Hakuna kitu kibaya kama hofu na tena hofu ya kufa. Kila Mtanzania sasa hivi ana hofu kubwa sababu hali ya huu ugonjwa unaoingamiza kwa hapa Tanzania hijulikani ipo katika level gani. Nasema hivyo sababu bado sijasikia toka kwa mamlaka husika kuwa maambukizi yanaaendelea kushika kasi? Yamepungua? Au yameisha?
Kwa hali kama hii inapotokea watu wananza kuendelea kutoa habari kuwa bado kuna watu wanakufa na kuzikwa usiku tena bila heshima na habari zenyewe hazijathibitishwa na wengine kuweka picha za watu wanazikwa ili hali sio hapa Tanzania sio jambo zuri.
Wengine wanaleta habari kuwa bibi zao wamezikwa bila heshima. Sasa kama hakuwa mgonjwa wa Covid -19. Kwa nini msiende kulalamika kwenye mamlaka za juu. Na ikibidi mfungue hata kesi.
Maana kuna watu wengi tunasikia wanapoteza jamaa zao na wanaruhusiwa kwenda kuwazika. Iweje nyie ndugu zenu ambao hawakuugua Covid -19 wazikwe na serikali!
Jambo la msingi tupo katika janga baya sana. Tuache upotoshaji na tuonyeshe uzalendo na Umoja.