TAHURI: Tumuunge mkono Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona

TAHURI: Tumuunge mkono Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona

Hyo chanjo wangetumia wao kwanza WAPONE.
kwani lazma tupeana hizo chanjo si watuache TUFE.
Kwanini tunalazimishana hizo chanjo kuna SIRI GANI?.
mpe anayetaka asiyetaka ACHANA NAE
shida ipo wapi
Shida ipo mkuu kwao,wanataka ku recover uchumi wao kwa nguvu zote .shida vaccine yao ni ghali na pia inawalakini .imagine vaccine ya HIV,cancer,na Magonjwa mengine wameshindwa kuzipata kwa miongo kadhaa now.Ila hii covid ya mwaka mmoja tu vaccine ishapatikana .Na pia iko tofauti baadhi ya maeneo Kama US,Canada na Europe hazitumiki.sisi wajinga lakini hatuwezi kuwa wajinga muda wote never,acha tufe tu
 
Taasisi ya Haki za Binadamu, Tanzania Human Rights-Foundation (TAHURI) imetoa tamko la kuwataka Watanzania kuungana pamoja katika vita dhidi ya Shirika la Afya Duniani, WHO na Rais Magufuli huku likiwataka wananchi kumuunga mkono Rais wao.

Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Bollen Ngetti amesema;

"Tunaweza kutofautiana katika mambo mengi ya kiitikadi, kimtazamo na maono lakini katika mambo ya msingi kwa nchi kama hili la chanjo ni sharti tuungane kuwa kitu kimoja".

Aidha, Ngetti ambaye ni mwandishi wa habari nchini amesema Watanzania wasikimbilie tu athari za kiafya kwa chanjo hiyo na badala yake waangalie athari za kiuchumi.

"Tutambue kuwa dunia iko katika vitu kubwa ya kiuchumi. Kama Tahuri hatutajikita sana katika athari za kiafya za chanjo hiyo lakini tufikirie ni fedha kiasi gani chanjo hiyo itaswaga?"

"Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa WHO ili nchi za ki-Afrika kupata chanjo kutoka makampuni yaliyojiorodhesha kwenye mkataba wa COVAX ambayo ni BioNTech na Moderna itazigharimu kiasi cha Dola za Marekani kati ya 7-11 kwa chanjo moja".

Ngetti ameendelea kusema, "kwa Tanzania pekee kama Rais Magufuli ataruhusu chanjo itatugharimu Tsh104Trilioni kwa idadi ya watu wetu nchi nzima. Hii ni fedha nyingi sana kwa nchi changa kama sisi".

Ngetti amefafanua kuwa fedha hizo zitatakiwa kukopwa kutoka Benki ya Dunia kwa udhamini wa ADB na itachukua miaka zaidi ya kumi kuzirejesha kwa riba ya asilimia 7.2.

Aidha, Ngetti amehoji, "kama nia njema kwa nini wazungu wamekimbilia kutafuta chanjo badala ya tiba kamili? Walijua kwa tiba utahitaji dozi chache sawa na idadi ya walioambukizwa ambao kwa sasa ni milioni 100 lakini kinga utacheza namba ya watu duniani".

"Jambo la pekee kama Taifa tunalotakiwa kufanya ni kufuata masharti ya kujikinga huku tulifanya kazi kwa bidii, huu ni upepo unaovuma na kupita, tusiondoshwe kwenye reli".

Ngetti amemaliza kwa kusema, "Magufuli si kichaa, wala hana historia ya ukichaa, anatutakia mema tusimvunje moyo. Lakini pia wataalamu wetu nao wakeshe maabara kukuna vichwa aidha kuchunguza chanjo hizo au kugundua za kwetu kama Waganda wanavyofanya"

My Take: Kwa vita hii tutashuhudia na kusikia mengi. Vita hii ya Magu na wanasayansi itaibua makubwa. Subiri tuone!

Nilikuwa najiuliza nini kimemkumba Bollen Ngetti? Kumbe yupo huku? Aisee Adui Muombee Njaa.
 
