Taifa la Israel halina uhalali wa kumiliki Gaza

biblia haijaacha kitu imeeleza wazi kabisa kati ya yakobo na esau kuwa wataunda mataifa mawili ambayo hayatakuja kuelewana hadi kiama na mdogo atakuwa na nguvu kuliko mkubwa,vita hii ilianza toka wakiwa tumboni mwa mama yao wallllikuwa wakipigana mpaka mama akajuta kwanini alibeba hiyo mimba
 
Hapa point yangu "wagalatia mnajipendekeza kwa miyahudi while wenyewe hawathamini" angalia sasa wakristo walivyo wachache kuliko hata waislamu


Kama hawamtambui yeye kama ni masihi, je, wanamtambua kama nani? Umeisikiliza hiyo clip mpaka mwisho?
Kaka unajadili hapa habari za nchi ya Israeli na bado hujaelewa punje? Hujajisomea hata kidogo?
Basi raia wa Israeli asilimia 20 ni Waisraeli Waarabu, yaani wajukuu wa wale Wapalestina ambao walibaki wakati wa kuanzishwa kwa nchi ya Israeli mwaka 1948. Hao Waisraeli Waarabu upande wa kidini wengi ni Waislamu, wengine Wakristo na Wadruzi.
Halafu asilimia 80 ni Waisraeli wale wanaoitwa "Wayahudi" ingawa si wote wenye dini.
Kwa hiyo ukiona namba hizo za "17.8% Muslim, 2.0% Christian" hazisemi chochote kuhusu uhusiano kati ya Wayahudi, Wakristo na Waislamu.
Kati ya hao wanaoitwa "Wayahudi" wako Wakristo wachache kutoka Urusi (kama 40,000), lakini si Waarabu. Walifika wakati Urusi ulianza kuruhusu watu kuondoka baada ya ukomunisti, na Israeli ilisema karibuni nyote wenye asili ya Kiyahudi (maana Wayahudi wa Kidini walibaki wachache mno baada ya miaka 60 za ukomunisti na sisasa iliyopinga dini yote). Katika kipindi kile walikuwepo Warusi walioona basi tuondoke hata kama hatuko Wayahudi, angalau tuweze kutoka Urusi iliyokuwa na hali mbaya sana kiuchumi. -- Wako pia Wayahudi wachache sana waliogeukia Ukristo.
Lakini uhusiano kati ya Wakristo na Wayahudi hautegemei swali kama wako wanaopenda kuhama.
 
Jamani, habari hizo zote kutoka Biblia hazisaidii kitu kuelewa hali ya nchi ya Israeli na haki za watu wake kulingana na haki za Wapalestina.
 
Hapa point yangu "wagalatia mnajipendekeza kwa miyahudi while wenyewe hawathamini" angalia sasa wakristo walivyo wachache kuliko hata waislamu


Kama hawamtambui yeye kama ni masihi, je, wanamtambua kama nani? Umeisikiliza hiyo clip mpaka mwisho?
Warumi 9:24-29 KJV -
24 ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia?
25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.
26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.
27 Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.
28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.

Wagalatia 3:7
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.

Warumi 9:6-8
6 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.
7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa;
8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.
 
Hapa point yangu "wagalatia mnajipendekeza kwa miyahudi while wenyewe hawathamini"
Kwamba Ukristo unategemea Uyahudi ili uendeleze huduma zake ama?

Kujipendekeza kuna maana pana kidogo.
Historia ya Ukristo inaanzia katika Taifa linaloitwa Israel na watu wa hilo taifa wanafahamika.

Ulitaka Ukristo ukajipendekeze Mexico au Argentina?
Come on you need to grow up!
angalia sasa wakristo walivyo wachache kuliko hata waislamu
Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi andika upumbavu uliouchora!

Hao Waislamu wa Israel 99% ni watu wa Taifa la Palestine eidha kwa kuzaliwa au kwa chimbuko wamo ndani ya Israel kwa sababu ambazo kila mtu anazijua.

