Wiki iliyopita siku ya Jumamosi, Watoto waliporudi nyumbani walileta taarifa ya kushtua kuwa Shule ya Msingi Ubungo National Housing (NHC) inauzwa, na wazazi tunahitajika kufika shuleni leo Jumanne kwa ajili ya kikao kilichopangwa. Hali hii ilisababisha taharuki miongoni mwa wazazi. Tulipofika shuleni leo, tumeambiwa kuwa shule inavunjwa na badala yake itabadilishwa kuwa English Medium.
Your browser is not able to display this video.
Hata hivyo, tulipokea taarifa hii bila barua rasmi kutoka shuleni, tena watoto ndio waliotufahamisha kuhusu mabadiliko haya. Tumefika shuleni hapa, lakini tumeambiwa Mkuu wa Shule anaumwa na hayupo, Mkuu Msaidizi anasema yupo kwenye kazi maalum, na hata Afisa Elimu na Mratibu hawapo. Hatujui hatma ya watoto wetu.
Baada ya kufika hapa leo, tumeelezwa kuchagua shule nyingine kwa ajili ya kuwatoa watoto wetu, lakini hakuna maelezo ya kutosha kuhusu kwanini shule ya Serikali inavunjwa au kwanini taarifa hii inatolewa kwa dharura. Wengine wanalazimishwa kusaini makubaliano ya kuhamisha watoto bila kujua vema maelezo ya mabadiliko haya ya ghafla.
Hii ni hali ya kusikitisha kwa wazazi na inahitaji uwazi zaidi kutoka kwa viongozi wa elimu na serikali kuhusu mustakabali wa watoto wetu kwani hivi sasa unawahamishaje watoto mwishoni mwa mwaka?
Wiki iliyopita, watoto waliporudi nyumbani walileta taarifa ya kushtua kuwa Shule ya Msingi Ubungo National Housing (NHC) inauzwa, na wazazi tunahitajika kufika shuleni leo Jumanne kwa ajili ya kikao kilichopangwa. Hali hii ilisababisha taharuki miongoni mwa wazazi. Tulipofika shuleni leo, tumeambiwa kuwa shule inavunjwa na badala yake itabadilishwa kuwa English Medium.
Peleka mtoto hapo Mugabe acha kelele ambazo hazisaidii,Serikali imeamua kubadili shule iwe ya kiingereza huoni ni maendeleo hayo?Kwa maana nyingine mdogo wake na huyo utampeleka hapo asome kwa kiingreza.
IBILISI RUDISHA FAHAMU ZETU(MIMI NA MKE WANGU). BY ISSAI SINGANO . (Singano jr). DIBAJI Saa saba mchana Frida alionekana akiingiza gari ndani ya hospitali na taasisi ya kitafiti ya Neuroscience inayopatikana Kibaha , kilomita kadhaa kutoka ilipo hospitali ya Tumbi. Ilikuwa ni hospitali kubwa...
Hizo ndio sera nzuri za ubinafsishaji. Vitu kama hivi ndio vinagusa raia vizuri wanaelewa haswa nini kinafuata. Maana wakiambiwa wapiganie haki zao hawaelewi. Safi sana.
Kazi iendelee.
Peleka mtoto hapo Mugabe acha kelele ambazo hazisaidii,Serikali imeamua kubadili shule iwe ya kiingereza huoni ni maendeleo hayo?Kwa maana nyingine mdogo wake na huyo utampeleka hapo asome kwa kiingreza.
Peleka mtoto hapo Mugabe acha kelele ambazo hazisaidii,Serikali imeamua kubadili shule iwe ya kiingereza huoni ni maendeleo hayo?Kwa maana nyingine mdogo wake na huyo utampeleka hapo asome kwa kiingreza.
Kuhamisha mtoto sio ishu mkuu, wanatoaje taarifa kama ni jambo la dharula? kwani wangetujulisha mapema kungekuwa na shida gani ili tufanye mchakato kwa utaratibu unaofaa
Kwan NHC ambae ndo mmiliki anasemaje unaenda kumuhoji mwalimu mkuu wakat mkurugenzi wa NHC yuko si wakahoji na kutafta majibu uko
NHC ni wafanyabiashara na wameona biashara ya shule za kisasa inalipa wameamua kuhamia uko medium school