Eti wangeleta TIBA badala ya chanjo msipende kudiscus mambo ya kitaalam ki siasa zaidi VIRUS vinakufa kwa dawa gani.?

Wanakufa kwa Tangawizi, karafuu, Camphor, Kitunguu saumu nk.
 
Ngetti njoo utueleze ukweli ukoje.
Magufuli aliongelea ubaya wa chanjo na kwamba zina athari kwa kwa binadamu. Akasema Wazungu hawana nia njema na kama wangekuwa na nia njema wangeshaleta chanjo ya TB, Malaria, Kipindupindu na Kansa. Akasisitiza kwa kuna nchi wasichana wake wa miaka 14 walipewa chanjo ya kansa ya kizazi mpaka Leo ni Wagumba.
Hakuna mahali popote alipoongelea gharama za chanjo ya Covid19 kuwa kubwa. Wewe haya ya trillion 11 kuwa sababu ya nchi kukataa chanjo umeyatoa wapi? Mbona mpaka sasa mnalipisha wagonjwa wa Corona zaidi ya mil.10 kwenye hospitali binafsi na hamuwakemei wamiliki? Unajua gharama ya chanjo hizo mpaka kukamilika ni kiasi gani?
Unaposema tiba ni rahisi kuliko chanjo unatumia kigezo gani? Unapokinga watu uanazuia watu kuugua, hivyo hakutakuwa na gharama za tiba. Chanjo ya Ndui inatolewa mara moja kwa kila Mtanzania mara tu azaliwapo, Je ingekuwa gharama kiasi gani kumtibu Mtanzania mmoja anayeugua Ndui hata mara 10 tu maisha yake yote? Na tungekuwa na uhakika kiasi gani kama tiba inaokoa maisha kwa 100%? Malaria ina tiba na Watanzania wanakufa na tiba ipo, itakuwaje kwa Corona ambayo Leo mnaomba tiba badala ya Chanjo kwa kisingizio cha gharama?
Linapokuja suala la kununua ndege za Masifa mnasema tutanunua kwa gharama yoyote, lakini kwenye uhai wa Watanzania mnaona ni gharama kubwa?
Umeliweka hili vizuri sana na inashangaza na kutia aibu sana Taifa kwa watalaamu wetu hasa madakitari kukaa kimya Rais, asiye mtalaamu, anapotoa matamshi ya siyo na ushahidi wotewote. Rais ametoa mfano wa Chanjo iliyowafanya gumba watoto wa Kike wa miaka 14 wa nchi ambayo hakutaja ingawa hata watoto wetu walichanjwa wala hakutoa takwimu za nchi hiyo wala za kwetu. Kuna wakati WHO iliona Polio ilikuwa karibu kwisha kama Ndui ilivyokwisha kwa Chanjo kwa hiyo ilitoa chanjo kwa nchi fulani zikiwemo Nigeria na Pakistan ambazo zilikataa kupokea kwa sababu kama za Magufuli kwa madai kuwa dini yao ya Kiislam hairuhusu lakini muda mfupi Polio ililipuka kwenye nchi hizo tu lakini bahati nzuri nchi hizo ni za wasomi waliweka dini kando wakashrikiana na WHO ugonjwa ukaisha. Chanjo haitibu ugonjwa kama wajinga wanavyodhani bali inatoa Kinga kwa wazima ili wasipatwe na ugonjwa uliopo au unaoenea na kama sisi hatuna covid-19 na majirani zetu wote wanao, wajinga wetu wangetambua kuwa Chanjo inahitajika sana hapa ili tuendelee kuishi bila gonjwa hilo. Kuficha takwimu madhara yake ni makubwa sana kwa nchi ikiwa ni pamoja na uchumi wa nchi na wa raia mmojammoja kuvurugika kwa sababu maingiliano na watu wa nchi zingine kibiashara yanakoma kwani matamko ya majukwaani kuwa hatuna ugonjwa hayatoshi ndo maana wageni wote ambao lazima waje huvaa barakoa tusiwaambukize. WHO wamekwisha tangaza kuwa tujiandae kupokea mgao wetu wa Chanjo ili kutulinda na gonjwa kwa sababu ulimwengu wote unajua kuwa ugonjwa Tanzania upo sana na kama mwanachama wa WHO hawawezi kutuacha kwa sababu Rais ametamka. Tanzania ndo mwanachama wa WHO, siyo Magufuli wala Ngetti wala Meya wa Moshi, kwa hiyo nchi yetu itapata mgao kwa ajili ya wananchi wake kama nchi zote masikini hasa za Afrika, lakini kama hizo Chanjo zitatupwa ziwani na wajinga wetu ni juu yetu na WHO itaendelea kuwalinda majirani dhidi yetu.
 
