TAHURI: Tumuunge mkono Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona

TAHURI: Tumuunge mkono Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona

KWani wewe una tatizo la corona au unalisikia redioni na TV , sasa unataka dawa? Wafie mbali huko!

In 1996, an outbreak of measles, cholera, and bacterial meningitis occurred in Nigeria. Pfizer representatives and personnel from a contract research organization (CRO) traveled to Kano to set up a clinical trial and administer an experimental antibiotic, trovafloxacin, to approximately 200 children. Local Kano officials reported that more than 50 children died in the experiment, while many others developed mental and physical deformities. The nature and frequency of both fatalities and other adverse outcomes were similar to those historically found among pediatric patients treated for meningitis in sub-Saharan Africa.[173] In 2001, families of the children, as well as the governments of Kano and Nigeria, filed lawsuits regarding the treatment. According to the news program Democracy Now!, "[r]esearchers did not obtain signed consent forms, and medical personnel said Pfizer did not tell parents their children were getting the experimental drug." The lawsuits also accuse Pfizer of using the outbreak to perform unapproved human testing, as well as allegedly under-dosing a control group being treated with traditional antibiotics in order to skew the results of the trial in favor of Trovan. While the specific facts of the case remain in dispute, both Nigerian medical personnel and at least one Pfizer physician have stated that the trial was conducted without regulatory approval.

Source: Pfizer - Wikipedia
Mimi tatizo langu siyo korona, ni argument ambayo haitoi mbadala. All human knowledge is approximate. Mambo mengi ni trial and err - kwa sababu binadamu hana absolute knowledge. Kwa maana hiyo, kuna error zinatokea, lakini hiyo haina maana kwamba all human endevours are useless because of possible errors.
 
Eti wangeleta TIBA badala ya chanjo msipende kudiscus mambo ya kitaalam ki siasa zaidi VIRUS vinakufa kwa dawa gani.?
Kama bwana wao anadhani kila gonjwa linaweza kuwa na chanjo unadhani wao akili zao zitakuwa tofauti? Kwangu mimi ukiniambia Magufuli alifika kidato cha sita nitakataa katu katu. Kuna namna iliyofanyika. Upeo wa form six hauwezi kuwa mdogo namna hiyo.
 
Yani toka korona imeanza hakuna utafiti wowote wa kitaalamu tumefanya na kutoka na majibu hadharani hata kuthibitisha tu kama huu ugonjwa watu wanaugua ama la. Cha ajabu tunaendeshwa na hisia na mawazo ya watu wasio na elimu ya afya kukataa chanjo ya ugonjwa. Tutoke basi na utafiti wa kitaalamu tuiambie dunia kwamba corona sisi hatuugui au tuwaambie tuna dawa yetu badala ya kutoa vijituhuma visivyo na ushahidi wowote. Kuongoza wajinga wengi raha sana jamani
Utafiti kutoka afrika tena Tz usikilizwe na dunia nzima?
 
Mimi niko na Mh. Rais wangu Magu hadi mwisho, na nina hoja kubwa sana na sababu nyingi za kisayansi kwanini napinga chanjo, labda watupe bure, hii ni biashara ya kuibiana na kutufanya tuwe maskini wa akili na mali. Mabeberu ni watu wa kuwa nao makini sana
 
Huyo ngeti hili jina sii geni sana kipindi ha nyuma sikumbuli alifanyaga nini ila alivumaga sana
Huyu alikuwa mtu sana wa JK na baadaye Membe. Amewahi kuwa mkosoaji mkubwa wa JPM kiasi cha kuswekwa ndani then gerezani Keko. Aliyemwokoa ni Lissu. Siamini amekuwaje leo amuunge mkono Jiwe. Mwenye picha yake ailete humu.
 
