Taharuki: Mtanzania diaspora atekwa nyara Kilimanjaro

Taharuki: Mtanzania diaspora atekwa nyara Kilimanjaro

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,483
Reaction score
40,130
Anaandika Liberatus Mwang'ombe

IMG-20251228-WA0090.jpg


Mpaka uzi huu unapanda hewani, jeshi la utekaji la polisi hawajatoa kauli yeyote

UPDATE
Mdogo wake Thadei Kweka aitwaye JB Kweka, kupitia Club House amethibitisha kutekwa kwake. Ameeleza zaidi kuwa polisi wamekiri kumkamata. Tukio la kukamatwa kwake limejiri baada ya askari wasio na sare kuvunja nyumba aliyokuwepo usiku na kumchukua kwa nguvu.

JB Kweka ametaarifu zaidi kuwa, polisi walipofika naye mafichoni walimkagua na kugundua ana hati ya kusafiria ya Marekani ndipo wakampeleka kituo cha Hai, wakatoa taarifa na sasa haijulikani wamemuhamishia kituo gani.

Screenshot_20251229_100132_Clubhouse~2.jpg


Taarifa imeshatolewa Ubalozi wa Marekani Tanzania na Ikulu ya White House.

Taarifa zaidi zitawajia
 
linapotokea tatizo Kama MTU msomi anza na kuwasiliana na mamlaka husika

Tatizo halitatuliwi kwa likes na comments pekee .


N.B TUENDELEE KUMUUNGA MKONO , MAMA WA AFRICA DR SAMIA SULUHU HASSAN NA PIA KUWA WAZALENDO KATIKA TAIFA LETU🇹🇿🙏🏽
 
Nauliza tu, siku hizi mtu yeyote akikamatwa na polisi maana yake ametekwa?.
Unajua taratibu za ukamataji kisheria? Watu wanakuja kwako, wanavunja mlango, wanakubeba juju baada ya kukupiga sana,kisha wanakutupa kwenye gari na kukupeleka pasipojulikana! Huyo anakuwa amekamatwa kisheria? Mwingine walikaa naye kwa zaidi ya siku 30 huku wakikana kumshikilia,ndipo wakaja kukiri kuwa naye baada ya kelele nyingi za raia,hao watu hawana tofauto na majambazi.
 
Back
Top Bottom