Naona kama inatumika nguvu kubwa kwenye hizi chanjo.

Na hilo ndilo lengo lao kuu, wamepania kupiga hela ndefu kwa kupitia chanjo maana wanajua watu wote Duniani hatutakuwa na jinsi - wote tutalazimika kuchanjwa - Serikali za kiafrika zisipo kuwa makini zitajikuta zinabebeshwa mzigo mkubwa wa madeni kupitia mikopo ya Workd Bank - tukumbuke kwamba taifa ambalo linamiliki hisa nyingi za World Bank ni Amerika hivyo Taifa hilo ndilo lenye sauti kwenye taasisi hiyo, hivyo ni rahisi kutekeleza ajenda zao kupitia WHO (mfadhili mkubwa wa WHO ni Merikani), vile vile Majority ya Big Pharma companies zinazo tengeneza madawa na Chanjo zitakazo sambazwa na WHO Duniani kampuni hizo ni za huko Merikani - hapo unategemea nini?

Ndio maana mimi napendekeza kwa Serikali yetu kwamba kama kutakuwepo ulazima wa kufanya zoezi la kuchanja watanzania wote, basi salama yetu itatokana na chanjo zinazo zalishwa Uchina na Urusi mataifa haya hayana ajenda za siri za kutaka kupunguza idadi ya watu kwenye Dunia ya tatu kwa kupitia kwenye chanjo. My opinion.
 
Eti wangeleta TIBA badala ya chanjo msipende kudiscus mambo ya kitaalam ki siasa zaidi VIRUS vinakufa kwa dawa gani.?
Penguin talking rubbish! Waelewa wameelewa. Ukiona hujaelewa haikuhusu au ni level juu ya uelewa wako. Asiyejua maana haambiwi maana!
Huyu Bollen Ngetti ni yule aliyekuwa akitekwa uchao? Kama kuna wakunijibu, tafadhali fanya hivyo. Au yeye mwenyewe kwa ufupi atukumbushe madhila yake ya kutekwa na yameishaje kama yameisha. Kama ni yeye alikuwa anatekwa naona kazoea hiyo hali. Leo kajiteka!
 
Jamani mara hii mshasahau kua Mzee ndio aligundundua corona kwa Papai,Mbuzi na nk, pia lile sakata la vipimo feki na watu wake wa Maabara kuu ya Taifa kisha baada ya hapo tukaingia katika maombi na corona ikapotelea mbaaaali mmesahau tu...?! Hayaa mara tukaanza sikia mara India nao wamegumia vipimo vya Uchina kua ni fake akaja Museveni nae akatoa speech kama ya Mzee wetu. Hatukukaa sawa Taifa la KENYA ambalo lilionyesha dharau na kejeli hadharani dhidi ya kauli za Rais wetu hapo awali like Maombi ya siku tatu (3) na Mbuzi nao wanacorona nao wakatangaza Maombi ya siku tatu Kitaifa haikutupa shidaa mara paap!!!! Rais wa Marekani kipindi hiko Donald Trump nae akafuata kile Rais wetu alilitangazia Taifa kuhusu maombi kwa pamoja Wamarekani wakaingia katika maombi ya kitaifa, Kama watanzania tukaanza kummwagia sifa kedekede Rais wetu tukampa na majina kama Rais wa dunia, Mwenye maono na mengine mengiii Tanzania ikang'ara kimataifa na kuonekana kama sehemu salama zaidi kipindi hiki cha Mtikisiko wa covid19 duniani kwa ujumla. Hiki kipindi cha kwanza Tanzania tukavuka kwa usalama zaidi maana ya kua kila shughuli iliendelea kama ilivyo Ada. Awamu ya upili sasa imeingia naam, imeingia wakati ambao Dunia tayari imeshapata chanzo 4 mpaka 8 kwa taarifa zaidi huku company za utengezezaji wa chanjo hizo wakielezea kwa ufanisi namna ambavyo chanjo hizo zinafanya kazi yake katika miili yetu. Mara ameibuka tena yule tuliempa majina mengi ya kishujaa tena ya upekee kabisa akatia neno katika hizo CHANJO ZA COVID mzozo umeibuka ghafla huku kukiwa na taharuki kibao za tetesi ya virus vipya kuingia nchini mwetu, Muda huu Mzee anaonekana asiye faa kwa kauli yake ya kulihimiza Taifa kuhusu madhara ya kukimbilia chanjo mjadala umekua mkubwa mambo yanaongelewa mengi huku yakishika kasi kutia hofu ndani ya mioyo ya watu hii ni hatari kwa Taifa.

