Taifa letu wapinzani kutekwa limekuwa jambo la kawaida kijana wa BAVICHA mkoa wa Mwanza amefikisha siku 15 na hakuna taarifa yoyote

Taifa letu wapinzani kutekwa limekuwa jambo la kawaida kijana wa BAVICHA mkoa wa Mwanza amefikisha siku 15 na hakuna taarifa yoyote

💭

Na hawa Wapinzani wa JF mbona huwa hawatekwi?

Kwasababu wanaishi kama ndege pori?
 
Hivi viongozi wa TISS huwa wanafikiria "intelligently" kweli?.
Au tumewapa kazi ya TISS watu wasio wazalendo?.
Nasikitika sana.
Na Mungu baba ashughulike na wale wote wanaoua na kuteka watanzania wenzetu.
NB: Uhai wetu u mikononi mwa Mungu.

Kuna hatari kubwa sana kwa nchi pale Majeshi yanapokuwa yemeunganishwa moja kwa moja na Siasa za nchi, na Watawala wa nchi kuyatumia Majeshi hayo katika kufanya Siasa za kuwadhibiti na kuwadhoofisha Watu wengine ambao wanaonekana kuwa ni Washindani wao wa kisiasa.
Ndio maana unaona kwamba UN imekuwa ikisisitiza na inaendelea kusisitiza kwamba Majeshi katika nchi ni lazima yawe na Nidhamu za Kijeshi, na lazima Majeshi hayo yawe 'neutral' kuhusiana na masuala haya ya Siasa.

Kwa bahati mbaya sana, kwa Tanzania mwiko huu umevunjwa kabisa. That's why unaona kwamba Usalama wa Umma/Wananchi ni Mdogo Sana kutokana na kushamiri kwa matukio ya Utekaji Watu
 
💭

Na hawa Wapinzani wa JF mbona huwa hawatekwi?

Kwasababu wanaishi kama ndege pori?
Wapinzani wa JF au Wapinzani wa mitandaoni huwa hawatekwi???
Are you serious???

FYI: Baadhi ya maiti za Watu ambazo zimekuwa zikiokitwa kwenye viroba huko mitaani kwenye mitaro ya maji, fukwe za bahari, mito, baadhi yao walikuwa watumiaji wazuri Sana wa mitandao ya kijamii.
 
It seems like you are among of the people with a short-sighted mind.

Tatizo hili la Utekaji watu na Mauaji lilianza hata kabla ya Magufuli hajazaliwa. Vitendo hivi vya Utekaji watu vilikuwepo Tz tangu zamani Sana enzi za Utawala wa Awamu ya Kwanza na hadi Sasa, na vitaendelea kuwepo hadi hapo chanzo chake kitakapokomeshwa kabisa.
Kwa hiyo ni halali utekaji iendelee??????!!!!!!!!🇹🇿🇹🇿🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸
 
Wapinzani wa JF au Wapinzani wa mitandaoni huwa hawatekwi???
Sikumumunya. Wapinzani wa JF
Are you serious???
Umeandika kwa hasira sana.
FYI: Baadhi ya maiti za Watu ambazo zimekuwa zikiokitwa kwenye viroba huko mitaani kwenye mitaro ya maji, fukwe za bahari, mito, baadhi yao walikuwa watumiaji wazuri Sana wa mitandao ya kijamii.

Niwekee taarifa yeyote kuthibitisha hayo madai yako hapo juu. 🙏

Zingatia: karibia watu wote waliokufa kuanzia miaka ya 90 kuja juu, kwa namna moja au nyingine, naamini walikuwa ni watumiaji wazuri tu wa mitandao ya kijamii. Nakusihi usiweke hoja hio katika jibu lako.
 
Kwa hiyo ni halali utekaji iendelee??????!!!!!!!!🇹🇿🇹🇿🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸

Ni halali ndiyo,. Mimi binafsi naona kwamba Utekaji Watu uendelee, LAKINI ni kwa wale Watu ambao tu kimsingi ITATHIBITIKA kwamba kuna ULAZIMA wa kufanya hivyo ili KUWEZA KULINDA na KUTETEA MASLAHI MAPANA ZAIDI YA WANANCHI/UMMA WA WATANZANIA, wala siyo vinginevyo. Katika kufanikisha suala hili, ni LAZIMA SANA Mamlaka za kutekeleza jambo hili zithibitishe uaminifu wake kwa umma pasipo kuacha hata chembe ya shaka. Mamlaka au Watu waaminifu Sana ndio wanaohitajika kwenye utekelezaji wa suala hili.

