco faida za meditation mnaziorodhesha tu, leteni basi scientific substantiation. Na hasara zake ni nini?
 
Last edited by a moderator:
 
Nadhani hapa sasa tukubaliane kutokukubaliana, Mimi na Mchambuzi sio wahubiri, wala mafundisho yetu ya meditation hatujasema ni mafundisho ya dini fulani, tumetoa mafundisho kwa watu wote wa dini zote, maadam umejitabaisha wewe umejiconfine kwenye Biblia, them keep your confinment kwenye Biblia, ambayo imekuja imeikuta meditation tayari ipo, Yesu amekuja amaikuta maditation ipo, ameitumia, ameifundisha ameondoka na kuiacha meditation ipo, kama kupitia Mafundisho ya Yesu, Bibilia na Ukristu, kuna specific meditationa za Kikristu tuu, then natoa wito kwa Wakristo wote, fuateni meditation ya kwenye Bibilia, sisi wengine tuendelee na darasa la meditation ya watu wote!.

Mimi ni Mkiristu, Mkatoliki, mama yangu ni Born Again!. Sisi Wakatoliki tunaipiga pombe kama kawa, Divai hadi Altareni kwa hoja kuwa huo ndio muujiza wa kwanza wa Bwana wetu Yesu Kristo, alioufanya kwenye harusi ya Kana!. Mama yangu haamini katika pombe, akiamini kunywa pombe ni dhambi kwa mujibu wa imani yake, na kutusisitiza tuokoke tujiunge na dini za wokovu, baadhi ya wadogo zangu wameokoka na sisi wengine tumekomaa na kuendelea kusimama na Kanisa Moja, Takatifu la Mutume, ambalo ndilo pekee Bwana wetu Yesu Kristu aliliacha, hivyo kutobabaishwa na hivi vijikanisa lukuki vinavyoibuka kama uyoga na kutuhubiria Pombe ni dhambi!. Hivyo ndivyo ninavyokuona wewe na mahubiri yako humu kuwa Tahajudi ni upagani!. Endelea na unachoamini, na sisi tuache tuendelee kuwafundisha watu kujitambua hadi kufikia kiwango cha kutodanganyika na hivi vidini vya uongo uongo vyeme wahubiri wanaotumia nguvu za giza kuwapoteza watu wa Mungu!.

Please keep your way and let us keep our way na kama vipi, unaweza kuanzisha uzi wako wa "Jifunze Kufanya Tahajudi ya Kikristu" ili Wakristu wafanye Tahajudi ya kwenye Biblia!.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…