Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Wapo wapi "Mystic figures" wa Kitanzania wakati huu?. Yapo wapi mafundisho na mafunzo ya kujitambua badala ya kutambulishwa? Wapo wapi watu watakaosaidia wasijua kusudi la uwepo wao kulijua kusudi hilo kama anavyofanya Sdhguru India?. Je tuna tayari wa kuwasikiliza?
Wapo wapi watu watakaofunua maarifa yetu kama walivyofanya "Toltec societies" . Yupo wapi mtu atakayesimama na kutumia ukweli kama "Don Miguel Ruiz" katika Kitabu chake cha " The four Agreement" na sasa "The five Agreement?".
Yupo wapi atakayetuambia tukaeiewa kuwa tunaouita uhalisia ni uhalisia uliochelewa "delayed reality" . Na tuapohisi tumekuwa jambo tayari tumeshachelewa?.
Ni muda wa juu sana sasa kurejea kwenye falsafa yetu ya "Ubuntu" lakini swali ni juu ya mfumo wa kifugwaji "domestication" ulioshika mizizi akilini mwetu utaondolewa na nani?. Anayeusema ukweli katika mawanda yasiyoonekana leo anaonejana amepagawa. Ni kama tunahitaji mtu mwingine atakayetufafanulia katika lugha yetu ya karibu juu ya kisa cha Plato Cha alichokiita " The Allegory of the cave".
Binadamu hajaamka bado kwa muda mrefu, anaishi katika ulimwengu wa ndoto "dream world". Naomba radhi kusema kuwa Watanzania wengi bado tupo kwenye ndoto zaidi na ni kama hatutaki kabisa kuamka.
Yupo wapi Mtu kama Paulo Freire atakayetuambia juu ya kuwa razini " Consipcientization". Yupo wapi atakayetuambia kuwa hata tunapohisi tupo razini Kuna viwango vya kuwa razini ili tupende kuamka zaidi na kutoka katika kiwango duni cha kujitambua "naive consciousness".
Mtu ni kama nguvu ya sumaku inayovuta vitu vinavyovutika kwake, na kwa hakika tumevuta nguvu hasi kwa kiwango cha juu sana, wapi wapi wa kutumia hili kwa lugha ya karibu na uelewa wetu wa kawaida?
Tunahitaji uwanja huru " neutral ground" usiofungamana na imani au itikadi yoyote na kuvuta umajui wetu pamoja wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule. Wanaopaswa kuandaa mawanda ya uwanja huru na maeneo huru " buffer zone" ni kama baadhi yao wamekumbwa na upepo wa maslahi binafsi " vested interests".
Taifa linahitaji watu aina ya Hobbes, John Locke waliojaribu kuelezea nadharia ya kusudi la Serikali kuwa ni kuweka utaratibu penye vurugu na kuepusha vita ya mtu dhidi ya mtu "to bring order out of chaos and escape the effect of war of all against all".
Nani atakayesimama na Azimio la Arusha kama Azimio muhimu kama anavyosimamia " Profes Issa Shivji licha ya wengi kusema limepitwa na wakati?. Ni wangapi tuna angalau nakala ya ufafanuzi wa Ujamaa na tunajaribu kuona Ujamaa wetu tulioasisiwa ni upi Ili tuone tofauti ya Ujamaa wa Kiafrika na Ujamaa wa ulaya?. Nani atakayetuambia kuwa Ujamaa ni moyo kama alivyotuambia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere?.
Bado tupo ndotoni tulio wengi na wanaozinduka ni kama wanarudi usingizini tena. Zipo wapi nyimbo za kuchukua hadhari "proactive measures" badala ya za kungojea matokeo "reactive measures".
Mungu atujalie nafasi nyingine Tanzania