Nilitarajia jana ningemwona Rais wetu mpendwa akihutubia taifa na kutueleza nchi ilikofikia kimaendeleo, hasa ktk sekta ya Elimu ,Afya ,Ulinzi na Uchumi.
Hotuba ya Rais kuingia mwaka mpya huwa ni muhimu mno kuliko hata hotuba ya kila mwezi.
Bahati mbaya ni kwamba, tangu Rais Magufuli aingie madarakani zaidi ya miaka minne iliyopita hajawahi kuhutubia taifa, ni ajabu sana.
Hotuba ya Rais kwa taifa huondoa minong'ono na tetesi mbaya zinazokatisha tamaa kwa wananchi.
Hotuba ya Rais kwa taifa hujenga matumaini mapya kwa wananchi waliokata tamaa.
Sasa Rais wetu hajawahi kuhutubia taifa na inaonekana hana mpango huo.
Angeweza kuhutubia taifa hata akiwa Chato mapumzikoni, Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliwahi kuhutubia Taifa akiwa amelazwa Hospital nje ya nchi Uswisi.
Maneno ya Tundu Lissu yataishi hakika.
"Tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea ".
Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa sio presidential material. Get used to it