Taja jina la shule ya msingi uliyosoma enzi hizoo

Taja jina la shule ya msingi uliyosoma enzi hizoo

Hebu tuzikumbuke Shule zetu za msingi tulizosoma miaka hiyo na Jambo gani ambalo hutalisahau?

Aidha si vibaya ukasema ulikuwa unashika Nafasi ya ngapi.

Karibuni!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kipumbwi primary school, namba wa kwanza, head teacher = Andalu. Sitasahau nilipotaka kuadhibiwa kwa uonevu wa mwalimu, sijui ni kitu gani kilitokea lakini banda la mbuzi wa shule lilishika moto hivyo adhabu haikufanyika!
 
Kitangili s/msingi Nzega.

Namkumbuka mwalimu Kagenzi-english darasa la tatu tulimwita "mwalimu that is ittttts".

Pia mwalimu Joel Kigatta-hesabu farasa

Sent by Nokia E5 using Jamii Forums mobile app
 
Hili jina geni kwangu labda kama iliwahi kubadilishwa jina. Kwa niijuayo mitaa hiyo ni Kilimanjaro International School, Kilimajaro Primary School??

Hii ni shule ya miaka mingi mkuu na kama umewahi kuishi moshi shanty town karibu na CCP utakuwa unaijua .Mimi nimeanza pale 1981 na nikatoka 1987 mpaka leo ipo na jina lake ni hilo hilo,Ilikuwa inashindana sana na Kibo Primary school
 
mhn! kama naingia woga hivi? isije ikawa watu wanatafutwa! ilianza ulisoma sekondari gani o-level baadaye zinakuja private msg hivi wewe sio fulani sasa hapa ndo panitisha wakiunganisha dot lazima wakupate
 
KITANGIRI PRIMARY SCHOOL 2000-2006
MWANZA

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
Idetero primary school ! nimewah kuwa no 11 darasa la 3 niliugua sana pumu kwa miez 5 nyumbani! lakini miaka yoote nilikua namba 1/2! standard seven tulifaulu mimi na kaka mmoja anaitwa Fred! nilikua naongoza kiwilaya ! asante Mwalimu NDELWA!
Ndio maana nasema we ni binti yangu naijua hiyo shule ipo karibu na Mtwango kwetu
 
shule ya msingi Yamu-kirua vunjo, katika kipindi chetu tulitembelewa na wageni wa serikal,mama zakia megji, pr sarungi na mkuu wa mkoa kipindi hicho. tulipewa nguruwe wa mradi
wakati fulani zilipita parachut 2 mwalim mkuu akagonga kengele ishara ya kitu chaajabu ambacho hakijawai kushuhudiwa na mtu yoyote, tulijificha chini ya madawati na waalimu.
 
Hii ni shule ya miaka mingi mkuu na kama umewahi kuishi moshi shanty town karibu na CCP utakuwa unaijua .Mimi nimeanza pale 1981 na nikatoka 1987 mpaka leo ipo na jina lake ni hilo hilo,Ilikuwa inashindana sana na Kibo Primary school

Ok, ok, nishaikumbuka imejificha sana, kwenye kona ya kwenda KCMC kama unatokea keep-left cha YMCA?? yenyewe unanyoosha kidogo kama unaenda Shanti hivii....!!
 
Back
Top Bottom