Taifa Stars tafuteni kipa mahiri na siyo Manula

Taifa Stars tafuteni kipa mahiri na siyo Manula

Anapenda Sana sifa na kupambwa na media anajua sifa ni kufungwa Tu hatoi pasi Kwa wakati wenzie wanafungua space anaforce apige golini utafikiri mchezaji wa toto African
 
Leo nimeshuhudia mtanange baina ya Taifa Stars na Benin kupitia luninga. Kusema ukweli Taifa Stars wamecheza vizuri kuliko wapinzani wao aliyewaangusha ni kipa Manula.

Namshauri Kocha wa Taifa Stars kutafuta kipa mahiri badala ya Manula. Kipa gani anashindwa kudaka mpira uliopigwa mita 30 kama ya leo.

Wapo akina Kakolanya, Metacha, Mgore n.k. Kwa nini kila uchaguzi wa Taifa Stars kipa ni Manula?. Achaneni na Manula. Leo lawama lazima zimwendee kutokana na goli lililofungwa na Benin.
Manula hajawahi kunivutia huenda anatumia ushirikina ila sio kipa mzuri kuliko wote
 
naona kwenye kiwango mmeshindwa mmeingia kwenye ushirikina. Utopolo mnawaza kuroga tu. Kama hana uwezo aliwezaje kuwa kipa bora kwa miaka 7. Wewe ni nani ikiwa CAF wanatambua Manula ni kipa bora
Hana lolote atazidi kuzigharimu timu anazozidakia. Kipa bora hawezi kuwa anafungwa mabao ya aina ileile kila match
 
Congo ya wapi hiyo?
Simba alivyoenda alifungwa goli nyingi za mbali?
Simba alivyoenda alifungwa goli nyingi za vichwa na kona ,si mipira ya mbali.
Unazungumzia mechi ipi? Na walitoa goli ngapi kwa ngapi
 
Wachezaji woote wa uwanjani wamepitwa kizembe alafu lawa ziende kwa kipa,kwa uli mpira uliopigwa kuwa goli ni kipa ganimwa Tanzania angedaka?
 
Wabotswana wakiangalia udakaji wa Manula wanacheka sana
 
Mi naona tz tunapanda kiwango ila polepole sana
Watu kama wakina ajibu wangekua serious sahv wangekua wanaleta difference kwenye timu ...wakina mkude nao ndo hvo

Upande wa mwenda simlaumu sana ila alieingia baada yake ndo aliharibu zaidi maana goli lilitoka kwake
Mo hussein ni mtu wa maana sana yule

Aishi simlaumu asee lile goli linafungwa na yeyote sina sababu kwa kweli ya kumlaumu maana amesave sana mipira kabla na baada ya pale

Msuva aaaaaaaah msuva sema wanasema haukua mguu wake ule yeye anatumia wa kulia so ndio alikosa open chance lakini ilikaa vibaya kwake afu pia yule beki wa benin akili kubwa aliendelea kwenda hakukata tamaa hata baada ya kipa kupitwa na msuva

Fei toto anajua ila exposure inahitajika zaidi kwa yule kijana
Sijui simba tumbebe nini?? Awe anaingia dakika za mwisho mwisho caf champions kujaza eksipiriensi yake kwa ajili ya taifa[emoji23][emoji23][emoji23] maana hawa wenzetu wamekalia kutafta njia zao mpya za kuingilia kila uwanja[emoji23][emoji23][emoji23]

Pale kwenye kiungo yule namba 20 asingetoka alikua anaweka tempo ya mpira fresh sana labda kama aliumia ila kama ilikua ni kiufundi tu basi walikosea mimi naona

Kuhusu samatta mimi naona kajitahidi atleast asee sio kama zamani he was waaay worse than last match ila poppa nae alipoteza mpira sana final third kama rookie hv kumbe veteran kabisa

Kibu naona alipaswa aanze na boko asingetoka maana yule lusajo ni mgeni kwenye haya mambo na uzoefu kwenye michuano kama hii ni muhimu so bora tu boko angebaki maana hakuna differrence yoyote kwangu alivotoka

Kwa kumlizia naona kama tushatoka hivi....sijui lakini lakini naona tujaribu tu kwengine maana sare tu ingefanya tuwe watu watatu tupo sawa

Nakaribisha maoni na ukosoaji[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Back
Top Bottom