Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Ukiona vyaelea ujuwe vimeundwa.tupo hapa tulipo tukiwa na utulivu wa kisiasa kwa sababu kuna watu walijitoa kwa jasho na Damu kulilinda ,kulipigania na kulitetea Taifa letu.tupo hapa tulipo kwa sababu kuna watu walitimiza vyema sana wajibu wao na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu badala ya matamanio yao binafsi.
Tupo hapa tulipo kwa sababu kuna watu waliamua kuilinda,kuitetea,kuihifadhi na kuilinda katiba yetu ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania dhidi ya wenye uroho na uchu wa madaraka.tupo hapa tulipo kama Taifa kwa sababu ya wazalendo ambao waliamua kwa jasho na Damu kulibeba Taifa letu katika mioyo ,vifua na Mabega yao.
Tupo hapa tulipo kama Taifa kwa sababu kuna watu waliamua kusahau na kuwa mbali na familia zao kwa ajili ya kupigania na kulinda maslahi ya Taifa letu. Ni uchapakazi wao, kujitoa na kujitolea kwao,uadilifu wao, uzalendo wao,uaminifu wao na kulinda viapo vyao kwa Taifa letu ndio kumefanya Taifa letu kuendelea kuwa lenye Amani,utulivu na usalama wa kutosha.
Watanzania tutambue ya kuwa hawa wazee wetu wameumia sana ,kuteseka sana ,kunusurika kifo na kupoteza Maisha yao kwa sababu ya kulilinda Taifa letu. Wamevuja jasho na Damu kutetea na kuilinda mipaka yetu. miili yao ilijaa na kuvuja jasho kwa ajili yetu watanzania. Hivyo hatuna budi kuwaheshimu,kuwaombea na kutambua mchango wao na uzalendo wao uliotukuka kwa Taifa letu ambao hakuna pesa ya aina yoyote ile na ya kiwango chochote kile inaweza kulingana na kujitoa kwao walikofanya kujitoa Maisha yao kwa ajili yetu.
Mungu wa Mbinguni aendelee kuwajalia Maisha marefu hawa Majenerali wetu.aendelee kuwapatia afya njema na uhai, kwa sababu ni hazina kwa Taifa letu na mawazo yao bado yanahitajika sana kwa Taifa letu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.