Kama hawamtambui yeye kama ni masihi, je, wanamtambua kama nani?
Haijalishi wamtambue wasimtambue ni wao.
Tunachojua hawapo kutukana, kubeza ama kujikweza ili wao wainuke na wengine waanguke.

Uislamu upo ili ujikweze, ujibaraguze, utambe ili ukue kwa kutukana ama kubeza imani zingine.
Umeisikiliza hiyo clip mpaka mwisho?
Sifanyi hiyo kazi
 
Hujui historia
 
Kwani humu kuna Israeli au mpalestina? Wabongo kwa umbea ? Ww nchi za wengine zinakuhusu ni? Unakula vizuri? Unavaa vizuri? Kama una watoto wana soma vizuri? Hayo ndio maeneo yako na ya nchi yako.ndio maana wanafunzi wafundishwa elimu ya Tanzania na sio ya ujerumani haina impact kwa Taifa letu au Africa mashariki yetu
 
Hivi Nyerere alipokuwa akipinga udhalimu wa Israel dhidi ya Wapalestina alikuwa BEBERU!? Acha ujinga wa kuona dhuluma ya binadamu wenzako popote pale duniani haikuhusu wewe hata kuikemea kwa sababu tu ya rangi yako. BEBERUS duniani kote wanaopenda amani walipambana na makaburu wa South Africa ikiwemo kuwawekea vikwazo vikali vya kiuchumi ili kuhakikisha wanaachana na udhalimu wao na kuhakikisha Afrika Kusini wanakuwa uhuru.


Wewe mmatumbi pambana na hali yako, mambo ya Israel, Palestine achana nayo kama ambavyo wao hawajihusishi na yako. Acha kufia dini mlizoletewa na miarabu/mizungu kwa viboko na mijeredi.
 
Quran na hadith takatifu zinasema Wana wa Israel watarudi kwao Israel
 
Jamani, habari hizo zote kutoka Biblia hazisaidii kitu kuelewa hali ya nchi ya Israeli na haki za watu wake kulingana na haki za Wapalestina.
Ndivyo unavyofikiri, Biblia ni kitabu cha ahadi na unabii pamoja na mambo mengine. Mungu wa Biblia Yahweh aliwaahidi mababa wa Israeli kwamba amewapa eneo hilo kwa ahadi ya milele. Wakimkosea atawahamisha na kuwaondoa hapo ila ni kwa muda tu, baadaye atawarudisha. Kumkosea walimkosea, wakaabudu miungu na misanamu, kuwaondoa aliwaondoa. Lakini wengi wao aliwarudisha miaka takriban 450 kabla ya Kristo. Wakajenga hekalu upya lakini walikuwa chini ya Waajemi, baadaye Wayunani na mwisho Warumi (wakiwa na utawala wa ndani wakati wa Herode). Baadaye wakamkosea Mungu tena wakamuua Masihi. Mwaka 70 AD Warumi wakaja tena wakawahamisha na eneo lao lijabadilishwa jina na Warumi kutoka Yudea kuwa Philistine Asia. Jina Palestine lilianzia hapo, walibaki wahayudi wachache pamoja na Wagiriki wachache. Baada ya mwaka 600AD Waarabu walianza kutanua mipaka yao na baadaye wakaeneza dini ya Kiislamu. Kwa hiyo Wapalestina wa leo ni hao Waarabu wachache walioishi eneo hilo wakichangamana na Wakristo na Wayahudi. Huu mgogoro wa sasa ni tunda la dunia kukataa na kujaribu kubadili hiyo ahadi ya milele kwa Wayahudi kwenye eneo hilo.
Nilisemahapo mwanzo kwamba Mungu wa Biblia ni Mungu wa unabii: nabii zote zinazohusu siku za mwisho duniani hapa zinawaona wayahudi wakiwa na taifa lao na Yerusalem mji wao mkuu.
Sasa tunapata shida sana kwa kujaribu kwa nguvu zote kubatilisha ahadi ya Mungu kwa mababa wa Israel (Abraham, Isaka na Yakobo ndio Israel). Hakuna nguvu, hata dunia yote ikiungana hatuwezi kuwatoa hao jamaa Yersalem. Sio kwa sababu ni wakali wa vita ila tutakuwa tunapingana na ahadi ya Mungu pamoja na neno la unabii. Ninafahamu wapo ambao haya niliyoandika hawayaamini - na ndio chanzo cha shida zote hizo zinazotokea Palestine leo. Ningetamani Dunia yote ingekubali kwamba Mungu ndio mtawala ana haki kumpa mtu yoyote eneo atakalo yeye Mungu. Sisi tukipinga tutakuwa tunapiga mateke mchongoma. Wenye masikio ya kusikia na wenye hekima wanaojitakia amani wao na watoto wao huiombea Israel amani na ustawi. Kwa sababu huwezi kumlanii mtu ambaye Mungu amembariki na tena "hakuna uchawi juu ya Yakobo".
 
