Bila Makonda kukamatwa na kufikishwa mahakamani, yote yanayofanyika kuhusu haki, ni unafiki mtupu.
Nchi hii ni kama kuna watu wamepewa vibali vya kufanya uovu wa kila aina, hata kuua, kuteka watu na kupora mali za watu kwa namna watakayo. Halafu wapo watu wakifanya uovu hata mdogo sana, kwa unafiki mkubwa, wanachukuliwa hatua ili ionekane watawala wanachukia uovu, wakati kiuhaliasia wanapalilia uovu.
Makonda kuna ushahidi wa kila aina, mpaka Serikali ya Marekani ikaweka wazi kuwa mtu huyu anadhulumu haki ya watu kusihi (anaua), mpaka ikampiga marufuku kukanyaga kwenye nchi yao, halafu wajinga, punguani na wanafiki wakubwa utawasikia, eti kama mna ushahidi, mmpeleke mahakamani!! Punguani wakubwa nyie. Tangu lini mwovu wa makosa ya jinai anapelekwa mahakamani na raia? Hiyo ni kazi ya polisi. Katiba yetu imetoa mamlaka hayo kwa DPP pekee yake. Wananchi wengine wote uwezo wao kwenye makosa ya jinai, unaishia kuwa mashahidi lakini siyo kufungua kesi.