Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wiki iliyopita siku ya Jumamosi, Watoto waliporudi nyumbani walileta taarifa ya kushtua kuwa Shule ya Msingi Ubungo National Housing (NHC) inauzwa, na wazazi tunahitajika kufika shuleni leo Jumanne kwa ajili ya kikao kilichopangwa. Hali hii ilisababisha taharuki miongoni mwa wazazi. Tulipofika shuleni leo, tumeambiwa kuwa shule inavunjwa na badala yake itabadilishwa kuwa English Medium.
Hata hivyo, tulipokea taarifa hii bila barua rasmi kutoka shuleni, tena watoto ndio waliotufahamisha kuhusu mabadiliko haya. Tumefika shuleni hapa, lakini tumeambiwa Mkuu wa Shule anaumwa na hayupo, Mkuu Msaidizi anasema yupo kwenye kazi maalum, na hata Afisa Elimu na Mratibu hawapo. Hatujui hatma ya watoto wetu.
Baada ya kufika hapa leo, tumeelezwa kuchagua shule nyingine kwa ajili ya kuwatoa watoto wetu, lakini hakuna maelezo ya kutosha kuhusu kwanini shule ya Serikali inavunjwa au kwanini taarifa hii inatolewa kwa dharura. Wengine wanalazimishwa kusaini makubaliano ya kuhamisha watoto bila kujua vema maelezo ya mabadiliko haya ya ghafla.
Hii ni hali ya kusikitisha kwa wazazi na inahitaji uwazi zaidi kutoka kwa viongozi wa elimu na serikali kuhusu mustakabali wa watoto wetu kwani hivi sasa unawahamishaje watoto mwishoni mwa mwaka?
Pia soma ~ RC Chalamila: Shule ya Ubungo NHC haiuzwi, inaboreshwa
Pia soma ~ RC Chalamila: Shule ya Ubungo NHC haiuzwi, inaboreshwa