Wazili si chochote ndugu usipoteze mda wako kumsikiliza mwenye nguvu ni amili jeshiHivi Waziri wa mambo ya nchi alisemaje? Mbona wakaidi hawa? Ngoja uone rungu la waziri litakavyowaangukia
Wazili si chochote ndugu usipoteze mda wako kumsikiliza mwenye nguvu ni amili jeshiHivi Waziri wa mambo ya nchi alisemaje? Mbona wakaidi hawa? Ngoja uone rungu la waziri litakavyowaangukia
Kibaraka Wakili wa Polepole hajatoa taarifa kwa mamlaka husika?linapotokea tatizo Kama MTU msomi anza na kuwasiliana na mamlaka husika
Tatizo halitatuliwi kwa likes na comments pekee .
N.B TUENDELEE KUMUUNGA MKONO , MAMA WA AFRICA DR SAMIA SULUHU HASSAN NA PIA KUWA WAZALENDO KATIKA TAIFA LETU🇹🇿🙏🏽
Mpaka watu wapige keleleJeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kumkamata na kumshikilia Thadey Sabinus Kweka kwa tuhuma za makosa ya jinai ikiwemo uchochezi, likieleza kuwa hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi iliyotolewa siku ya Jumatatu Desemba 29, 2025 na Msemaji wa Jeshi hilo, Makao Makuu ya Polisi Dodoma, DCP David Misime, mtuhumiwa huyo alikamatwa usiku wa Desemba 28, 2025, mkoani Kilimanjaro, na kwa sasa anashikiliwa kwa ajili ya kuendelea na taratibu za kisheria.
“Taratibu za kukamilisha ushahidi ikiwa ni pamoja na kupata maelezo yake juu ya tuhuma hizo unaendelea ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata”, imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa ya Polisi imekuja saa chache baada ya kusambaa kwa madai katika mitandao ya kijamii yakidai kuwa Thadey Kweka, Mtanzania anayeishi nchini Marekani na akitajwa kama mwanaharakati wa demokrasia na haki za binadamu, alikuwa ametekwa nyumbani kwake Moshi na watu waliodaiwa kuwa na silaha.
Imeelezwa kuwa Thadey Kweka aliwasili nchini Tanzania wiki iliyopita kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka, pamoja na kuhudhuria harusi ya ndugu yake mkoani Kilimanjaro.
Jeshi la Polisi halijatoa maelezo ya kina juu ya mazingira ya kukamatwa kwake zaidi ya kueleza kuwa alikamatwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria, huku likisisitiza kuwa uchunguzi unaendelea ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.
Hahaha Mimi nitekwe kwa sababu zipi ?
Kama alihamsisha maandamano sawa na Liberatus Mwang'ombe muache apate kinachomstahili. Mali za watu na za Serikali zimeteketea na watu wameuliwa kwa aajili ya ujinga wao.Anaandika Liberatus Mwang'ombe
View attachment 3522077
Mpaka uzi huu unapanda hewani, jeshi la utekaji la polisi hawajatoa kauli yeyote
Kuhamasisha maandamano ni kosa kwa sheria ipi?Kama alihamsisha maandamano sawa na Liberatus Mwang'ombe muache apate kinachomstahili. Mali za watu na za Serikali zimeteketea na watu wameuliwa kwa aajili ya ujinga wao.
Mpaka watu wapige kelele
Ipo siku kibaka atakwapua simu..Police makao makuu watatoa taarifa kwa jamii.Polisi hawawezi kutoa matangaza ya kila mtu anayekanatwa. Huyu ilibidi watoe tangazo kwa sababu kuna watu wenye nia ovu walikuwa wanasambaza taarifa za kichochezi kuwa ametekwa.
Mimi nataka wamteke mpaka balozi wa Marekani nchini Tanganyika ili wakipate kile wanachokitafuta.Anaandika Liberatus Mwang'ombe
View attachment 3522077
Mpaka uzi huu unapanda hewani, jeshi la utekaji la polisi hawajatoa kauli yeyote
UPDATE
Mdogo wake Thadei Kweka aitwaye JB Kweka, kupitia Club House amethibitisha kutekwa kwake. Ameeleza zaidi kuwa polisi wamekiri kumkamata. Tukio la kukamatwa kwake limejiri baada ya askari wasio na sare kuvunja nyumba aliyokuwepo usiku na kumchukua kwa nguvu.
JB Kweka ametaarifu zaidi kuwa, polisi walipofika naye mafichoni walimkagua na kugundua ana hati ya kusafiria ya Marekani ndipo wakampeleka kituo cha Hai, wakatoa taarifa na sasa haijulikani wamemuhamishia kituo gani.
View attachment 3522136
Taarifa imeshatolewa Ubalozi wa Marekani Tanzania na Ikulu ya White House.
Taarifa zaidi zitawajia
Uwe na akili kidogo.Nauliza tu, siku hizi mtu yeyote akikamatwa na polisi maana yake ametekwa?.