MUHIMU SANA KUFAHAMU:
Usifikiri kwamba Watu kamwe hawatekwi kwenye hizo nchi ambazo tunaamini kwamba zimeendelea na/au zina Demokrasia, la hasha! Huko Watu wamekuwa wakitekwa Kama hivi inavyofanyika katika nchi zetu hizi za kiAfrika, ISIPOKUWA ni kwamba, Mamlaka au Watawala wao ni WAAMINIFU SANA, kwa nchi nyingi za wenzetu ukiona mtu ametekwa ujue kwamba ni kweli kabisa kwa 100% alistahi au anastahili kufanyiwa hivyo na ilikuwa ni LAZIMA kwa Watekaji kufanya hivyo. Ni kwamba suala la Utekaji lilikuwa ndio suluhisho la mwisho kabisa katika kutatua tatizo lililojitokeza, na hapakuwa na namna nyingine mbadala ili kuweza kulinda maslahi mapana zaidi ya umma/Wananchi wengi zaidi wasio na hatia.
 
Hivi viongozi wa TISS huwa wanafikiria "intelligently" kweli?.
Au tumewapa kazi ya TISS watu wasio wazalendo?.
Nasikitika sana.
Na Mungu baba ashughulike na wale wote wanaoua na kuteka watanzania wenzetu.
NB: Uhai wetu u mikononi mwa Mungu.
TISS ya sasa inatoka UVCCM unategemea uzalendo gani hapo wao kazi yao kubwa ni kulinda chama na maslahi yake mambo mengine hamna
 
Kimsingi kama taifa timefikia pabaya sana ! Kupotezwa imekuwa jambo la kawaida na viongozi wa dini wamekaa kimya na watu wanaopotea mimi huwa sioni makosa yao
Hatuna viongozi wadini Tanzania, kuna viongozi wa taasisi kama tasiasisi nyingine tu za kawaida viongozi wote machawa wanatuma mawakala wao kwenad kuomba michango ya mambo yao wala si watu wakuwategemea kabisa kwani nao wanatafuuta fedha tu kama NGO nyingine tu. Hawezi kukemea mabaya kama Yesu alivyokuwa anafanya aliwakemea waziwazi mafarisayo na masudukayo wanafiki.
 
TISS ya sasa inatoka UVCCM unategemea uzalendo gani hapo wao kazi yao kubwa ni kulinda chama na maslahi yake mambo mengine hamna
Kwa hao Watu, wao neno Uzalendo wanalitafsiri kwamba ni kama 'kujiunga na kuwa mwanachama mtiifu wa CCM, sambamba na kuimba mapambio ya kuabudu na kuisifu Ccm na mambo yake yote.' Wao wanajua kuwa huo ndio uzalendo, tena wanaita kuwa eti ni 'uzalendo wa kiTanzania.'
 
TISS ya sasa inatoka UVCCM unategemea uzalendo gani hapo wao kazi yao kubwa ni kulinda chama na maslahi yake mambo mengine hamna
Je, tukiingia chadema madarakani ina maana tutawafukuza TISS wote kwasababu ni wa CCM?

chadema tutawezaje kulinda maslahi yetu? Manake hatuwezi danganyana na Sisi chadema hatuna maslahi.
 
Je, tukiingia chadema madarakani ina maana tutawafukuza TISS wote kwasababu ni wa CCM?

chadema tutawezaje kulinda maslahi yetu? Manake hatuwezi danganyana na Sisi chadema hatuna maslahi.
Kazi za Majeshi ya Serikali katika nchi yoyote ile hapa duniani ni kulinda maslahi ya Watu wote katika nchi bila ya upendeleo usio wa haki na bila ya
kuegemea upande wowote ule kisiasa.
Jeshi la Serikali ni LAZIMA liwe neutral ili kuhakikisha Usalama wa Watu wote kabisa waliopo katika nchi pamoja na Usalama wa mali zao.
 
Back
Top Bottom