DOKEZO Taharuki yazuka, Wazazi wajaa Shule ya Msingi Ubungo NHC baada ya taarifa kuwa shule inauzwa

DOKEZO Taharuki yazuka, Wazazi wajaa Shule ya Msingi Ubungo NHC baada ya taarifa kuwa shule inauzwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wiki iliyopita siku ya Jumamosi, Watoto waliporudi nyumbani walileta taarifa ya kushtua kuwa Shule ya Msingi Ubungo National Housing (NHC) inauzwa, na wazazi tunahitajika kufika shuleni leo Jumanne kwa ajili ya kikao kilichopangwa. Hali hii ilisababisha taharuki miongoni mwa wazazi. Tulipofika shuleni leo, tumeambiwa kuwa shule inavunjwa na badala yake itabadilishwa kuwa English Medium.
Hata hivyo, tulipokea taarifa hii bila barua rasmi kutoka shuleni, tena watoto ndio waliotufahamisha kuhusu mabadiliko haya. Tumefika shuleni hapa, lakini tumeambiwa Mkuu wa Shule anaumwa na hayupo, Mkuu Msaidizi anasema yupo kwenye kazi maalum, na hata Afisa Elimu na Mratibu hawapo. Hatujui hatma ya watoto wetu.
1731402677641.png
Baada ya kufika hapa leo, tumeelezwa kuchagua shule nyingine kwa ajili ya kuwatoa watoto wetu, lakini hakuna maelezo ya kutosha kuhusu kwanini shule ya Serikali inavunjwa au kwanini taarifa hii inatolewa kwa dharura. Wengine wanalazimishwa kusaini makubaliano ya kuhamisha watoto bila kujua vema maelezo ya mabadiliko haya ya ghafla.
1731402707733.png
Hii ni hali ya kusikitisha kwa wazazi na inahitaji uwazi zaidi kutoka kwa viongozi wa elimu na serikali kuhusu mustakabali wa watoto wetu kwani hivi sasa unawahamishaje watoto mwishoni mwa mwaka?


Pia soma ~ RC Chalamila: Shule ya Ubungo NHC haiuzwi, inaboreshwa
 

Attachments

  • video_2024-11-13_08-38-46.mp4
    38.6 MB
Wiki iliyopita, watoto waliporudi nyumbani walileta taarifa ya kushtua kuwa Shule ya Msingi Ubungo National Housing (NHC) inauzwa, na wazazi tunahitajika kufika shuleni leo Jumanne kwa ajili ya kikao kilichopangwa. Hali hii ilisababisha taharuki miongoni mwa wazazi. Tulipofika shuleni leo, tumeambiwa kuwa shule inavunjwa na badala yake itabadilishwa kuwa English Medium.
Tumsikilize upya yule sheikh aliyesema "...pale juu hapako sawa"
 
 
Peleka mtoto hapo Mugabe acha kelele ambazo hazisaidii,Serikali imeamua kubadili shule iwe ya kiingereza huoni ni maendeleo hayo?Kwa maana nyingine mdogo wake na huyo utampeleka hapo asome kwa kiingreza.
Kuhamisha mtoto sio ishu mkuu, wanatoaje taarifa kama ni jambo la dharula? kwani wangetujulisha mapema kungekuwa na shida gani ili tufanye mchakato kwa utaratibu unaofaa
 
Kwan NHC ambae ndo mmiliki anasemaje unaenda kumuhoji mwalimu mkuu wakat mkurugenzi wa NHC yuko si wakahoji na kutafta majibu uko
NHC ni wafanyabiashara na wameona biashara ya shule za kisasa inalipa wameamua kuhamia uko medium school
 
Back
Top Bottom