Taifa lipaze sauti kubwa Askofu Mwamakula aachiwe mara moja. Hakuna hatia aliyoifanya

Taifa lipaze sauti kubwa Askofu Mwamakula aachiwe mara moja. Hakuna hatia aliyoifanya

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Taifa zima lipaze sauti mpaka wanaofanya uonevu waone aibu.

Kuanzia Masheikh, Maaskofu na Wachungaji, Wafugaji na Wakulima, Wafanyabiashara na Wafanyakazi. Kesho kwa pamoja tupaze sauti kubwa Mtanzania mwenzetu mpenda haki aachiwe tena akiwa mzima wa afya.

Kuandaa maandamano ya hiari kudai katiba ni kosa? Maandamano aliyoandaa yanahatarisha amani?

Katiba ya JMT ibara ya 21(2) ipo wazi kila mtanzania anayo haki kushiriki masuala ya kitaifa ambayo yanamanufaa kwa umma.

Kwa kuandaa maanadamano ya hiari na ya amani kuna kosa?

Kama kuna hatari au uvunjifu wa amani, mbona hatujaambiwa kama taarifa za intelijensia zimebaini hatari yoyote?

Bishop Mwamakula aachiwe bila mashariti wala madhara.
 
Nchi za madictator kudai katiba ni kosa, ila kutaka dictator aongezewe muda wa madarakani kinyume na katiba ni sawa.
Taratibu, hapa hoja ya msingi askofu aachiwe. Akiwa salama bila mashariti.
 
Hana hekima kwa kudai katiba mpya? Wenye hekima ni wanaotaka rais aongezewe muda wa kukaa madarakani kinyume na katiba? Hapo Askofu ndio ameshatibua mahesabu yote ya kujiongezea muda wa kukaa madarakani. Mlitamani kusiwepo mtu wa kudai katiba mpya, ili muandae maigizo ya kujifanya mnamshinikiza jiwe aendelee kukaa madarakani,basi ile hoja iliyokuwa imefukiwa ya katiba mpya imefufuliwa tena.
Katiba mpya kwa manufaa ya kila Mtanzania
 
Hana hekima kwa kudai katiba mpya? Wenye hekima ni wanaotaka rais aongezewe muda wa kukaa madarakani kinyume na katiba? Hapo Askofu ndio ameshatibua mahesabu yote ya kujiongezea muda wa kukaa madarakani...
Askofu pamoja na hao wengine wanaoshawishi kumwongezea mtu muda hawana hekima.
 
Back
Top Bottom