Ni yeye hata wakati anaongea sisi pale Serena sikuamini macho yangu kumuona. Nimeanza kuamini jamaa ni "kitengo".
Penguin talking rubbish! Waelewa wameelewa. Ukiona hujaelewa haikuhusu au ni level juu ya uelewa wako. Asiyejua maana haambiwi maana!
Huyu Bollen Ngetti ni yule aliyekuwa akitekwa uchao? Kama kuna wakunijibu, tafadhali fanya hivyo. Au yeye mwenyewe kwa ufupi atukumbushe madhila yake ya kutekwa na yameishaje kama yameisha. Kama ni yeye alikuwa anatekwa naona kazoea hiyo hali. Leo kajiteka!
 
He/she is the one.
 
upande wa baba yangu watu watatu walipata mwangwi wa covid19 kazini, mimi binafsi ni muhanga wa covid19 mwaka 2019 kazini wakati inapamba moto. mwaka 2017 kwa bahati mbaya nilisahau kadi yangu ya manjano NRB, nimefika Horohoro ili nivuke kwenda Tanga KE wakanizuia kuvuka boda ikabidi nichome tena kwa 1000Ksh kwa sababu hawakuamini kama nimechoma.
Dunia ina mizizi yake, kikubwa ili kuibomoa lazima uwe umejipanga, ndugu zetu wanataka kwenda India, je wataenda bila idhini ya WHO/et al? wakati serikali ikipambana na the so called mabeberu wajue pia hatuko kisiwani tunategemea namna ya kuishi kutoka kwa wenzetu japo uwezekano wa 60% ya watanzania wasiwe na direct interest ya uhamiaji etc lakini haifanyi tuache kuchangamana na dunia
 
Ni takriban miaka miwili jina la Cyprian Musiba limesikika sana kwenye vyombo vya habari akiwa ni wakili wa Rais Magufuli akimtetea kwa kila jambo huku akiwatukana wakosoaji wa Rais.

Kazi hiyo Musiba ameifanya kwa muda mrefu kupitia magazeti aliyopewa na "kitengo" yakichapishwa Malindi Printers ambayo ni kampuni ya TISS ya uchapaji.

Taarifa zilizopo ni kwamba kwa sasa kazi hiyo ya kumsifu na kuabudu amepewa Mwandishi Bollen Ngetti ambaye amejitokeza hadharani kumuunga mkono Rais Magufuli na msimamo wake kuhusu Chanjo kupitia taasisi ya Tanzania Human Rights-Foundation, (TAHURI).

Chanzo changu kimedokeza, "ndugu yangu sasa ni zamu ya Bollen Ngetti, kijana msomi na mweledi lakini amekubali kutumika, inauma sana. Ngetti aliaminika sana na wapenda demokrasia japo pia inadaiwa ni wa kitengo. Kifupi tumempoteza kijana huyu ambaye huwezi kujua anakoishi jijini Dar'.

Kwa sasa Musiba amesitishiwa huduma zote za hifadhi naona toleo jipya ni Bollen Ngetti. Walio karibu naye wamwondoe huko mapema atetee wanyonge.
 
Le mutuz yupo kwa waganga wa kienyeji anampiga Ndumba kali ashindwe kumfunika cyprian Musiba
 
Taasisi ya Haki za Binadamu, Tanzania Human Rights-Foundation (TAHURI) imetoa tamko la kuwataka Watanzania kuungana pamoja katika vita dhidi ya Shirika la Afya Duniani, WHO na Rais Magufuli huku likiwataka wananchi kumuunga mkono Rais wao.

Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Bollen Ngetti amesema;

"Tunaweza kutofautiana katika mambo mengi ya kiitikadi, kimtazamo na maono lakini katika mambo ya msingi kwa nchi kama hili la chanjo ni sharti tuungane kuwa kitu kimoja".

Aidha, Ngetti ambaye ni mwandishi wa habari nchini amesema Watanzania wasikimbilie tu athari za kiafya kwa chanjo hiyo na badala yake waangalie athari za kiuchumi.

