Pamoja na hiyo lengo lao la kutuma ujumbe kwa wahusika limemitia maana Diwani, mhandisi na viongozi wengine walitoka ofisini na kukimbilia huko fasta. Kingine kwa kuwa picha imesambaa mpaka kwa wakubwa ni wazi kwamba hata kama haitowekwa lami itawekwa walau maram na matengenezo mengine maana viongozi wetu huku mikoani na wilayani wataogopa kutumbuliwa.