Hata Afrika, hapa kwenyu mipaka tu ilichorwa, hakukuwa na nchi bali ni jamii za kutangatanga, kuja na kuondoka. Mkoloni alipokuja ndio mababu zetu wakawa 'trapped' sehemu walijipata ndani na kuwa wa sehemu hizo aka nchi permanently hadi wewe na mimi kujipatia hapa tulipo. Hivi waweza pata upo Tz lakini wakichunguzwa uko wenyu freshi, labda unatokea Mogadishu... Maybe! 🤣 🤣 🤣
 
Hao jamaa(Israel), kulingana na elimu yangu, hawatolewi na mtu yeyote yule, isipokuwa Mungu, sasa waache wapigane ila ndo ivyo. Nchi ndogo ila ina nguvu usiyodhania.
 

Mkuu bora umeliona, japo tunatofautiana imani lakini umeonyesha utu na huruma kwa wapalestina. God bless you BAK!

Hii nyingine mtoto akimkimbilia baba yake kumuwaga baada ya kuuawa kwake dhidi ya waisrael. Mkuu nimetokwa machozi kuona hii video, na wengi imewaliza. Lakini nashangaa humu wanafurahia dhulma na mauwaji yanayofanywa na israel.

Hii hapa👇🏼




Wapalestina 69 wameuawa👇🏼
 
Lakini jamani hawa wapalestina wangeacha kurusha hayo makombora. Waache vinginevyo kwa ninavoona wayahudi hawamsikilizi yeyote wapalestina wataumizwa sana tukiangalia. Waambieni waache kurusha hayo makombora yao.
 
Lakini jamani hawa wapalestina wangeacha kurusha hayo makombora. Waache vinginevyo kwa ninavoona wayahudi hawamsikilizi yeyote wapalestina wataumizwa sana tukiangalia. Waambieni waache kurusha hayo makombora yao.

Watu wamevamia msikiti na kuwanza kuwarushia mabomu ya machozi na kujeruhi, utaacha kurudisha!!! Umeondokewa na wazazi, wakaka, wadada na watoto utakaa kimya!!!! Hata kama ni wewe huwezi vumilia haya mateso.
 
Watu wamevamia msikiti na kuwanza kuwarushia mabomu ya machozi na kujeruhi, utaacha kurudisha!!! Umeondokewa na wazazi, wakaka, wadada na watoto utakaa kimya!!!! Hata kama ni wewe huwezi vumilia haya mateso.
Kwa hapo kisasi kimeizidi akili, akili haitumiki kabisa. Wayahudi wameweka mitambo ya kugundua kwamba Kuna makombora yanakuja. Ving'ora hulia na watu wote hujificha. Makombora yakifika yataharibu miundo mbinu michache na kuuwa wachache wasiojikinga. Lakini hapo wayahudi wanapata sababu ya kushambulia maeneo ya wapalestina indiscriminately na bila huruma. Baya zaidi hakuna anayeweza kuinuka kwenda kuwapa msaada wapalestina kimapambano. Ni vikao viwili vitatu halafu maisha yanaendelea. Huku Palestinians wanapotezwa. Ushauri ni kuacha kuwachokoza wayahudi. Wapalestina watafute maisha mengine tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…