"Tutambue kuwa dunia iko katika vitu kubwa ya kiuchumi. Kama Tahuri hatutajikita sana katika athari za kiafya za chanjo hiyo lakini tufikirie ni fedha kiasi gani chanjo hiyo itaswaga?"

"Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa WHO ili nchi za ki-Afrika kupata chanjo kutoka makampuni yaliyojiorodhesha kwenye mkataba wa COVAX ambayo ni BioNTech na Moderna itazigharimu kiasi cha Dola za Marekani kati ya 7-11 kwa chanjo moja".

Ngetti ameendelea kusema, "kwa Tanzania pekee kama Rais Magufuli ataruhusu chanjo itatugharimu Tsh104Trilioni kwa idadi ya watu wetu nchi nzima. Hii ni fedha nyingi sana kwa nchi changa kama sisi".

Ngetti amefafanua kuwa fedha hizo zitatakiwa kukopwa kutoka Benki ya Dunia kwa udhamini wa ADB na itachukua miaka zaidi ya kumi kuzirejesha kwa riba ya asilimia 7.2.

Aidha, Ngetti amehoji, "kama nia njema kwa nini wazungu wamekimbilia kutafuta chanjo badala ya tiba kamili? Walijua kwa tiba utahitaji dozi chache sawa na idadi ya walioambukizwa ambao kwa sasa ni milioni 100 lakini kinga utacheza namba ya watu duniani".

"Jambo la pekee kama Taifa tunalotakiwa kufanya ni kufuata masharti ya kujikinga huku tulifanya kazi kwa bidii, huu ni upepo unaovuma na kupita, tusiondoshwe kwenye reli".

Ngetti amemaliza kwa kusema, "Magufuli si kichaa, wala hana historia ya ukichaa, anatutakia mema tusimvunje moyo. Lakini pia wataalamu wetu nao wakeshe maabara kukuna vichwa aidha kuchunguza chanjo hizo au kugundua za kwetu kama Waganda wanavyofanya"
 
kwa hiyo content ya mwandishi pesa ya chanjo ni ndefu sana lakini atambue pesa inatafutwa lakini uhai huwezi utafuta
huyo mwandish anajipendekeza kwa mkuu
 
Hapo ndipo mtaona umuhimu wa kuweka budget kwenye mambo ya maana na sio kuspend pesa kwenye vitu ambavyo ulazima ni 50 percent haya yasingetukuta.
Afya pamoja na ulinzi.

Kama tungekuwa na chanjo yetu wenyewe yenye viwango na high quality tanzania then tunaisambaza africa nzima basi tungekuwa powerful in africa in 3 month.
 
Sasa eti anataka TIBA na siyo chanjo. Anampangia nani sasa. Hiyo tiba si utafute mwenyewe? Mbona chanjo ya polio na Ndui tulichanjo? Hospitalini chanjo zipo kibao hasa kwa watoto na mama wajawazito. Mbona hawajazikataa? Kupingana na utaalamu kwa kauli za kisiasa ni ujinga. Halafu wewe kama hutaki chanjo kwa nini umkataze na mwingine? Labda wewe binafsi unataka kufa na mwingine anataka kuishi asomeshe watoto wake halafu unaanza kumkatalia alinywe dawa. Tatizo lako ni nini?

Mimi nikichanjwa wewe inakuhusu nini?
Kinachonishangaza ni kwa nini kwenye utawala huu tuu ionekane tupo makini na hii chanjo? ETI tupo kwenye vita vya uchumi na mabeberu( USA) hii kauli mi huwa inanitafakarisha sana yaani TZ imefika point tumepaa ghafla mpaka competitor wetu ni USA.Hivi wazungu unataka kuniambia wameshindwa kutuua muda wote huo leo waje kutuua kwenye chanjo ya corona.
HAPA NINACHOONA KUNA NAMNA ambayo tunalithishwa ugomvi ambao hautuhusu.
 