MWISHO: nimalizie kwa maswali FIKIRISHI ndani ya vichwa vyetu kama watanzania, Ni nini kilitufanya tukaamini hatuna CORONA na tuko salama kiasi tukaendelea kuchangamana mpaka sasa?!.... Je, mnakumbuka yale majeneza yaliyokua yanazikwa usiku, vipi?!.... Ile movie iliishia wapi baada ya msimamo wa serikali juu ya kua Taifa liko salama hivyo ikibidi yazikwe tu mchana. Na veepe! kuhusu watu waliokua wanaanguka pale Kariakoo haya mapicha yaliishia wapi?!..... AMANI IWE NANYI WANA JF nawasilisha.
 
unadhani hyo chanjo utapewa BURE?[emoji1787][emoji1787].
Amka wewe.
Hyo chanjo ni NA HELA SIO BURE.
WHO imetoa chanjo kwa AU ambazo itazigawa na Tanzania imo.
WHO inatupa chanjo, magari na wataalamu kila mwaka kwa sababu sisi ni wanachama wake.
 
Taasisi ya Haki za Binadamu, Tanzania Human Rights-Foundation (TAHURI) imetoa tamko la kuwataka Watanzania kuungana pamoja katika vita dhidi ya Shirika la Afya Duniani, WHO na Rais Magufuli huku likiwataka wananchi kumuunga mkono Rais wao.

Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Bollen Ngetti amesema;

"Tunaweza kutofautiana katika mambo mengi ya kiitikadi, kimtazamo na maono lakini katika mambo ya msingi kwa nchi kama hili la chanjo ni sharti tuungane kuwa kitu kimoja".

Aidha, Ngetti ambaye ni mwandishi wa habari nchini amesema Watanzania wasikimbilie tu athari za kiafya kwa chanjo hiyo na badala yake waangalie athari za kiuchumi.

"Tutambue kuwa dunia iko katika vitu kubwa ya kiuchumi. Kama Tahuri hatutajikita sana katika athari za kiafya za chanjo hiyo lakini tufikirie ni fedha kiasi gani chanjo hiyo itaswaga?"

"Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa WHO ili nchi za ki-Afrika kupata chanjo kutoka makampuni yaliyojiorodhesha kwenye mkataba wa COVAX ambayo ni BioNTech na Moderna itazigharimu kiasi cha Dola za Marekani kati ya 7-11 kwa chanjo moja".

Ngetti ameendelea kusema, "kwa Tanzania pekee kama Rais Magufuli ataruhusu chanjo itatugharimu Tsh104Trilioni kwa idadi ya watu wetu nchi nzima. Hii ni fedha nyingi sana kwa nchi changa kama sisi".

Ngetti amefafanua kuwa fedha hizo zitatakiwa kukopwa kutoka Benki ya Dunia kwa udhamini wa ADB na itachukua miaka zaidi ya kumi kuzirejesha kwa riba ya asilimia 7.2.

