Nchi ya Israel ilianza mwaka 1948.
Historia ya Biblia ni kuhusu falme mbalimbali zilizopatikana na kupotea katika miaka 1000 KK hadi 70 BK.
Tena katika maeneo tofautitofauti mara kwa mara. (Umewahi kuanglia ramani za historia ya Biblia? )
Nchi ya kisasa iliundwa katika sehemu za maeneo ya falme hizo za kale, pamoja na maeneo ambayo hayakuwa kamwe ndani yake.
Lakini kuwepo kwa falme za kale miaka 2000 iliyopita haiwezi kuwa msingi kwa kutambuliwa kwa nchi za kisasa. Hata kama wahubiri wanadai ni vile.
Je Wamongolia warudi na kudai utawala juu ya Asia yote kwa sababu waliwahi kuitawala miaka 800 iliyopita?
Je Waturuki warudi na kudai utawala juu ya Afrika ya Kaskazini kwa sababu waliitawla kwa karne kadhaa??
Je Wahadzabe wadai Wabantu wote waondoke Tanzania na kurudi Kamerun kwa sababu hiyo ilikuwa nchi yao???
Nchi ya Israeli ilianzishwa kwa maazimio ya Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Hapo ndipo msingi wake na haki yake kuwepo.
Historia ya kale katika Biblia ina maana kubwa kwa maisha ya kiroho, haiwezi kuwa msingi kwa madai ya kisiasa ya leo
Sikutaka sana kuingia into details; alicho kisema bwn zitto Jr ndicho hsa historia ya taifa hili la Israel; iko hivi; baba wa taifa hili ndio hasa baba wa Waarabu (Iran, Iraq kwa asili sio waarabu) aliitwa Ibrahim baba yake akiwa mzee Tera, huyu mzee alibahatika kuzaa watoto wa kiume 3, wa kwaza akiwa ndio huyu Ibrahimu ambae ndie focal point ya mjadara huu; hawa watu walikua wenyeji wa nchi ya Uli ya Ukaldayo ambayo ndio Iraq ya leo, Ibrahimu katika kutafuta maisha alihamia nchi ya Caanan ambayo ndio hi inaitwa Palestina au Israel ya leo; mzee huyu aliingia hapo akiwa na mtoto wa mdogo wake anaitwa Lutu, hawa watu 2 walikua na mifugo yao mingi, yaelekea wenyeji wa hapo hawakua wafugaji kiviile kama hizi 2 people, wachungaji wa hawa ndugu 2 wakagombana huko machungani, mzee Ibrahimu akaona isiwe shida, dogo akahamia Sodoma wakati mzee akabaki hapo hapo Caanani/Palestina, kumbuka kipindi chote hiki huyu mzee Ibrahimu hakua na mtoto though alikua na mke, walihamia Misri kwa kukimbia njaa ilioibuka hapo mashariki ya kati, finally alirudi tena hapo this time akiwa na house girl wa Kimisri; miaka kadhaa baadae huyu mzee Ibrahimu alimzalisha huyu house girl wake mtoto wa kiume, huyu mtoto ndio alikuja kutengeneza mataifa 12 ya Kiarabu; miaka 12 baada ya huyu mtoto wa beki 3 kuzaliwa, mkewe Sara nae akashika mimba nae akaza mtoto wa kiume na huyu ndio hasa aliyekuja kutengeneza taifa la Israel na Jordan cause huyu mtoto wa mzee Ibrahimu kwa Sara mkewe alizaa mapacha, mmoja aliitwa Yakobo na mwingine Esau, huyu Esau ndiye hasa baba wa Edom (sasa Yordan/Jordan ) ingawa historia ya nchi hi ni uzao wa watoto wawili, mabinti wa Lutu wale waliozalishwa na baba yao na huyu Esau. Yakobo baadae alibadiri jina kutoka Yakobo kwenda Israel, huyu mwamba alipiga copy za kiume 12 na ndio hayo makabila 12 ya Israel ya leo, waliishi hapo baadae walikimbilia Misri kwasababu ya njaa na nabiii Musa kutoka kabila la Walawi ndiye aliowaongoza ndugu zake kurudi nyumbani though hakuwafikisha na ndipo Joshua kutoka kabila la Yuda ndiye aliyewafikisha hapo panapoitwa leo Israel/Palestina/Caanan; kumbuka haya mambo yametokea miaka zaidi ya 1000 kabla ya Yesu Kristo; wameishi hapo miaka na miaka, mara wapigwe na nchi jirani, sometimes walitekwa mateka baadhi ya vijana wao kwenda nchi zingine nk.
Now confusion inayokuja kuhusu mwaka 1948 iko hivi; kipindi Yesu anazaliwa, dunia ya wakati huo ilikua inatawaliwa na dola ya Kirumi (sasa ni Roman empire au Itali ukipenda) baada ya Yesu kwenda zake huko tunakosoma kwenye vitabu vya dini, hawa jamaa walivamiwa na kupigwa vibaya, wengi wao walikimbilia mataifa mbalimbali, wengine Italy, Africa (Africa hasa Ethiopia, kumbuka Ethiopia/Kushi ilikua na mahusiano ya kibiashara na Israel/mashariki ya kati siku nyingi) wengine walikwenda Asia na Amerika, i hope uliwahi kuiona ile movie ya Escape from Sobibo, inaeleza vizuri, is a true story but also tunasoma katika historia kwamba Hitler aliwaua almost Wayahudi 6,000,000, vita kuu ya pili ya dunia ndio iliwalazimisha wengi kurudi nyumbani hasa kutoka mataifa ya Ulaya, Wayahudi wengi waliobaki huko walikokua ni wale wa Amerika.
Kwa leo niishie hapo