Taifa lipo kwenye hofu kubwa, mnapopotosha umma ni kama mnachochea moto

Taifa lipo kwenye hofu kubwa, mnapopotosha umma ni kama mnachochea moto

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,772
Hakuna kitu kibaya kama hofu na tena hofu ya kufa. Kila Mtanzania sasa hivi ana hofu kubwa sababu hali ya huu ugonjwa unaoingamiza kwa hapa Tanzania hijulikani ipo katika level gani. Nasema hivyo sababu bado sijasikia toka kwa mamlaka husika kuwa maambukizi yanaaendelea kushika kasi? Yamepungua? Au yameisha?

Kwa hali kama hii inapotokea watu wananza kuendelea kutoa habari kuwa bado kuna watu wanakufa na kuzikwa usiku tena bila heshima na habari zenyewe hazijathibitishwa na wengine kuweka picha za watu wanazikwa ili hali sio hapa Tanzania sio jambo zuri.

Wengine wanaleta habari kuwa bibi zao wamezikwa bila heshima. Sasa kama hakuwa mgonjwa wa Covid -19. Kwa nini msiende kulalamika kwenye mamlaka za juu. Na ikibidi mfungue hata kesi.

Maana kuna watu wengi tunasikia wanapoteza jamaa zao na wanaruhusiwa kwenda kuwazika. Iweje nyie ndugu zenu ambao hawakuugua Covid -19 wazikwe na serikali!

Jambo la msingi tupo katika janga baya sana. Tuache upotoshaji na tuonyeshe uzalendo na Umoja.
 
Magufuli safari hii ajipange kiakili na "DUA/MAOMBI MABAYA DHIDI YAKE", kutoka kwa raia wanavyonyanyasika kila kukicha nchini.

Raia tumepitia mengi sana toka apewe madaraka. Ila hili la kutuua kwa "CORONA" kwa kuthamini "PESA kukiko MAISHA", na kutuficha ukweli kuhusu haya maambukizi kufikia hatua raia wanajisahau na kuona hali shwari, kumbe hali ndio inazidi kuwa mbaya sana.

Na kuishia kuzika ndugu zetu usiku wa manane, kwa kuwatupia kwenye mashimo (siwezi kuyaita makaburi yale) kama "WANYAMA/VIBUDU" bila kusaliwa wala kuoshwa wala kupewa heshima yoyote ya mwisho.

Viongozi wanashupalia "FANYENI KAZI, UCHUMI UTAYUMBA, TUTASHINDWA KUJENGA SGR" wakati wao wamekimbia ofisi zao kwa kuogopa COVID-19.

#Naamini mungu ataanza kuwanyoosha CCM popote mtakapojificha (kwa kuunga mkono maamuzi ya kipuuzi ya kutokufanya LOCKDOWN nchi nzima). Mungu amlaani yule aliethamini "WATALII" na hakuthamini "AFYA NA MAISHA YA RAIA (Watoto, Wajane, Wajawazito, Walemavu, Wazee na Vijana)".
 
We are on the right track
Screenshot_2020-05-02-11-04-10.png
 
Hii nchi mpaka ccm itoke ndio itakuwa vizuri. Halafu kuna watu hawafai kabisa kuongoza mfano mtu anajificha wakati ndio alihitajika zaidi yeye anavua samaki, jamani!
 
Magufuli safari hii ajipange kiakili na "DUA/MAOMBI MABAYA DHIDI YAKE", kutoka kwa raia wanavyonyanyasika kila kukicha nchini.

Raia tumepitia mengi sana toka apewe madaraka. Ila hili la kutuua kwa "CORONA" kwa kuthamini "PESA kukiko MAISHA", na kutuficha ukweli kuhusu haya maambukizi kufikia hatua raia wanajisahau na kuona hali shwari, kumbe hali ndio inazidi kuwa mbaya sana.

Na kuishia kuzika ndugu zetu usiku wa manane, kwa kuwarupia kwenye mashimo (siwezi kuyaita makaburi yale) kama "WANYAMA/VIBUDU" bila kusaliwa wala kuoshwa wala kupewa heshima yoyote ya mwisho.

#Naamini mungu ataanza kuwanyoosha CCM popote mtakapojificha (kwa kuunga mkono maamuzi ya kipuuzi ya kutokufanya LOCKDOWN nchi nzima). Mungu amlaani yule aliethamini "WATALII" na hakuthamini "AFYA ZA RAIA".
Laani hii iambatane na uchizi, utapiamlo wa akili na upofu wa macho.

Sema ameen.
 
Kwa hali kama hii inapotokea watu wananza kuendelea kutoa habari kuwa bado kuna wanakufa na kuzikwa usiku tena bila heshima na habari zenyewe hazijathibitishwa na wengine kuweka picha za watu wanazikwa ili hali sio hapa Tanzania sio jambo zuri.
Mtu akiamua kuficha jambo halafu mtu huyo huyo unataka akuthibitishie, hahahaa labda kama sio dunia hii!!!
 
Back
Top Bottom