Aidha, Ngetti amehoji, "kama nia njema kwa nini wazungu wamekimbilia kutafuta chanjo badala ya tiba kamili? Walijua kwa tiba utahitaji dozi chache sawa na idadi ya walioambukizwa ambao kwa sasa ni milioni 100 lakini kinga utacheza namba ya watu duniani".

"Jambo la pekee kama Taifa tunalotakiwa kufanya ni kufuata masharti ya kujikinga huku tulifanya kazi kwa bidii, huu ni upepo unaovuma na kupita, tusiondoshwe kwenye reli".

Ngetti amemaliza kwa kusema, "Magufuli si kichaa, wala hana historia ya ukichaa, anatutakia mema tusimvunje moyo. Lakini pia wataalamu wetu nao wakeshe maabara kukuna vichwa aidha kuchunguza chanjo hizo au kugundua za kwetu kama Waganda wanavyofanya"

My Take: Kwa vita hii tutashuhudia na kusikia mengi. Vita hii ya Magu na wanasayansi itaibua makubwa. Subiri tuone!
Hivi huyu Bolen ngeti ndo yule iliye tekwa mala mbili na wale jamaa?
 
Eti wangeleta TIBA badala ya chanjo msipende kudiscus mambo ya kitaalam ki siasa zaidi VIRUS vinakufa kwa dawa gani.?
Wewe hata mzungu akisema umpe tako ili upone si utakubali na kusema ni Jambo la kitaalamu,
Tafutrni njia mbadala na si kufanyiwa biashara ya lazima.
 
KWani wewe una tatizo la corona au unalisikia redioni na TV , sasa unataka dawa? Wafie mbali huko!

In 1996, an outbreak of measles, cholera, and bacterial meningitis occurred in Nigeria. Pfizer representatives and personnel from a contract research organization (CRO) traveled to Kano to set up a clinical trial and administer an experimental antibiotic, trovafloxacin, to approximately 200 children. Local Kano officials reported that more than 50 children died in the experiment, while many others developed mental and physical deformities. The nature and frequency of both fatalities and other adverse outcomes were similar to those historically found among pediatric patients treated for meningitis in sub-Saharan Africa.[173] In 2001, families of the children, as well as the governments of Kano and Nigeria, filed lawsuits regarding the treatment. According to the news program Democracy Now!, "[r]esearchers did not obtain signed consent forms, and medical personnel said Pfizer did not tell parents their children were getting the experimental drug." The lawsuits also accuse Pfizer of using the outbreak to perform unapproved human testing, as well as allegedly under-dosing a control group being treated with traditional antibiotics in order to skew the results of the trial in favor of Trovan. While the specific facts of the case remain in dispute, both Nigerian medical personnel and at least one Pfizer physician have stated that the trial was conducted without regulatory approval.

Source: Pfizer - Wikipedia

Kibaya zaidi pamoja na rekodi yenye walakini miaka ya nyuma huhusu kampuni ya Pfizer linapokuja suala la chanjo, bado Kampuni hiyo inafanya lobbying ya hali ya juu kwa kutumia kitengo chake cha ushawishi to grease WHO officials ili chanjo za Kampuni za Pfizer na washiriki wake ndio zipewe kipa umbele kuenezwa Duniani as if Mataifa mengine haya zalishi chanjo - swali ni: Kwa nini chanjo zao zinapigiwa debe mno - kuna nini?
 
Yani toka korona imeanza hakuna utafiti wowote wa kitaalamu tumefanya na kutoka na majibu hadharani hata kuthibitisha tu kama huu ugonjwa watu wanaugua ama la. Cha ajabu tunaendeshwa na hisia na mawazo ya watu wasio na elimu ya afya kukataa chanjo ya ugonjwa. Tutoke basi na utafiti wa kitaalamu tuiambie dunia kwamba corona sisi hatuugui au tuwaambie tuna dawa yetu badala ya kutoa vijituhuma visivyo na ushahidi wowote. Kuongoza wajinga wengi raha sana jamani
 
Back
Top Bottom