Taifa Stars tafuteni kipa mahiri na siyo Manula

Leo nimeshuhudia mtanange baina ya Taifa Stars na Benin kupitia luninga. Kusema ukweli Taifa Stars wamecheza vizuri kuliko wapinzani wao aliyewaangusha ni kipa Manula. Namshauri Kocha wa Taifa Stars kutafuta kipa mahiri badala ya Manula. Kipa gani anashindwa kudaka mpira uliopigwa mita 30 kama ya leo. Wapo akina Kakolanya, Metacha, Mgore n.k. Kwa nini kila uchaguzi wa Taifa Stars kipa ni Manula?. Achaneni na Manula. Leo lawama lazima zimwendee kutokana na goli lililofungwa na Benin.
Naomba wachezaji wote watolewe kocha atafute wengine wanashindwa kufunga goli hata moja.
 
Wawaachie watoto wakina Soppu na mechack abraham,Ata huyo Msuva hakuwa na mchezo mzuri.Any way🙄
Kabisa kiongozi! Unajua nimekuwa nafuatilia kwa muda tu sijaona mshike mshike wa maana haswa unaoletwa na samatta katika taifa stars......ni mwendo wa kula vipigo tu huku tukiambulia makelele tu ya kabla ya mechi kutoka vyombo vyetu vya habari kuwa 'samatta ndani!' n.k
 
Acha ushabiki maandazi,ile goli la curve asifiwe mpigaji na siyo kumlaumu Manula.Bado manula ni kipa bora kwa sasa,afu kingine walaumu wale wachezaji walokosa nafasi nyingi za wazi na kiwango duni cha Poppa🤗
Simba ilivyo enda congo nyakati fulani manula aligungwa magoli ya namna hiyo mengi ufupi kutoka nje ya lindo lake huwa vinamgharimu sana
 
Leo nimeshuhudia mtanange baina ya Taifa Stars na Benin kupitia luninga. Kusema ukweli Taifa Stars wamecheza vizuri kuliko wapinzani wao aliyewaangusha ni kipa Manula. Namshauri Kocha wa Taifa Stars kutafuta kipa mahiri badala ya Manula. Kipa gani anashindwa kudaka mpira uliopigwa mita 30 kama ya leo. Wapo akina Kakolanya, Metacha, Mgore n.k. Kwa nini kila uchaguzi wa Taifa Stars kipa ni Manula?. Achaneni na Manula. Leo lawama lazima zimwendee kutokana na goli lililofungwa na Benin.
Kuna Watu wenye Akili tukiwa tunawadharau na Kuwaiteni Wapumbavu msiwe mnakataa au mnakasirika.

Kila Mtu kaona kuwa Mabeki Bakari Mwamnyeto na Dickson Job ( Wote kutoka Yanga SC ) ndiyo walishindwa Kukaba ( Kumkaba ) Mfungaji na akafunga ila huwasemi hawa unakimbilia kumsema Kipa Aishi Salum Manula ( Tanzania One ) kutokea Simba Sports Club.

Huyu huyu Kipa Manula usiyempenda na unayemchukia kwakuwa ni wa Simba SC na Wewe ni mwana Yanga SC ndiyo ameisaidia vilivyo Taifa Stars ( hasa Kimafanikio ) kwa kuokoa Michomo hatari kiasi kwamba hata huko CAF ameshatajwa kuwa ni miongoni mwa Makipa Watano Bora kwa sasa ndani ya Bara la Afrika.
 
Simba ilivyo enda congo nyakati fulani manula aligungwa magoli ya namna hiyo mengi ufupi kutoka nje ya lindo lake huwa vinamgharimu sana
Congo ya wapi hiyo?
Simba alivyoenda alifungwa goli nyingi za mbali?
Simba alivyoenda alifungwa goli nyingi za vichwa na kona ,si mipira ya mbali.
 
Beki zenyew Zilikuwa zimesimama Kama wote namba nne hakukukuwa na kiongoz pia manula nae haya magoli hajaanza Leo kufungwa huu mtindo wake wa kutoka golin unamgarimu
 
Kuna Watu wenye Akili tukiwa tunawadharau na Kuwaiteni Wapumbavu msiwe mnakataa au mnakasirika.

Kila Mtu kaona kuwa Mabeki Bakari Mwamnyeto na Dickson Job ( Wote kutoka Yanga SC ) ndiyo walishindwa Kukaba ( Kumkaba ) Mfungaji na akafunga ila huwasemi hawa unakimbilia kumsema Kipa Aishi Salum Manula ( Tanzania One ) kutokea Simba Sports Club.

Huyu huyu Kipa Manula usiyempenda na unayemchukia kwakuwa ni wa Simba SC na Wewe ni mwana Yanga SC ndiyo ameisaidia vilivyo Taifa Stars ( hasa Kimafanikio ) kwa kuokoa Michomo hatari kiasi kwamba hata huko CAF ameshatajwa kuwa ni miongoni mwa Makipa Watano Bora kwa sasa ndani ya Bara la Afrika.
Sasa wewe una tofauti gani na hao mashabiki wa Yanga wanaomponda Manula mbona na wewe ni hivyo hivyo tu.

Lazima ifike mahali tukubali kwamba Tanzania mpira wetu ni mdogo na tunacheza sana kwenye vyombo vya habari na ujio wa hawa wachezaji wa kigeni ndio utatumalizia kabisa mpira wetu.
 
Back
Top Bottom