Taasisi ya Haki za Binadamu, Tanzania Human Rights-Foundation (TAHURI) imetoa tamko la kuwataka Watanzania kuungana pamoja katika vita dhidi ya Shirika la Afya Duniani, WHO na Rais Magufuli huku likiwataka wananchi kumuunga mkono Rais wao.

Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Bollen Ngetti amesema;

"Tunaweza kutofautiana katika mambo mengi ya kiitikadi, kimtazamo na maono lakini katika mambo ya msingi kwa nchi kama hili la chanjo ni sharti tuungane kuwa kitu kimoja".

Aidha, Ngetti ambaye ni mwandishi wa habari nchini amesema Watanzania wasikimbilie tu athari za kiafya kwa chanjo hiyo na badala yake waangalie athari za kiuchumi.

"Tutambue kuwa dunia iko katika vitu kubwa ya kiuchumi. Kama Tahuri hatutajikita sana katika athari za kiafya za chanjo hiyo lakini tufikirie ni fedha kiasi gani chanjo hiyo itaswaga?"

"Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa WHO ili nchi za ki-Afrika kupata chanjo kutoka makampuni yaliyojiorodhesha kwenye mkataba wa COVAX ambayo ni BioNTech na Moderna itazigharimu kiasi cha Dola za Marekani kati ya 7-11 kwa chanjo moja".

Ngetti ameendelea kusema, "kwa Tanzania pekee kama Rais Magufuli ataruhusu chanjo itatugharimu Tsh104Trilioni kwa idadi ya watu wetu nchi nzima. Hii ni fedha nyingi sana kwa nchi changa kama sisi".

Ngetti amefafanua kuwa fedha hizo zitatakiwa kukopwa kutoka Benki ya Dunia kwa udhamini wa ADB na itachukua miaka zaidi ya kumi kuzirejesha kwa riba ya asilimia 7.2.

Aidha, Ngetti amehoji, "kama nia njema kwa nini wazungu wamekimbilia kutafuta chanjo badala ya tiba kamili? Walijua kwa tiba utahitaji dozi chache sawa na idadi ya walioambukizwa ambao kwa sasa ni milioni 100 lakini kinga utacheza namba ya watu duniani".

"Jambo la pekee kama Taifa tunalotakiwa kufanya ni kufuata masharti ya kujikinga huku tulifanya kazi kwa bidii, huu ni upepo unaovuma na kupita, tusiondoshwe kwenye reli".

Ngetti amemaliza kwa kusema, "Magufuli si kichaa, wala hana historia ya ukichaa, anatutakia mema tusimvunje moyo. Lakini pia wataalamu wetu nao wakeshe maabara kukuna vichwa aidha kuchunguza chanjo hizo au kugundua za kwetu kama Waganda wanavyofanya"

My Take: Kwa vita hii tutashuhudia na kusikia mengi. Vita hii ya Magu na wanasayansi itaibua makubwa. Subiri tuone!
Ngeti kaamua kusaka uteuzi kishamba kwa njia haramu za kishetani
 
Kinachonishangaza ni kwa nini kwenye utawala huu tuu ionekane tupo makini na hii chanjo? ETI tupo kwenye vita vya uchumi na mabeberu( USA) hii kauli mi huwa inanitafakarisha sana yaani TZ imefika point tumepaa ghafla mpaka competitor wetu ni USA.Hivi wazungu unataka kuniambia wameshindwa kutuua muda wote huo leo waje kutuua kwenye chanjo ya corona.
HAPA NINACHOONA KUNA NAMNA ambayo tunalithishwa ugomvi ambao hautuhusu.
Hakuna vita ya kiuchumi bali CCM imetumia kama kauli mbiu kuwaduwaza watanzania wakati wao wakila keki ya Taifa kiulaini mpaka watanzania waje kushituka imefika 2025 wanaondoka zao huku watanzania wakibakia kutaabika kwa kutengwa na Duniani
 
Back
Top Bottom